Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

Hatimae nimewafikia...

Mtongozo wa Theo si wa nchi hii, Violeth anajipeleka machinjioni mwenyewe..
....namuona anajaribu kusikiliza na nyimbo zake eti...hahahaha atajuta kudate na staaa
 
Asante shunie.kupendwa raha basi tu. Unakuwa unajisikia furaha kila wakati.ila hapo kuna mmoja ataumizwa
 
SEHEMU YA 22

Msichana huyo akateremka, Theo alibaki ndani ya gari akimwangalia. Alimpenda, kwa jinsi alivyoonekana, alimchanganya kupita kawaida. Violeth alitembea kwa mwendo wa kawaida kwenda ndani, Theo aliyebaki ndani ya gari alitamani kuwasha taa na kumwangalia msichana huyo lakini alishindwa kufanya hivyo.

Baada ya kuhakikisha ameondoka, alichokifanya ni kuwasha gari lake na kurudi nyumbani kwake. Njiani, moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakuamini kama kweli msichana huyo alikubali kutoka naye mtoko na kwenda kula chakula cha usiku, alifurahi kama mtu aliyeshinda mamilioni ya pesa.

Alipofika nyumbani, kama kawaida yake kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu msichana huyo na kuanza kuongea naye. Alichokihitaji ni kumuweka karibu, asiwe na muda wa kumfikiria mwanaume mwingine zaidi yake.

Huo ndiyo ulikuwa muendelezo wa ukaribu wao, japokuwa Violeth alifika nchini Tanzania kwa lengo la kushiriki katika Mashindano ya Urembo wa Tanzania lakini hakutaka kuondoka kurudi nchini Ufaransa.

Theo alimchanganya mno, alijisikia amani kuwa naye karibu, kila wakati mwanaume huyo alimjia kichwani mwake. Alijua kupenda, kumjali na kumfanya kujisikia kuwa mwanamke aliyekuwa na bahati katika dunia hii.

Ukaribu wao ukawafanya waandishi kuandika sana kuhusu wao lakini Violeth alikataa kwa nguvu kubwa tena huku akimwambia na Theo naye akatae kwani alijua kwa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa akimpenda, ilikuwa vigumu sana kukataa kama kweli hawakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Siku zilikatika tu, na baada ya miezi miwili ndipo msichana huyo akaamua kuondoka kurudi Ufaransa. Theo hakutaka kuona akienda peke yake, kwa kuwa alimpenda aliamua kumsindikiza mpaka huko na kufika nyumbani kwa Violeth.

Waliyafurahia maisha na kwa mara ya kwanza wakabusiana midomo, na baada ya dakika kadhaa wakawa kitandani na kuanza kufanya mapenzi. Moyo wa Theo uliridhika, hicho ndicho kitu alichokuwa akikihitaji sana kutoka kwa mwanamke huyo, alimpenda na kwake alikuwa kila kitu.
 
SEHEMU YA 23

Moyo wake ukazidi kumpenda, kumjali ka mpenzi wake. Mpaka kufikia hatua hiyo hakukuwa na siri tena, wakajiweka wazi na kuanza kupostiana kwenye mitandao ya kijamii.

Kila Mtanzania aliyeona picha za watu hao, jinsi walivyokuwa wakipostiana walishangaa, uhusiano huo ulitangazwa sana kwenye magazeti, mitandao ya kijamii lakini walipinga kwamba hakukuwa na jambo lolote lile lililokuwa likiendelea.

“Ila jamani huu ujumbe kiboko,” alisema mwanaume mmoja, alishikilia simu yake na wakati huo alikuwa akiangalia posti ya Theo aliyoiandika kwa maneno marefu kuhusu Violeth.

“Ujumbe gani?”
“Aliouandika Theo. Aiseee!” alisema jamaa huyo.
“Hebu usome kwa sauti!” alisema jamaa mwingine na kuanza kuusoma, ujumbe huo uliandikwa hivi...

‘Wakati mwingine huwa ninaamka usiku wa maneno na kuyafikiria maisha yangu, huwa ninajiuliza, ninaota ama? Hapo kabla sikuwahi kupata furaha hii niliyokuwanayo, labda hii ndiyo picha halisi ya mapenzi.

‘Nilipokuona mara ya kwanza, moyo wangu ulishtuka, mwili ulikufa ganzi na kuhisi kama nilikuwa kwenye ulimwengu mmoja wa ajabu sana. Sikuamini kama kuna siku nitakuwa katika mikono yako, ukinipenda kama unavyofanya sasa hivi.

‘Violeth! Nikiambiwa nichague kitu chochote kile duniani kwa sasa, nitakuchagua wewe katika maisha yangu yote. Sikuwa nimekamilika, nilikuwa na mapungufu sana lakini baada ya kuwa nawe, nimekamilika, nimekuwa mwanaume ambaye anastahili kuitwa mwanaume kwa sasa.

‘Kila ninapokaa peke yangu, nalikumbuka tabasamu lako tamu, linanifanya nijione kuwa mtu mwenye bahati sana, nakumbuka kicheko chako kile cha uchokozi kinachonichanganya kupita kawaida. ‘Violeth! Kuna maneno mengi nahitaji kukwambia lakini hayo yote yamebebwa na neno moja tu,

NAKUPENDA SANA.’
Yalikuwa maneno yaliyobeba ujumbe mzito, kila mtu aliyeusoma alishtuka, hakuamini kama kungekuwa na mwanamke ambaye angeandikiwa maneno matamu kama hayo aliyoandikiwa Violeth.

Mambo yalikuwa moto, Theo alichanganyikiwa mno, hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kumwambia Violeth kwamba alihitaji kumuoa, kufunga ndoa na kuishi kama mume na mke.
 
SEHEMU YA 24

Alipomwambia maneno hayo, msichana huyo alishtuka, alimwangalia Theo, alihitaji kujua kama alimaanisha ama alikuwa akimtania. Ili kuonyesha kwamba kile alichomwambia kilitoka moyoni mwake, palepale alipokuwa akatoa pete na kutaka kumvalisha.

“Theo! Are you serious?” (Unamaanisha Theo?) aliuliza Violeth huku machozi ya furaha yakianza kumtiririka mashavuni mwake.
“This is what I’m doing baby!” (ndicho ninachokifanya mpenzi) alisema Theo na kuanza kumvisha pete msichana huyo.

Sherehe hiyo ilikuwa ni ya washikaji tu, hakukuwa na mwandishi wa habari wala mtu yeyote ambaye alihudhuria, kila kitu kilifanyika kimyakimya kiasi kwamba kulionekana kama hakuna kitu chochote kilichokuwa kikiendelea.

Taarifa ya kila kitu kilichotokea kikawekwa siku iliyofuata katika mitandao ya kijamii, watu walishtuka, kama kulikuwa na kitu kilichoitwa Breaking News basi siku hiyo ndiyo ilikuwa habari yenyewe.

Wengi walifurahia, waliomba usiku na mchana Theo aoe, apate mwanamke ambaye angemthamini na kuzalia watoto maishani mwake, hakutaka kufanya hivyo kwa kuwa alibabaikiwa na wanawake wengi lakini siku hiyo aliamua kuweka wazi kwamba alikuwa kwenye uhusiano na msichana mwenye mafanikio makubwa, Violeth.

“Jamani siamini!” alisema msichana mmoja, alikuwa akiwaambia wenzake, kile kilichoonekana kwenye simu yake kilikuwa kama ndoto.

“Huamini nini?”
“Eti Theo amemviha pete Violeth!”
“Unasemaje?” aliuliza msichana mwingine huku akionekana kushtuka, akaichukua simu ya rafiki yake ili ajionee mwenyewe.

Kile alichoambiwa ndicho kilichoonekana kwenye simu ile, picha ya pete na nyingine nyingi juu ya kile kilichotokea kilimshangaza kila mmoja, kulikuwa na watu wengi ambao hawakuamini kama mwanaume huyo alichukua uamuzi mgumu na mkubwa kama huo.
 
SEHEMU YA 25

Waandishi hawakutaka kuishia hapo, walichokifanya ni kuanza kumtafuta Theo.

Simu yake haikuwa ikipatikana na walipoulizia waliambiwa kwamba wawili hao waliondoka na kwenda Visiwani Hawaii kwa ajili ya kula bata tu huku wakijiandaa kufunga ndoa katika miezi kadhaa ijayo kitu ambacho

kilimfurahisha kila mmoja kwani kwa jinsi Theo alivyo, umaarufu, utajiri, alistahili kabisa kuishi na msichana kama Violeth ambaye kila siku alikuwa msichana mnyenyekevu na mwenye moyo wa kumsaidia kila aliyemuomba msaada.

Kama walivyoambiwa ndivyo ilivyokuwa. Wawili hao walikuwa katika visiwa hivyo huko Marekani.

Muda wote walionekana kuwa na furaha mno, Violeth alijulikana dunia nzima, kila mtu aliyekuwa akimuona huko alitamani sana kupiga naye picha.

Japokuwa kwa Afrika Theo alikuwa supastaa lakini alipofika huko na Violeth akaamini kwamba ustaa wake haukufua dafu kwa mtu kama huyo.

Kuna muda alijisikia wivu, wanaume walimsogelea msichana huyo, walimshika kiuno na kupiga naye picha. Moyo ulimuuma, wivu ulimkamata lakini hakuwa na jinsi.

Huko ilikuwa ni kula raha tu, walitumia kiasi kikubwa cha pesa na ili kuwaonyeshea watu kwamba walikuwa kwenye mapeni ya dhati, picha nyingi ziliwekwa mitandaoni ambapo watu walizipakua na kuweka kwenye akaunti zao.

“Violeth mpenzi! Ninakupenda mno,” alisema Theo huku akimwangalia msichana huyo, alikuwa juu ya kifua chake kwenye mchanga wa Bahari ya Atlantiki.

“Nakupenda pia mpenzi!”
“Ninahitaji unizalie watoto watatu. Ningependa tuanze kwa kupata mapacha, wawe wa kike na kiume, wa kiume aitwe Harry,” alisema Theo huku akizichea nywele za Violeth aliyekuwa kifuani kwake.

“Na wa kike?”
“Chagua wewe!”
“Aitwe Rachel!”
“Jina zuri pia!” alisema Theo na kumbusu kichwani.
 
SEHEMU YA 26

Walikaa huko wiki nzima, kwenye magazeti mbalimbali Bongo waliandika kuhusu watu hao, si huko tu bali hata nchini Marekani magazeti mengi ya udaku yaliandika kuhusu wawili hao, hasa Violeth ambaye alikuwa maarufu sana.

Kupitia Violeth, watu wa huko wakaanza kumfahamu Theo, wakamfuatilia na kugundua kuwa miongoni mwa watu waliokuwa na majina makubwa barani Afrika.

Alikuwa na wafuasi wengi mitandaoni kuliko hata mastaa wengine huko, nyimbo zake zilikuwa kali na video zake kwa upande wa Youtube zilikuwa zikitazamwa zaidi ya watu milioni mia moja kitu kilichomfanya kila mmoja kuona huyo hakuwa mtu wa mchezo kabisa.

Jarida la Flamingo, haraka sana likafanya mawasiliano na Violeth na kuomba nafasi ya kuweza kuzitumia picha zao kwenye jarida hilo. Hakukuwa na tatizo kabisa, wakaweka mikataba, wakalipwa na picha kuanza kupigwa na kuwekwa.

Wakazidi kupata umaarufu, harusi ambayo walitarajia kufanya ilimfanya kila mtu kutamani kuhudhuria ili kuona jinsi watu hao watakavyooana na kuwa mume na mke.

Siku zilikatika na baada ya wiki moja wakarudi Tanzania ambapo kipindi maalumu cha mahojiano juu ya uhusiano wao kuandaliwa. Walihojiwa na kuulizwa maswali mengi, waliyajibu kwa ufasaha na kutaja siku ya harusi kwamba ni baada ya mwezi mmoja.
 
SEHEMU YA 27

“Na hiyo harusi itafanyikia hapa au Ufaransa?” aliuliza mwandishi.
“Hapahapa Tanzania!”

Kila walilolisema ndilo lililofanyika kwani baada ya kupita mwezi mmoja, hatimaye Theo na Violeth wakafunga ndoa kwenye Kanisa la St. Joseph lililokuwa jijini Dar es Salaam na watu hao kuwa mume na mke.

Harusi hiyo ilikuwa gumzo, kanisa hilo lilijaza watu wengi, kila mmoja alitaka kushuhudia kilichokuwa kikienda kutokea. Wengi walipiga picha kwa ajili ya kuweka kwenye mitandao yao ya kijamii, waandishi wa habari walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanapata picha ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Wanandoa hao walikuwa na nyuso za furaha, walimshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto walizokuwa wamejiwekea za kufunga ndoa na kuwa pamoja.
Kila mtu Tanzania alikuwa bize kufuatilia harusi hiyo iliyokuwa gumzo kila kona.

Masupastaa wengi duniani walihudhuria, walifurahi na kuona hatimaye yule msichana mrembo, ambaye mpenzi wake alikufa kwenye ajali ya ndege hatimaye alikuwa akiolewa na mwanaume mwenye pesa na maarufu mno barani Afrika.

“She is very beautiful,” (ni mrembo mno) alisema mwanamke mmoja, alikuwa ni Naomi Campbell, mmoja wa wanamitindo maarufu duniani.
|
|
Je, nini kitaendelea?

Kumbuka hii ni miongoni mwa simulizi zinazoumiza na kufundisha mno. Endelea kunifuatilia.
 
SEHEMU YA 27

Harusi ilifungwa na hatimaye maharusi kuondoka kuelekea nchini Marekani kula raha visiwani. Walipendeza, walikuwa pamoja kila wakati na walikuwa gumzo kila kona.

Uzuri wa Violeth ukaongezeka zaidi, alinawiri na muda wote alionekana kuwa na furaha tele. Mawazo ya marehemu mume wake yaliondoka, kulikuwa na mwanaume mwingine ambaye aliingia kwenye maisha yake na kumpa furaha ya milele.

Huko Visiwani walikaa kwa siku tano ndipo wakaenda jijini New York katika Hospitali ya St. Mathew Medical Center na kuonana na Dk. Stephen Hill ambaye alikuwa ni mtaalamu wa masuala ya uzazi na kumwambia nia yao ya kutaka kupata mapacha.

Huyo ndiye aliywaambia ni kitu gani cha kufanya. Aliwaambia kila kitu, namna ambavyo walitakiwa kufanya kupata mtoto wa kike, wa kiume, mapacha wa jinsi moja ama tofauti.

Walisikiliza ushauri wa daktari huyo na kuondoka kurudi hotelini, walikaa huko kwa siku kadhaa na ndipo wakaamua kurudi nchini Tanzania.

Maisha yalikuwa na raha, hakukuwa na machozi, kila aliyewaona ilikuwa ni rahisi kugundua kama wawili hao walikuwa wakipendana sana.

Kila kona walikuwa wawili, kwenye mitandao ya kijamii walitawala wao tu. Theo aliendelea na shughuli zake za muziki, alitunga nyimbo kali, zilizombeba na kumpa jina kubwa zaidi.

Kila mtu aliyezisikia alizipenda na kuamini kwamba kwa kipindi hicho mwanaume huyo ambaye alikuwa akishikilia Tuzo za AFRIMMA kwa kuwa Mwanamuziki Bora kwa miaka mitatu mfululizo alikuwa bora zaidi ya mwanamuziki yeyote yule Afrika.

Jina lake liliongezeka zaidi, utajiri ukawa mkubwa na hatimaye akaanzisha redio na televisheni zake mwenyewe, akanunua hisa ya asilimia thelathini katika Mtandao wa Mawasiliano wa Tricom.

“Nilivyokuwa masikini zamani, nadhani nina kiu sana ya kuwa bilionea mkubwa, ila siwezi kufanikiwa hivyo bila kuwa na wewe, mfariji wangu, mshauri wangu mkuu na msimamizi wa mali zangu zote. Kilicho changu, ni chako pia,” alisema Theo huku akimwangalia Violeth ambaye alikuwa pembeni yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom