Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

Aarggghh heary unapenda magazeti yaani
Hahaa kama haukubali shauri yako ...ila kama nimfuatililiaji mzuri wa mikasa inayo ufika huu ulimwengu kwa kupitia hizi jinsia mbili basi utanielewa tu ...

Kwa nyinyi watu wa imani mnavisa kibao tu ambavyo viko wazi " .... Adamu+eva+shetani=tunda la dhambi ... eva ndiye aliyekuwa sababu ya kupokea ushawishi toka kwa shetani .. ushawishi uliopelekea balaa kubwa mpaka leo hii ...(watu wa imani mnaamini hivi)

Samson na delila ( najua unajua kisa chake)
Malkia creopatra( wa misri )na Julio Cesar ' nadhani itakuwa umesikia kisa chake ...

Hayo nimekutajia matukio yale maarufu zaidi duniani ambayo yapo mpaka kwenye vitabu vya imani na vya history"

Achilia mbali haya matukio ya kawaida ya kina Irene uwoya na marehemu ndikumana"

Wema sepetu na kanumba
 
SEHEMU YA 61

“She won’t die....she won’t die...” (hatokufa....hatokufa...) alisema Theo huku akiwa amemkumbatia mke wake.

Walikaa kwenye hali hiyo kama dakika tano huku kila mmoja akilia. Walipomaliza, Theo akaanza kupiga hatua kumfuata Rachel kitandani pale, alipomfikia na kumwangalia, moyo wake ukazidi kuuma zaidi.

Mtoto huyo mdogo alitia huruma, alikuwa kimya kitandani huku akipumulia mtungi wa gesi iliyokuwa pembeni yake. Baada ya dakika kadhaa daktari akaingia na kuwaomba kutoka kwani walihitaji kuendelea na matibabu.

Wakatoka chumbani humo na kuelekea kwenye korido ambapo hapo wakawakuta waandishi wa habari ambao nao walijifanya kama wagonjwa na kuanza kuwapiga picha pamoja.

Muda wote huo Theo alikuwa akiumia, alijiona kuwa mkosaji kwamba yeye ndiye aliyesababisha hayo yote kwani kama angetulia nyumbani aliamini kwamba angemsaidia mke wake muda wote mpaka kufika hapo hospitalini.

“Ungenipigia simu mke wangu....” alisema Theo kwa sauti ya chini.
“Nilishindwa...nilichanganyikiwa mume wangu....” alisema Theo.

Wakauomba uongozi wa hospitali uwaondoe waandishi hao mahali hapo, wakafanya hivyo na kubaki peke yao na baadhi ya wagonjwa waliokuwa hapohapo.

Siku hiyo haikuwa ya kuondoka tena kurudi nyumbani, walitakiwa kuendelea kubaki hapohapo mpaka pale ambapo daktari angewaeleza kulikuwa na tatizo gani. Kwa sababu familia ilikuwa kwenye hayo matatizo, Theo akaahidi kupambana nayo mpaka mwisho, hata Iyanya, akapanga kumsahau.
|
|
|
|

JE, nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom