Moyo Ulioonja Maumivu

Moyo Ulioonja Maumivu

SEHEMU YA 45

“Wazazi wangu walifariki dunia miaka miwili iliyopita, wakaniacha huku nikiwa sijatimiza ndoto zangu. Ninatamani sana kuwa mwanamitindo, mbele yangu naona giza kubwa na sijui nitatoka vipi.

Kuja kwenye video yako si kwamba napenda kushiriki, ninahitaji kuonekana tu ili kampuni zinijue na hatimaye niwe mwanamitindo kama Naomi Campbell,” alisema Iyanya huku akimwangalia mwanaume huyo.

Alimdanganya, aliona hiyo ndiyo njia nyepesi ya kumpata mwanaume huyo. Hakuishia hapo, ili kutengeneza uhalisia, akaanza kuyavuta machozi yake na kumtoka huku yakitiririka mashavuni mwake.

Ilikuwa ni vigumu sana kugundua kama msichana huyo alikuwa akiigiza, Theo akamuonea huruma, akamsogelea na kumvutia kwake, akamkumbatia huku watu wakiangalia, walipigwa na mshangao.

“Nitakusaidia! Maneno yako yamenigusa sana,” alisema Theo huku msichana huyo akiwa kifuani mwake.

Aliishi maisha hayo, alipenda sana kusaidia watu waliokuwa kwenye matatizo mbalimbali, hakufikiria kama msichana huyo alimdanganya, hakuhitaji kuwa mwanamitindo bali alichokihitaji kilikuwa ni penzi lake tu.

Alimuahidi kumsaidia, hivyo akampa namba yake ya simu kwa ajili ya kuwasiliana.

Hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa alilolifanya kwani hata baada ya kumaliza video hiyo wakaanza kuwasiliana, Theo alijitahidi kumuonyeshea kwamba alipambana kuhakikisha anamsaidia lakini msichana huyo alipambana kuonyesha kwamba alikuwa akihitaji kuwa naye.

Kwa kuwa Theo alikuwa maarufu, alijuana na watu wengi, akawasiliana na baadhi ya mameneja wa kampuni za mitindo na kuwaambia kuhusu Iyanya. Kwa kuwa alisema mtu maarufu, wengi walikubali kumsimamia msichana huyo.

“Nimezungumza na kampuni nyingi, zote zimehitaji kufanya kazi na wewe, ninaamini kabisa kwamba utafanikiwa,” alisema Theo kwenye simu.

“Siamini....siaminiiii...” alisema Iyanya huku akijifanya kulia, kwa sababu walikuwa wakiongea kwenye simu, Theo akahisi kabisa kwamba alikuwa akilia kumbe haikuwa hivyo.

Iyanya akamuomba sana kuonana naye tena, hilo halikuwa tatizo, Theo akakubali kwani alihisi ni kawaida kabisa. Akamwambia hoteli aliyokuwepo, akaelekea huko na kukaa kwenye mgahawa mmoja pamoja na wapambe wake na kuanza kuongea.
 
SEHEMU YA 46

Siku hiyo Iyanya alionekana kuwa tofauti, kivazi alichokuwa amekipiga kilimchanganya kila mtu, si watu waliokuwa hapo tu bali hata Theo yeye mwenyewe alichanganyikiwa.

Siku hiyo ndipo alipogundua kwamba msichana huyo alikuwa mrembo mno, alimwangalia kwa macho ya kuibia, mapaja yake, ngozi yake nyororo, sura yake ya kitoto, alichanganyikiwa.

Alikaa na kuanza kuzungumza, siku hiyo ndiyo Iyanya aliamua kuuteka moyo wa Theo, aliongea kwa mapozi huku akimshukuru kwa kila kitu, wakati mwingine sketi yake fupi laini aliyokuwa ameivaa aliipandisha juu kama bahati mbaya hivi.

Kila alipofanya hivyo, macho ya Theo hayakutaka kutulia hata kidogo, yalikuwa yakiangalia kitu kilichokuwa kikimchanganya kupita kawaida. Walikaa hapo kwa saa moja, Theo akaaga anaenda chumbani kupumzika.

“Basi tutaonana,” alisema Iyanya.
“Hutaki tukapumzike na kuongelea mambo mengine ndani?” aliuliza Theo.
Ni kama Iyanya hakuwa amesikia vizuri, alimwangalia mwanaume huyo, alichanganyikiwa.

Theo akamwambia asubiri yeye atangulie halafu kijana wake angempeleka chumbani kwani hakutaka watu wagundue kitu chochote kile.

Akasimama na kuelekea chumbani kisha kumpigia simu kijana wake na kumpeleka msichana huyo huko chumbani. Alipofika, Iyanya akaingia, chumba kilikuwa kizuri mno, Theo alikaa kitandani huku akiwa na taulo tu.

Msichana huyo alipoingia tu, kijana yule akaondoka huku akiwaacha wawili hao humo ndani. Theo akasimama na kumsogelea Iyanya, alipomfikia, akamshika kiuno na kumvutia kwake.

“Una macho mazuri sana, ninapenda unavyoniangalia,” alisema Theo huku akimwangalia msichana huyo.
“Asante sana!” aliitikia Iyanya huku akijifanya kuogopa, kama alikuwa bikira vile.

“Na ninahisi una lipsi laini sana, naomba nihakikishe,” alisema Theo, hapohapo wakaanza kubadilishana mate.

Mawazo ya Theo kwa mke wake, Violeth yakaondoka kabisa, muda huo alikuwa kwa Iyanya aliyeonekana kumtamanisha kupita kawaida. Walisimama huku wakibadilishana mate na baada ya hapo kuelekea kitandani.
 
Pepo chafu
 
Matatizo ya vipi hayo smart

Kama hivyo mwanamke anajua kabisa jamaa kaoa na mke wake yupo kwenye matatizo, lakini bado anajisogeza na kujipenyeza kwa ushawishi wote ili aliwe...

Sisi wanaume tunaweza kua dhaifa ila wanawake ni ibilisi...

Cc: mahondaw
 
Hayo ya matatizo sidhani kama anayajua smart sema tu tatizo la kujipenyeza ili aliwe kwani mwanaume angekataa ingekuwaje

Ndiyo maana nikasema though sisi wanaume ni dhaifa ila wanawake ni ibilisi...

Mnapotaka kufanikisha jambo liwe baya au zuri litafanikiwa tuu, iwe isiwe...

Cc: mahondaw
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom