Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

SEHEMU YA 61

“She won’t die....she won’t die...” (hatokufa....hatokufa...) alisema Theo huku akiwa amemkumbatia mke wake.

Walikaa kwenye hali hiyo kama dakika tano huku kila mmoja akilia. Walipomaliza, Theo akaanza kupiga hatua kumfuata Rachel kitandani pale, alipomfikia na kumwangalia, moyo wake ukazidi kuuma zaidi.

Mtoto huyo mdogo alitia huruma, alikuwa kimya kitandani huku akipumulia mtungi wa gesi iliyokuwa pembeni yake. Baada ya dakika kadhaa daktari akaingia na kuwaomba kutoka kwani walihitaji kuendelea na matibabu.

Wakatoka chumbani humo na kuelekea kwenye korido ambapo hapo wakawakuta waandishi wa habari ambao nao walijifanya kama wagonjwa na kuanza kuwapiga picha pamoja.

Muda wote huo Theo alikuwa akiumia, alijiona kuwa mkosaji kwamba yeye ndiye aliyesababisha hayo yote kwani kama angetulia nyumbani aliamini kwamba angemsaidia mke wake muda wote mpaka kufika hapo hospitalini.

“Ungenipigia simu mke wangu....” alisema Theo kwa sauti ya chini.
“Nilishindwa...nilichanganyikiwa mume wangu....” alisema Theo.

Wakauomba uongozi wa hospitali uwaondoe waandishi hao mahali hapo, wakafanya hivyo na kubaki peke yao na baadhi ya wagonjwa waliokuwa hapohapo.

Siku hiyo haikuwa ya kuondoka tena kurudi nyumbani, walitakiwa kuendelea kubaki hapohapo mpaka pale ambapo daktari angewaeleza kulikuwa na tatizo gani. Kwa sababu familia ilikuwa kwenye hayo matatizo, Theo akaahidi kupambana nayo mpaka mwisho, hata Iyanya, akapanga kumsahau.
|
|
|
|

JE, nini kitaendelea?

Jiwe, hivi hizi hadithi huwa unazitoa wapi?
 
Ngabu bwana hili swali unaniuliza mara ya pili ujue na mwanzo nilishakujibu

Nazitoa kwa nyemo zao la shigongo ndio mtunzi wa hizi story
Jiwe, hivi hizi hadithi huwa unazitoa wapi?
 
Hahahhah wala haujanikera Ngabu naanzaje kukereka mm uwe na amani tu

Eti mzee una uzee gani wewe damu bado changa wazee huwajui eenh
Oh samahani kama nimekukera. Uzee tu unanisumbua.

Nasahau sahau sana. Nisamehe tu.

Ahsante kwa kujibu.
 
SEHEMU YA 61

“She won’t die....she won’t die...” (hatokufa....hatokufa...) alisema Theo huku akiwa amemkumbatia mke wake.

Walikaa kwenye hali hiyo kama dakika tano huku kila mmoja akilia. Walipomaliza, Theo akaanza kupiga hatua kumfuata Rachel kitandani pale, alipomfikia na kumwangalia, moyo wake ukazidi kuuma zaidi.

Mtoto huyo mdogo alitia huruma, alikuwa kimya kitandani huku akipumulia mtungi wa gesi iliyokuwa pembeni yake. Baada ya dakika kadhaa daktari akaingia na kuwaomba kutoka kwani walihitaji kuendelea na matibabu.

Wakatoka chumbani humo na kuelekea kwenye korido ambapo hapo wakawakuta waandishi wa habari ambao nao walijifanya kama wagonjwa na kuanza kuwapiga picha pamoja.

Muda wote huo Theo alikuwa akiumia, alijiona kuwa mkosaji kwamba yeye ndiye aliyesababisha hayo yote kwani kama angetulia nyumbani aliamini kwamba angemsaidia mke wake muda wote mpaka kufika hapo hospitalini.

“Ungenipigia simu mke wangu....” alisema Theo kwa sauti ya chini.
“Nilishindwa...nilichanganyikiwa mume wangu....” alisema Theo.

Wakauomba uongozi wa hospitali uwaondoe waandishi hao mahali hapo, wakafanya hivyo na kubaki peke yao na baadhi ya wagonjwa waliokuwa hapohapo.

Siku hiyo haikuwa ya kuondoka tena kurudi nyumbani, walitakiwa kuendelea kubaki hapohapo mpaka pale ambapo daktari angewaeleza kulikuwa na tatizo gani. Kwa sababu familia ilikuwa kwenye hayo matatizo, Theo akaahidi kupambana nayo mpaka mwisho, hata Iyanya, akapanga kumsahau.
|
|
|
|

JE, nini kitaendelea?
Theo mjalaana,hawezi kumsahau iyanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom