Moyo wa mtu ni kichaka

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,778
Habari za Ijumaa wapendwa, basi leo nina tukio lilompata shost wiki hii.

Shost yangu Lilian anafanya kazi katika moja ya mashirika ya umoja wa mataifa, yeye alikwenda shule vizuri. Liliana anaishi Upanga katika nyumba za National Housing, yeye ni katika wale wanaopenda kuishi katikati ya jiji. Liliani nyumbani anaishi mwenyewe, dada wa kazi anakuja Monday - Friday, 08:00-16:00.

Lilian hana mume wala mtoto, katika maisha haya haya tunayoishi wewe na mimi, alikutana na kijana anaitwa Tony, Tony ni wale watu wa kuangalia fursa, Tony alimaliza Chuo cha Uhasibu kurasini na ni mwajiriwa, lakini mpaka anakutana na Lilian alikuwa anaishi kwa rafiki tena alikuwa analala sitting room.

Baada ya Tony kukutana na Lilian na kuanza mapenzi angalau alianza utaratibu wa kwenda kwa Lilian kila weekend, aliona aibu hata kusema anaishi wapi, lakini watoto wa mjini wanajua kuishi kijanja.

Tony alipata safari ya kikazi, alimuaga Lilian kuwa huko aendako atakaa wiki moja lakini babe uje nipokee airport wakati ninarudi, basi Liliani alikwenda kumpokea babe wake, kutoka airport Tony alimwambia Lilian amemiss sana wakapumzike kwanza Upanga mpaka kesho yake ndiyo atafikiria kwenda kwake. Khe basi ndiyo ikawa kesho yake, kwake akafuate nini wakati alikuwa na sanduku lake pale. Kumbe alisha plan jinsi ya kumove in bila Lilian kujua.

Kuishi pamoja sasa, anaweza amtumie whatsup message Lilian babe how was your day, ohh I'm home already but baby don't forget to buy a bread for tomorrow. Hali hii ilimfanya Lilian ajiulize, huyu mwanaume nikizaa nae si nitalea watoto wawili? Aliamua kutumia family planning wakati akisoma nyakati.

Kuna wakati Tony alikwenda kwao huko likizo, alikuta familia moja ina binti amefaulu form IV kwenda form V lakini familia ile haikuwa hata na uwezo wa kumfanyia binti shopping. Hii ilikuwa ni siri ya Tony kama alimpenda yule binti au aliona fursa, lakini aliwaambia wazazi atagharamia kila elimu ya yule binti.

Tony alijitwisha gharama zote za kumsomesha Angela, kwa matarajio ya kumoa amalizapo shule. Angela alisoma na kufaulu vizuri kidato cha sita, alipata nafasi ya kujiunga na chuo cha usimamizi wa fedha mjini Dar.

Basi Tony alimsomesha Angela kuwa wewe mimi ninaishi na huyu mwanamke lakini sina mpango nae, kwahiyo wewe unakuja Dar, utaishi hapa lakini kauka. Masikini Angela ameingia jiji la Dar kwa mara ya kwanza ndiyo anakutana na hali hiyo. Liliani alitambulishwa kuwa Angela ni binamu wa Tony mtoto wa shangazi kabisa. Lilian alimpokea Angela kwa kumfanyia shopping kwanza ili angalau afit in na wanafunzi wenzake chuoni.

Angela aliamka asubuhi akadeki nyumba yote, alimtengenezea Lilian toast na kuhakikisha chai iko mezani saa 12:30 asubuhi. Kwakweli Lilian mwanzo alitaka Angela akapangishe chumba akishazoea mji, lakini kutokana na tabia yake aliamua kumwachisha kazi msichana wa kazi na ile pesa ya mshahara wa dada ampe Angela imsaidie. Jumamosi Angela alifua na kupiga pasi nguo zote pamoja na kupika.

Kwa kweli Lilian alijituma sana kazini, kiasi cha kuaminiwa sana, alisafiri kila mkoa wa Tanzania na mara nyingi akiwa kiongozi wa msafara. Huku nyuma aliwapa nafasi nzuri Tony na Angela kuenjoy mapenzi yao.

Siku moja Lilian aliondoka asubuhi na aliwaaga kabisa kuwa ile siku walikuwa na safari ya kwenda Mkuranga. Angela hakuwa na darasa siku ile, na Tony alikuwa likizo, basi baada ya Lilian kuondoka, Angela alianza kazi zake za ndani, alisafisha nyumba, alianza kuchemsha maharage, alipika mchuzi wa nyama, basi akiwa anakuna Nazi aunge maharage Tony alimwita chumbani.

Kumbe masikini Lilian kule alikokuwa si kichwa kilianza kuuma vibaya sana, ilibidi watafute maarifa ya kumrudisha mjini, hali yake haikuwa nzuri kabisa. Amefika nyumbani anakuta mbuzi na Nazi viko jikoni, maharage bado ya moto, TV sitting room inawaka lakini hakuna watu, jamani hawa watu wako wapi, alianza kuita.

Sasa wale wezi hawawezi kukaa chumbani siku nzima, ilibidi tu watoke, wametoka Lilian hakuamini alichokiona, eti Tony anaomba msamaha, Liliani aliwafurumusha wote.

Majina niliyotumia katika kisa hiki ni ya kubuni, ninaomba msamaha kwa yeyote nitakae kuwa nimemkwaza kwa kisa hiki.
 
Habari za Ijumaa wapendwa, basi leo nina tukio lilompata shost wiki hii.

Shost yangu Lilian anafanya kazi katika moja ya mashirika ya umoja wa mataifa, yeye alikwenda shule vizuri. Liliana anaishi Upanga katika nyumba za National Housing, yeye ni katika wale wanaopenda kuishi katikati ya jiji. Liliani nyumbani anaishi mwenyewe, dada wa kazi anakuja Monday - Friday, 08:00-16:00.

Lilian hana mume wala mtoto, katika maisha haya haya tunayoishi wewe na mimi, alikutana na kijana anaitwa Tony, Tony ni wale watu wa kuangalia fursa, Tony alimaliza Chuo cha Uhasibu kurasini na ni mwajiriwa, lakini mpaka anakutana na Lilian alikuwa anaishi kwa rafiki tena alikuwa analala sitting room.

Baada ya Tony kukutana na
Malizia story kwanza basi
 
Internet imekata sijui au bando ndiyo kwishineiiii..........!!!!! au nawe tukupe pesa ya Juice......... uanzishe whatsapp group lako? kwa maana mwaka huu tusio na pesa tutakosa vingi vitamu kwa wakati kweli
 
Sky una story!

Most of the time, kama umempenda mwenzako kwa dhati na upendo unatoka moyoni, halafu mwenzako yupo na wewe kwa malengo yake mwenyewe, ukweli hudhihirika ili wewe uamue kwendelea au kupotezea.
 
Mkuu inauma, na hawa vijana watafuta fursa hawajali hata kukuambukiza magonjwa mradi yake yaende.
 
Back
Top Bottom