Movie ya Gemini man

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Image may contain: 1 person, standing and text




..Ni Henry Brogan..Former marine Scout Sniper..Binadam aliezawadiwa shabaha ya umbali mrefu karne ya 21...anaefanya kazi kama assassin kwenye usimamizi wa D.I.A..

...Defense Intelligence Agency wanaamini kwenye kitengo chao wana Henry Brogan..kazi yoyote inayohitaji kutenganisha roho ya mtu alitumwa yeye..

..Sio kwa sababu anajua sana kupigana..ni kwa sababu pamoja na umri wake wa miaka 51..macho yake yalikuwa yanaona vema lenzi ya bunduki...

..Henry akiwa nyuma ya kifaa cha moto,anamuhesabia adui yake sekunde za kupeleka msiba nyumbani kwake..hata ukiwa kwenye mwendo na umbali unaojua wewe...

..Akikuhitaji,basi risasi yake itakupeleka kwake..na wala umbali sio tatizo...ye ni sniper aliekamilika..

...Leo alipewa kazi kama siku zote..ila hakuifanya kama siku zote..jasusi aliehitajika kuuwawa,alikuwa ndani ya treni inayotembea..

..na Henry alishaseti kila kitu chake kutoka kwenye mashine ili ampeleke kwa mungu...

..Alidhamiria apige kichwa..taiming ikakataa akapiga shingo..adui akafa na henry akastaafu kazi..alijiona uwezo umeshuka..sasa apumzike..

...Akiwa ameamua kutumia muda wake uliobaki kula maisha,aliyoyatengeneza miaka mingi nyuma..analetewa taarifa kuwa yule mtu aliemuua kwenye treni hakuwa na hatia..

..na alistahili kuishi kwa sababu kuna kazi alihitaji kuikamilisha...

..Henry anachanganyikiwa na anaamua kurudi kazini ili ajue yule mtu ni nani na alikuwa akifanya kazi gani..

..Ni hapo ndipo alipojikuta anaingilia mikataba ya siri ya watu waliokuwa wakimtuma kazi..na anapoamua kutumia ujuzi wake kupambana nao..ndipo alipojikuta akisogelea kifo mdomo kwa mdomo..

..Kila hatua aliyopiga alikuwa akiwindwa na watu asiowajua...ni kama vivuli,walimfata kila alipokwenda na walitokea kwa nadra mbele yake na kwa kasi ya ajabu..

..Akaja kugundua kuwa hata aina ya ulengaji shabaha wanayotumia watu hao,ni kama shabaha anayotumia yeye..ni ni hiki!..

...Henry Brogan anapagawa na anaamua kuhamia colombia kujipanga na vita..lakini alichelewa..alikuta vile vivuli colombia pia vimefika kabla yake..afanyeje sasa..

..Akaweka uchunguzi chini..akanyanyua ufundi wake juu..ikapigwa vita ya kiume..inayowataka wanaume..na ni katika vita hiyo ndipo Henry akagundua kitu kipya..kilichomfanya aweke bunduki chini..

..Hawakuwa watu..alikuwa mtu..yess..Brogan alikuwa anawindwa na mtu mmoja tu..na kumuangalia vizuri akagundua kuwa mtu yule ni yeye...ooh mungu wangu..

..Hujanielewa!...

..Yule mtu aliemuua kwenye treni ni mwanasayansi aliekimbia maabara huku akiwa na kazi ya kumalizia..kazi yenyewe ni kufanya sampling clone ya binadamu..yaani kupandikiza binadamu kutokana na binadamu mwingine..

..Kawahiyo Henry alikuwa anawindwa na mwanae ambae hakumzaa wala hakumjua katoka wapi..ila wahuni wamemtengenezea mtu kama yeye mwenye ufundi kama wake..

..MWENYE UMRI WA MIAKA 21..WAKATI YEYE ANA 51..

..Ilikuwa ni jaribio la kimaabara..na lilipofanikiwa ndipo lilipotumiwa kumuangamiza yeye mwenyewe,kwa sababu alishaanza kuutafuta ukweli wa kifo cha yule mwanasayansi...

..Henry Brogan pamoja na ujanja wake wote..alisita kumuua mwanae..na mtoto ndo yuko moto kumuua baba..ye hajui chochote kwa sababu ye ni pandikizi tu la kisayansi..lililofanywa kiufundi...

..Nguvu zinamuisha jemedari huyu..na alipofanikiwa kuingia maabara akaujua ukweli..ni damu yake ndo ilitumika kutengeneza mtu yule..na hazuiliki sababu ye ni mashine cloned..

..Na Henry hataki kumuua yule kijana..sababu anajiona yeye ndani yake..

..Na wakati akifanya njia za kumrudisha yule kijana aujue ukweli na wamuangamize alieleta ile project..kinakuja kitu kigeni kabisa mwisho wa movie..

..Yule kijana hayuko peke yake..wametengenezwa wengi kama yeye,na kwa sura..na uwezo tofauti...

..Henry Brogan..yuko hatarini kutokana na damu yake mwenyewe..
#GEMINI MAN..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom