Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

Ebu niambie kabsa kama hii stori itakuja kuuzwa wassap nijue kabsaa maana....
Nimejikuta nacheka tu sinaga hizo mambo mkuu story ninazoweka zote huwa zinaisha hapahapa
 
Pole yake sana Violeth...

Theo akumbuke tu, ukionja asali utachonga mzinga ndiyo kitakachotokea, very bad...

Hakuna kitu kibaya kama usaliti...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 48

Alishangaa sana! Ikambidi amuulize na kitu ambacho Theo alikijibu ni kwamba alihitaji kuzungumza na production nyingine kwa kuwa alihitaji kufanya video nyingine.
“Kweli?” aliuliza Violeth.
“Kabisa....” alijibu.

Violeth hakuwa na hofu hata kidogo, alimwamini sana mume wake kwamba hawezi kumfanya kitu chochote kile, ila baada ya siku kadhaa akapokea simu kutoka kwa mwanamke asiyemfahamu ambaye alikuwa na habari moja yenye maumivu mno.

“Wewe nani?” aliuliza Violeth.
“Ninaitwa Mage mdaku!” alijibu msichana huyo.

“Nikusaidie nini?”
“Nina ujumbe wako mwanana!”
“Ujumbe gani?”
“Ingia kwenye akaunti ya udakuz utauona,” alisema mwanamke huyo na kukata simu.

Moyo wa Violeth ukawa na presha kubwa, hakutaka kuvumilia, haraka sana akaichukua simu yake na kuingia kwenye akaunti aliyokuwa ameambiwa kwa lengo la kuangalia kile alichokuwa ameambiwa.

Alipofungua tu, kitu cha kwanza kilichoonekana kilikuwa ni picha ya mume wake, si huyo tu, bali pembeni yake kulikuwa na msichana mwingine, alikuwa Iyanya na kwa jinsi walivyoonekana tu, picha ilionyesha kwamba walikuwa kwenye hisia kali za mapenzi, kwenye maelezo ya chini kuhusu picha hiyo yalisema kwamba wawili hao waliingia kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi, Iyanya alikuwa msichana mpya, mchepuko wa Theo.

Violeth hakuamini alichokiona, moyo wake ukapiga paa! Kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hapohapo akahisi mwili ukipigwa ganzi, akakosa nguvu, macho yake yakaanza kuona giza, hakuchukua sekunde nyingi, akaanguka na kupoteza fahamu, kile alichokiona, kilimshtua kupita kawaida.
|
|
|


Je, nini kitaendelea?
maumivu na panadol
 
SEHEMU YA 46

Siku hiyo Iyanya alionekana kuwa tofauti, kivazi alichokuwa amekipiga kilimchanganya kila mtu, si watu waliokuwa hapo tu bali hata Theo yeye mwenyewe alichanganyikiwa.

Siku hiyo ndipo alipogundua kwamba msichana huyo alikuwa mrembo mno, alimwangalia kwa macho ya kuibia, mapaja yake, ngozi yake nyororo, sura yake ya kitoto, alichanganyikiwa.

Alikaa na kuanza kuzungumza, siku hiyo ndiyo Iyanya aliamua kuuteka moyo wa Theo, aliongea kwa mapozi huku akimshukuru kwa kila kitu, wakati mwingine sketi yake fupi laini aliyokuwa ameivaa aliipandisha juu kama bahati mbaya hivi.

Kila alipofanya hivyo, macho ya Theo hayakutaka kutulia hata kidogo, yalikuwa yakiangalia kitu kilichokuwa kikimchanganya kupita kawaida. Walikaa hapo kwa saa moja, Theo akaaga anaenda chumbani kupumzika.

“Basi tutaonana,” alisema Iyanya.
“Hutaki tukapumzike na kuongelea mambo mengine ndani?” aliuliza Theo.
Ni kama Iyanya hakuwa amesikia vizuri, alimwangalia mwanaume huyo, alichanganyikiwa.

Theo akamwambia asubiri yeye atangulie halafu kijana wake angempeleka chumbani kwani hakutaka watu wagundue kitu chochote kile.

Akasimama na kuelekea chumbani kisha kumpigia simu kijana wake na kumpeleka msichana huyo huko chumbani. Alipofika, Iyanya akaingia, chumba kilikuwa kizuri mno, Theo alikaa kitandani huku akiwa na taulo tu.

Msichana huyo alipoingia tu, kijana yule akaondoka huku akiwaacha wawili hao humo ndani. Theo akasimama na kumsogelea Iyanya, alipomfikia, akamshika kiuno na kumvutia kwake.

“Una macho mazuri sana, ninapenda unavyoniangalia,” alisema Theo huku akimwangalia msichana huyo.
“Asante sana!” aliitikia Iyanya huku akijifanya kuogopa, kama alikuwa bikira vile.

“Na ninahisi una lipsi laini sana, naomba nihakikishe,” alisema Theo, hapohapo wakaanza kubadilishana mate.


Mawazo ya Theo kwa mke wake, Violeth yakaondoka kabisa, muda huo alikuwa kwa Iyanya aliyeonekana kumtamanisha kupita kawaida. Walisimama huku wakibadilishana mate na baada ya hapo kuelekea kitandani.
Kukulana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom