Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

SEHEMU YA 16

Waliyauliza maswali yao, Violeth alijibu kwa umakini lakini Theo hakutaka kujibu kabisa kwani endapo angelazimishwa sana basi angetoa siri kuwa alimpenda msichana huyo na alikuwa tayari kwa lolote lile.

Baada ya waandishi kumaliza maswali yao, wawili hao wakaenda ndani ya magari yao na kuondoka mahali hapo.

Kichwa cha Theo kilichanganyikiwa, muda wote alikuwa akimfikiria Violeth, alikuwa msichana mrembo mno ambaye alikuwa tayari kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anamchukua na kuwa mke wa maisha yake.

Alipofika nyumbani, kwa kuwa alikuwa na namba ya msichana huyo, akampigia na kuanza kuzungumza naye.

Alikuwa na furaha mno, kwa jinsi Violeth alivyosikika kwenye simu, sauti yake ilivyokuwa nzuri hakika ilimchanganya na kuhisi kama alikuwa akizungumza na msichana mwenye sauti nzuri kuliko wote katika dunia hii.

“Violeth! Ninakupenda sana,” alisema Theo kwenye simu, alikuwa amelala, simu ilikuwa sikioni mwake.

“Ooh my God! (Oh Mungu wangu!) alijifanya kushangaa msichana huyo. “Kwa kipindi kirefu tulichokaa pamoja, nimejisikia tofauti sana, umeuteka moyo wangu kiasi kwamba sitaki kusikia lolote lile kuhusu wewe.

You’ve changed my world. Violeth! Ninakuhitaji, ninataka kuwa nawe katika maisha yangu yote,” alisema Theo kwa sauti ya chini kabisa ambayo aliamini ingemchanganya msichana huyo.
“Hapana! Si kwa sasa!”
“Kwa nini?”

“Moyo wangu una maumivu makali sana!”
“Najua! Ninahitaji nafasi ya kuyaondoa maumivu hayo, nitakufanya kuwa mwanamke mwenye furaha kuliko wote katika dunia hii,” alisema Theo.
“Theo....”
“Violeth! Tafadhali naomba nafasi,” alisema Theo.

Bado Violeth hakujiamini, alijiona kutokuwa tayari kuingia kwenye ulimwengu wa mapenzi na mwanaume yeyote yule, alijiwekea msimamo kwamba hatoingia kwenye uhusiano katika kipindi hicho.

Alimwambia hilo Theo, mwanaume huyo hakusikia, leo alipoambiwa hivyo, kesho asubuhi alimpigia simu na kuendelea kumsisitiza.

Baadaye Theo akagundua kwamba alikuwa akikosea kila alipompigia simu msichana huyo na kumsisitizia awe mpenzi wake bali alichotakiwa kufanya ni kumuonyeshea kwamba alikuwa akimpenda mno.
 
SEHEMU YA 17

Hilo ndilo lililofanyika, usiku wa siku hiyo akampigia simu na kumwambia kwamba kungekuwa na gari fulani ambalo lingemfuata na kumchukua kisha kumpeleka sehemu kwenda kula chakula cha usiku pamoja hivyo alitakiwa kujiandaa.

Kwa Violeth hakukuwa na tatizo, akajiandaa, akaoga, akapaka mafuta ya kawaida, hakuwa mtu wa kupaka sana make up hivyo alijiweka kawaida tu.

Baada ya kumaliza akakaa kitandani na kuanza kufikiria kuhusu mwanaume huyo. Bado moyo wake haukuamua kama alistahili kuwa naye ama la.

Hapo kitandani akafungulia muziki kwenye simu yake na kuanza kusikiliza nyimbo mbalimbali za mwanaume huyo.

Siku zote nyimbo hizo zilionekana kuwa za kawaida lakini siku hiyo kila mstari katika nyimbo zile alihisi kama anaimbiwa yeye.
“Mungu wangu! Sitaki hili litokee,” alijisemea.

Baada ya dakika kadhaa akapigiwa simu na kuambiwa kwamba tayari gari lilifika mahali hapo, haraka akatoka chumbani na kwenda nje.

Gari zuri aina ya Range ilikuwa inamsubiri, akafunguliwa mlango na dereva, akaingia ndani na kuondoka mahali hapo huku tayari ikiwa ni saa mbili usiku.

Alikuwa kimya, hakutaka kuzungumza kitu chochote kile. Humo akachukua simu yake na kuingia kwenye akaunti ya Instagram ya Theo na kuanza kuangalia picha zake.

Kwa mara ya kwanza akaanza kuhisi kitu moyoni mwake, mapenzi yakaanza kuchipua haraka sana kiasi kwamba mpaka yeye mwenyewe alibaki akishangaa.

Baada ya dakika kadhaa, gari likasimama kwenye jengo moja kubwa, lilikuwa ghorofa jipya lililojengwa maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Siku hiyo Theo alilikodi kwa ajili ya kufanyia tukio lake tu.

Wale waliokuwa wakitakiwa kuwa wazi siku hiyo walilipwa pesa na kuambiwa wasifungue kwani kulikuwa na kitu muhimu sana kilikuwa kikitokea siku hiyo.
 
SEHEMU YA 18

Wakateremka, wakachukua lifti na kuelekea juu. Walipofika huko, wakateremka, hawakuishia kwenye chumba chochote kile bali walikwenda mpaka juu kabisa ya ghorofa sehemu ambayo kulikuwa na mitambo kadhaa, madishi ambapo huko ungeweza kuliona Jiji la Dar es Salaam kwa uzuri kabisa.

Kulipambwa vilivyo, katikati kulikuwa na meza kubwa iliyokuwa na vyakula mbalimbali, kulikuwa na chupa ya mvinyo.

Pembeni kulikuwa na maua yaliyokuwa yamemwagwa kwa chini, kulikuwa na kapeti jekundu kutoka pale alipokuwa akiingilia lakini pia kwa pembeni kulikuwa na wanaume wanne ambao walishika maneno yaliyosomeka ‘I LOVE YOU’.

Mbali na hayo yote pia kulikuwa na wanaume wawili walioshika vifaa viitwavyo saxophone ambavyo vilikuwa na muonekano kama wa tarumbeta, hao kazi yao ilikuwa ni kupuliza muziki wa taratibu mahali hapo.

Ukiachana na hayo, pia kwa mbele kulikuwa na viti vingine viwili ambavyo vilielekea upande uliokuwa na uwezo wa kuliona Jiji la Dar es Salaam kwa uzuri, yaani hivyo vilitakiwa kutumika kama mapumziko baada ya kula chakula, wakae na kuangalia jiji hilo lilivyokuwa likionekana kwa usiku.

Violeth alisimama mlangoni huku akiviangalia vitu vyote hivyo, ni kama alichanganyikiwa, hakuamini kama kungekuwa na mwanaume ambaye angemfanyia vyote hivyo.

Moyo wake ukazidi kutekwa, huku akiwa amesimama kama mtu aliyepigwa na butwaa, Theo akatokea na kuanza kumsogelea.

Alivalia shati jeupe, alichomekea kwa suruali yake nyeusi, alivalia tai na moka chini, saa ya Rolex aliyonunua kwa bei ya shilini milioni arobaini na nne Afrika Kusini, alitembea kwa mapozi huku akimfuata na sura yake ikiwa imependezeshwa kwa tabasamu pana.
“Tu es la bienvenue mignonne,”

(Karibu mrembo) alisema Theo kwa Kifaransa ambacho kilieleweka vizuri masikioni mwa Violeth. Akampa mkono na kumshika, akaanza kutembea juu ya kapeti jekundu.
“Umefanya yote haya kwa ajili yangu?” aliuliza Violeth huku akionekana kushangaa.

“Ndiyo! Nimefanya haya yote kwa ajili yako kwa kuwa unastahili,” alisema Theo huku akiachia tabasamu pana.
 
Endelea kunibania ivyo ivyo Shunie ila ipo cku utaachia tu. Nakula uhondo tartiiiib!
 
Violeth kashanasa hapa.....kazi kwake Theo.

SEHEMU YA 19

Walikwenda mpaka mezani, Theo akamuwekea kiti na kumtaka kukaa, msichana huyo akakaa na Theo kuelekea kwenye upande mwingine na kukaa kisha wale watu wa muziki kuanza kutumbuiza kwa kutumia saxophone

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo ilikuwa ni vigumu kuamini kwa Violeth kwamba vilifanywa kwa ajili yake. Siku hiyo Theo hakutaka kuzungumza lolote lile kuhusu mapenzi, alihitaji kumuonyeshea kwa matendo kwamba alikuwa akimpenda mno.

Walikula, walifurahi pamoja na baada ya kumaliza wakaenda kwenye vile viti viwili, wakakaa na kuanza kupiga stori huku wakiangalia mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.

Moyo wa Violeth ukajisikia amani mno, alihisi kupendwa zaidi ya mwanamke yeyote ndani ya dunia hii.

Alitamani kumwambia Theo kwamba alikubali kuwa mpenzi wake lakini alitakiwa kusikia kutoka kwa mwanaume huyo kama alikuwa akimpenda kama alivyomwambia siku iliyopita.
“Nikuulize swali?” aliuliza Theo.

“Niulize!”
“Au subiri nikwambie kitu. Unajua siku moja nilikaa na kujiuliza, hivi mtoto aliyezaliwa kwenye familia ya kitajiri, huwa anajisikiaje?” alisema Theo.
“Kivipi?”

“Mimi nimezaliwa kwenye familia ya kimasikini sana, familia ambayo haikuwa na kitu chochote kile. Kipindi kile nilikuwa najiuliza ni kwa namna gani watoto wa kishua walikuwa wakijisikia baada ya kugundua kwamba wametoka kwenye familia yenye pesa,” alisema Theo.
“Naanza kukuelewa.”
 
SEHEMU YA 20

“Nilijisemea tu kwamba na mimi siku moja hili swali natakiwa kuwauliza watoto wangu, hivyo nikapambana mpaka kufikia hapa nilipo,” alisema Theo huku akimwangalia Violeth.

“Nadhani swali lako limelenga sehemu fulani! Niambie umelenga nini!”
“Nataka nijue! Hivi unajisikiaje baada ya kugundua mtu fulani anakupenda sana?” aliuliza Theo.

“Nilijua tu! Ila umeanzia mbali!” alisema Violeth huku akitabasamu.

“Hahah! Najua ulilijua hili. Ninahitaji kufahamu, huwa unajisikiaje?” aliulia.
“Kwani wewe huwa unajisikiaje?”
“Sijawahi kujisikia kwa kuwa sijawahi kupendwa!” alijibu.
“Hujawahi kupendwa?”

“Ndiyo! Kila ninayempenda, hanitaki, wewe mwenyewe si unaona,” alisema Theo huku akimwangalia Violeth ambaye alibaki akitoa tabasamu na kuangalia chini kwa aibu kwani alijua kabisa kwamba mwanaume huyo alimaanisha yeye.

Walizungumza mambo mengi, baada ya kumaliza, akamsimamisha na kumuomba kumsindikiza nyumbani kwake kwani hakutaka kuona akiondoka peke yake.
Kwa Violeth hakukuwa na tatizo lolote lile, akakubali, akashikwa mkono na kuanza kuondoka mahali hapo.

Kwa kuwaangalia tu ilitosha kujua kama watu hao walikuwa wakipendana mno, walipendeza na kila hatua waliyokuwa wakipiga, iliwafanya hata wale watu waliokuwa mahali hapo kushangaa ni kwa namna gani Violeth hakuwa amekubali kuwa na mwanaume kama Theo.

Walipofika nje ambapo kulikuwa na walinzi waliokuwa wakihakikisha ulinzi unakuwa mkubwa mahali hapo, Theo akamfungulia mlango wa gari Violeth, akamuomba kuingia, alipofanya hivyo, yeye mwenyewe akaushikilia usukani na kuondoka mahali hapo, hakutaka kuwa na walinzi, alihitaji kuwa na Violeth tu ndani ya gari hilo.

Moyo wa msichana huyo uliridhika, alifurahi sana siku hiyo, Theo alijua kumfurahisha, alijua kumfanya kujisikia kuwa mwanamke wa kipekee katika dunia hii.

“Nimkubali au niendelee kuwa na msimamo wangu? Mh! Lakini napo kukataa inaonekana kuwa ngumu sana,” alijisemea msichana huyo huku Theo akiendelea kuendesha gari kwa mwendo wa kawaida kabisa.
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom