Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

Hayo ya matatizo sidhani kama anayajua smart sema tu tatizo la kujipenyeza ili aliwe kwani mwanaume angekataa ingekuwaje
Wanaume ndio tatizo...
Maana maamuzi ya mwisho.anayi yeye.bilisi tunamsingizia tu!
 
Ahsante sana Shunie kwa kuturushia Riwaya yaani nakuandalia zawadi yako
 
SEHEMU YA 47

Ni ndani ya dakika chache kitanda kikaanza kupiga kelele. Walifanya mapenzi kwa mara ya kwanza na walipomaliza baada ya saa mbili, Theo akampa kiasi cha dola mia tano na msichana huyo kuondoka zake.
'
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo, walikuwa wakionana na kufanya mapenzi, alimlipa pesa nyingi. Alikuwa amemaliza muda wa kukaa Afrika Kusini lakini hakutaka kurudi Tanzania, mapenzi ya Iyanya yalimteka kwani msichana huyo alikuwa hatari sana kitandani.

Wakati yeye akiendelea na maisha hayo ya kustarehe na msichana mpya, nchini Tanzania Violeth aliendelea kumlea mtoto wake kama kawaida. Moyo wake ulikuwa una kovu ambalo hakujua kama kuna siku lingeweza kufutika.

Kila alipomwangalia mtoto wake, Rachel, kumbukumbu zikamwambia kwamba alitakiwa kuwa na watoto mapacha lakini jambo ambalo Mungu hakutaka litokee, akamchukua mtoto mmoja.

Kila siku ilikuwa ni lazima kuzungumza na mume wake. Alimsistizia kwamba alikuwa akimpenda mno na hakukuwa na mwanaume mwingine katika dunia hii ambaye aliijua thamani yake kama ilivyokuwa kwake.

Theo alimjibu kwa kumwambia kwamba alikuwa akimpenda zaidi, hakukuwa na mwanamke yeyote katika dunia hii ambaye angeweza kuutoa moyo wake kwake, na alikuwa tayari kufanya lolote lile lakini mwisho wa siku waishi wote mpaka vifo vyao.

Wakati siku zikiwa zimekatika, huku muda ambao mume wake huyo alimwambia angekuwa amekwisharudi nchini Tanzania, alishangaa kuona ukimya ukitawala, kila alipokuwa akiongea naye, mwanaume huyo hakumwambia ishu ya kurudi Tanzania hata kidogo.
 
SEHEMU YA 48

Alishangaa sana! Ikambidi amuulize na kitu ambacho Theo alikijibu ni kwamba alihitaji kuzungumza na production nyingine kwa kuwa alihitaji kufanya video nyingine.
“Kweli?” aliuliza Violeth.
“Kabisa....” alijibu.

Violeth hakuwa na hofu hata kidogo, alimwamini sana mume wake kwamba hawezi kumfanya kitu chochote kile, ila baada ya siku kadhaa akapokea simu kutoka kwa mwanamke asiyemfahamu ambaye alikuwa na habari moja yenye maumivu mno.

“Wewe nani?” aliuliza Violeth.
“Ninaitwa Mage mdaku!” alijibu msichana huyo.

“Nikusaidie nini?”
“Nina ujumbe wako mwanana!”
“Ujumbe gani?”
“Ingia kwenye akaunti ya udakuz utauona,” alisema mwanamke huyo na kukata simu.

Moyo wa Violeth ukawa na presha kubwa, hakutaka kuvumilia, haraka sana akaichukua simu yake na kuingia kwenye akaunti aliyokuwa ameambiwa kwa lengo la kuangalia kile alichokuwa ameambiwa.

Alipofungua tu, kitu cha kwanza kilichoonekana kilikuwa ni picha ya mume wake, si huyo tu, bali pembeni yake kulikuwa na msichana mwingine, alikuwa Iyanya na kwa jinsi walivyoonekana tu, picha ilionyesha kwamba walikuwa kwenye hisia kali za mapenzi, kwenye maelezo ya chini kuhusu picha hiyo yalisema kwamba wawili hao waliingia kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi, Iyanya alikuwa msichana mpya, mchepuko wa Theo.

Violeth hakuamini alichokiona, moyo wake ukapiga paa! Kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hapohapo akahisi mwili ukipigwa ganzi, akakosa nguvu, macho yake yakaanza kuona giza, hakuchukua sekunde nyingi, akaanguka na kupoteza fahamu, kile alichokiona, kilimshtua kupita kawaida.
|
|
|


Je, nini kitaendelea?
 
Ebu niambie kabsa kama hii stori itakuja kuuzwa wassap nijue kabsaa maana....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom