Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,977
- Thread starter
- #121
SEHEMU YA 28
“Nashukuru kwa kunithamini! Nitakusimamia na kukushauri kwa kila kitu my hubby,” alisema msichana huyo.
“Nashukuru sana kwa kuwa nami!”
“Usijali! Nikwambie kitu?” aliuliza Violeth huku akimwangalia Theo.
“Niambie!”
“Nina mimba!” alisema Violeth maneno yaliyomfanya Theo kushtuka, akamkazia macho.
“Just hold on! Unasemaje?” aliuliza mwanaume huyo.
Violeth hakujibu, akamuonyeshea tumbo lake. Theo akasogeza sikio lake na kujifanya kama anasikiliza kilichokuwa humo tumboni.
Alikuwa na furaha tele, hakuamini kama naye alikuwa akienda kuitwa baba. Alitamani sana kuwa na mtoto, kwake, hakukuwa na kitu alichokipenda kama kuitwa baba.
Alishindwa kuvumilia, akamsogelea Violeth na kumbusu shavuni kisha kuanza kubadilishana mate. Alijiona kukua, kama alikuwa na utoto sasa ulikuwa ni muda wa kubadilika, alitegemea kuitwa baba baada ya miezi tisa.
Mimba hiyo ikaongeza mapenzi, wakapendana zaidi. Violeth hakuwa mtu wa kufanya kazi, Theo alimsaidia kwa kila kitu, alihakikisha hagusi kitu chochote kile kwa sababu hakutaka kuona akichoka kwa kuwa tu alibeba kitu tumboni mwake.
Taarifa za ujauzito wa Violeth haikuwa siri, Theo akawaambia marafiki zake kwa furaha, marafiki hao wakawaambia watu wengine na hatimaye kila mmoja kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.
Theo akaonekana shujaa, aliheshimiwa mno, alipigiwa simu na kupewa pongezi kwani kwa kazi aliyoifanya. Mzinguko yake mingi ikapungua na muda mwingi alikuwa na mke wake, walipiga stori huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha kupita kawaida.
Haraka sana wakaelekea hospitalini na kupima kwa Ultra-Sound ambapo majibu yalitoka kwamba Violeth alikuwa na mapacha wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike.
“Oyoooooo...” alisema Theo kwa furaha, akamsogelea mke wake na kumkumbatia, kumbatio kubwa na la haja, alilomshika vilivyo kana kwamba hakutaka kumuachia kutoka mikononi mwake.
“Nakupenda mke wangu...nakupenda mama wa watoto wangu,” alisema Theo huku akionekana kuwa na furaha mno.
“Nakupenda pia baba watoto,” alisema Violeth na kuanza kubusiana hapohapo ofisini kwa daktari.