Habari
Najua sikupaswa kupost hapa lakini namna navyojisikia anaeelewa ni Mungu pekee, nipo ndani na mwanangu nimelia sana nahisi nakosa control hadi mtoto naye analia, nikaona acha nipost Jf yamkini nikakaa sawa
Tumekuwa na mgogoro mwaka sasa ndani ya ndoa uliopelekea kutengana japo si kisheria
Si mgogoro mzito kwa watu wenye kuijua thamani ya ndoa mana ni miss understanding za kawaida hasa kwa sababu tumetofautiana kimitazamo kimalezi na hata mazingira tuliyokulia.
Nimekaa kimya mda mrefu sijamtafuta mwenzangu mana alisema niachane naye nisimtafute leo nikamkumbuka sana sababu ni mwanaume nayempenda kupita kiasi nikapiga moyo konde nisimtafute but hisia zikazidi akili nikampigia kama mara 7 hakupokea, nikamtext kumplease tuongee tofauti zetu kwa mara nyingine ikiwezekana tujirekebishe tuendelee na maisha.
Katika kuchart chart nikawa najaribu kujishusha nambembeleza tu yaishe akanitumia hii sms iliyolowanisha moyo wangu kwa machozi
Nanukuu
"" "
Hata hivyo, najua unaning'ang'ania kwasababu una maisha magumu, laiti ungekuwa na maisha mazuri, tusingesumbuana hapa kila leo. Nakuombea Mungu akupe maisha mazuri ili tuache kusumbuana, "
Nimehisi kama moyo unapasuka kwa sms hii, kiukweli sina maisha magumu kama nilivyoambiwa angalau naweza kula vizuri kuvaa mimi na mwanangu na mambo mengine mengi ila nishaambiwa maisha magumu ndo yanapelekea nimsumbue kutaka kuelewana.
Naombeni mnifariji mana moyo unabubujika machozi nimelia sana kwa maneno hayo toka kwa mume
Sent using
Jamii Forums mobile app