Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,977
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 21
Kichwa cha Violeth kilichanganyikiwa, hakutaka kuwa na Theo lakini kwa jinsi jamaa alivyomfanyia, alijiona kuwa na thamani kuliko mwanamke yeyote yule.
Theo hakuzungumza jambo lolote lile kuhusu mapenzi, alijua msichana kama Violeth hakuwa wa kumuingia haraka kama ilivyokuwa kwa wasichana wengine.
Huyo alikuwa aina ya wanawake wa kuwaendea taratibu, kuwaonyeshea jinsi unavyowajali na mwisho wa siku kumwambia kwamba ulikuwa ukimpenda kwa moyo wote.
Walikwenda mpaka katika hoteli aliyofikia na kusimamisha gari, akalizima kabisa na kuanza kuangaliana.
Violeth alikuwa kimya, macho yake yalikuwa yakimwangalia mwanaume huyo, alionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa akimpenda, moyoni mwake hakuwa na mwanamke yeyote ambaye alimthamini kama ilivyokuwa kwake.
“Umependeza,” alisema Theo kwa sauti ndogo iliyosikika ndani ya gari tu.
“Umeniambia hivyo sana yaani!”
“Najua! Kwa sababu unastahili, mdomo wangu hauchoki kukwambia jinsi ninavyokupenda,” alisema Theo huku akiendelea kumwangalia Violeth, hata kuyatoa macho yake usoni mwa msichana huyo alishindwa.
Violeth alibaki akitabasamu tu, hakuamini kama mwanaume huyo angemwambia maneno matamu kama hayo, kwake ilikuwa kama ndoto, alipenda kupendwa, kuthaminiwa na kwa jinsi Theo alivyokuwa akiongea alionekana kumaanisha mno.
Haraka sana mwanaume huyo akaupeleka mkono wake kwa Violeth na kuushika, msichana huyo akasikia msisimko wa hali ya juu, ni kama alipigwa shoti ya umeme, mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, damu ilizunguka mwilini mwake kwa kasi mno.
“Samahani kwa kukuchelewesha kurudi hotelini,” alisema Theo huku mkono wake ukiwa kwa msichana huyo.
“Usijali! Ahsante sana.”
“Nikusindikize?”
“Unataka tuanze kupigwa picha kesho tuonekane tena kwenye magazeti?” aliuliza Violeth huku akicheka.
“Sijali! Acha waandishi wapate cha kuandika maisha yao yasonge,” alisema Theo.
“No! Naomba ubaki. Nitajitahidi kwenda peke yangu! Kwa heri Theo, baki na amani ya Bwana,” alisema Violeth huku tabasamu kali lililomchanganya Theo likionekana usoni mwake.