Moyo Ulioonja Maumivu

Mtunzi Nyemo Chilongani sehemu ya 01


Gari aina ya Lamborghini Centenario LP 770 nyekundu yenye thamani ya zaidi ya dola laki tano ambazo zilikuwa ni zaidi ya bilioni moja lilisimama nje ya Ukumbi wa Mlimani City uliokuwa jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari waliokuwa mahali hapo kwa ajili ya kuripoti Mashindano ya Miss Tanzania wakaanza kulisogelea gari hilo huku wakiwa na kamera zao mikononi mwao.

Walimfahamu mtu aliyekuwa ndani ya gari hilo, walihitaji kupata picha kadhaa kwa ajili ya magazeti yao, tovuti na hata mitandao ya kijamii.

Hata kabla ya mtu kuteremka, wakaanza kupiga picha mfululizo, hakukuwa na mwandishi aliyekuwa radhi kuondoka mahali hapo, kila mmoja alihitaji kupata japo picha moja tu ya sura yake.

Baada ya kukaa kwenye gari kwa sekunde zaidi ya hamsini, hatimaye mlango ukafunguliwa na msichana mrembo, mwenye sura nyembamba, mrefu na kidoti pembeni ya pua yake, akateremka na kutoa tabasamu pana.

Alivalia gauni refu jekundu la kumeremeta mpaka chini, viatu vilivyokuwa na visigino virefu, shingoni alikuwa na cheni ya kike iliyoonekana kuwa ya dhahabu kabisa huku kwenye mkono wake wa kushoto akiwa na saa ya thamani aina ya Rolex aliyoinunua nchini Ufaransa alipokuwa akiishi.

Msichana huyu aliitwa kwa jina la Violeth Joseph Zilikana. Alikuwa mmoja wa wanawake waliokuwa na uzuri wa ajabu nchini Tanzania.

Alikuwa maarufu na aliyekuwa na pesa nyingi, alikwenda sehemu yoyote aliyotaka duniani, alipewa mialiko mingi kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kazi ya mitindo aliyokuwa akiifanya.

Umaarufu wake ulikuwa mkubwa mno, alijua kupendeza, watu wengi walimpenda na kutamani sana kuwa naye lakini kwa sababu mume wake alifariki dunia, hakuwa tayari kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yeyote yule.


View attachment 944998
Jamani mbona hukunitag mrembo...... Shunie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom