Moto wateketeza mabanda 100 soko kuu la Mwana Kwerekwe Zanzibar

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,604
2,000
Moto mkubwa ulioibuka joni hii katika soko kuu la Mwana Kwerekwe Zanzibar umeangamiza zaidi ya mabanda 100 ya vyakula na nguo na kusabisha hasara kubwa ya mamilioni ya fedha.

Moto huo umeweza kuteketeza mabanda hayo huku wamiliki wakishindwa kuudhibiti kutokana na upepo ambao baadhi ya wafanyabiashara hao wakiongea na ITV wamesema chanzo kikubwa cha moto huo ni jalala la taka likuwepo pembeni mwa soko hilo na vikundi vya mamantilie kudharau na kuchoma moto ndio uliosababisha kuteketezwa kwa mabanda hayo.

Wakati wafanyabiashara hao wakitoa sababu za jalala la taka kamishna msaidizi wa kikosiu cha zimamoto Zanzibar Haji Gora amelaumu baadhi ya watu kuchoma moto maksudi na kusababisha hasara hizo ambazo ni za mamilioni ya fedha na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa na utaratibu wa kujilinda wenyewe na sio kusubiri zimamoto wafike.

Huu ni moja ya moto mkubwa uliokumba Zanzibar ambapo hasara yake ni kubwa na ni athari kubwa kwa wafanyabiashara hao wadogo ambao tegemeo lao kubwa ni biashara hiyo ya vyakula na mitumba ambavyo karibu vyote vinatoka Tanzania Bara.

Chanzo: ITV
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,729
2,000
Bahati nzuri wananchi wamegundua chanzo mapema maana ungesikia ni fulani huyo analeta uchochezi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom