Moto wafukuta ndani ya CCM Sitta kushitakiwa NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto wafukuta ndani ya CCM Sitta kushitakiwa NEC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Dec 23, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amemjia juu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akimtuhumu kwa kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

  Kutokana na hatua hiyo, ameeleza nia ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili Sitta athibitishe madai yake.

  Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

  "Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

  Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja.

  Mgeja ambaye kwa wadhifa wake ni Mjumbe wa NEC Taifa, alisema CCM hakuna mwanachama aliye juu ya chama na kuwa maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya chama yanapaswa kuheshimiwa.

  "Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika," alisisitiza Mgeja.

  Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

  Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

  "Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

  Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
  akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.

  ......................................................

  Huyu ni mmojawapo wa 'viongozi' waliokunywa maji ya bendera ya kijani!
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, ameeleza nia yake ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili aliyekuwa spika wa bunge lililopipa Samwel Sitta athibitishe madai yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

  Amemjia juu akimtuhumu kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake .

  Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

  “Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

  Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho,” alisema Mgeja.

  “Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika,” alisisitiza Mgeja.

  Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

  Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

  “Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi,” alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

  Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
  akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa ni unafiki wa huyu mzee sitta kila wakati atakuwa kwenye hii hali, ukiamua usafi ni kwa asilimia 100, yeye analaumu tu kila kukicha, hili hali wengine ideology zetu ni 'no one is clean in ccm' aondoke tu ccm atafute sehemu nyingine, akishindwa akae kimya!!!!! yeye hana usafi wowote ule kutaka tu publicity, aacha upropaganda wake. unalaumu weee unabaki humo humo, akili hizo!!
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Khamis Mgeja katumwa kama alivyotumwa Chenge kugombea uspika aka kumwaga mboga na ugali ili wakose wote yeye na Sitta. Sitta ni mzalendo wa kweli na mtu yeyote anayejua hilo atakuwa upande wake. Ukweli ni kwamba mafisadi hawajaridhika na Sitta kupewa hata ukuu wa mkoa yaani wanataka wampotezee kabisa katika safu.
  Huyu Mgeja anawakilisha ule ukiritimba uliokuwapo wakati wa chama kimoja anasahau kuwa demographic na muda vimebadilika. Na kwa kuwa ni low profile, elimu yake ndogo na ana njaa amekubali kutwishwa zigo la kinyesi kwa bei rahisi ya kuwa mtumwa ili aje alimwage kwa Sitta inasikitisha kweli.
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  Yaani post zako ndio zile zile zinazo assume kuwa Kikwete ni SAFI, na kuwa Kikwete na hao mafisadi hawana mawasiliano, nani kawaroga nyie?? There is no way ukamtaja EL, RA JK asiwemo katika hii three cord company, no..way, tuache kudanganyana.

  Logic ndogo tu, kama JK angeamua awaondoe mafisadi anaweza, aidha kawashindwa au yuko pamoja nao, na kama ameshindwa basi sio rais kuna rais wa siri!! ni hizo possibility mbili tu, HAWAWEZI AU YUKO NAO!! na kama hawawezi na kuna rais wa siri basi Sitta asingepewa hata uwaziri kwa mujibu wa post yako. TUAMKE JAMANI hizi logic zenu zimekufa na wala hazilipi kabisa, inakuwa kama mateja wanasimuliana bwana
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sita

  • Amegundua na anatumia udhaifu wa JK- Kama kina chenge, alishidnwa kuwaweka pembeni mhhh
  • Ameanza Kampeni za 2015ni
  • Ana uchu wa madaraka hajardhika na nafasi aliyomegewa
  • Sitta ni mwanasiaa anataka afukuzwe uwaziri ili nyota yake kisiasa kizidi kung'aa 2015
  But wataka mabadiliko wote tunapenda ndani ya CCM wawepo kina Six wengi ili wayumbe

  HIi CCM imefikia pabaya Yaaani wanaona nafuu Sitta awe subject ya Kikao na sio Chenge, Rostam etc
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna ukweli ndani yake hawajaridhika wanataka akose kila kitu.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MGEJA BADALA YA KUPELEKA KESI KWA ROSTAM AZIZI NA LOWASA, KAMNYANGANYE TU KADI YA CCM KWANI NI MZIGO MKUWA SANA KWA SITTA HIYO

  Eti napeleka hoja binafi kwenye kikao cha Sisiem ambacho waamuzi wake ni Edward Lowassa na Rostam Aziz. Ndugu amka kumekucha acha kuvuta blanketi kweupe tayari Tanzania hadi vijijini!!! Hadanganywi mtu hapa tena!!!

  Mgeja kama kweli wewe MUISLAMU SAFI na unayetambua kwamba maana ya UISLAMU ni SALAMA au AMANI, kwanza chukua hizo hatua zako kuelezea umma wa Tanzania juu ya USHIRIKI WAKO KWENYE KUPANGA NJAMA ZA KUWAIBIA KURA ZAO kwenye kikao chenu cha siri Hotel Lakairo huku ukijua fika kwamba kufanya hivyo ni kuliweka taifa katika HATARI kubwa kwa makusudi kabisa na pia kukiuka maana halisi ya imani hii zuri kwetu.

  Nje ya hapo usitupigie kelele kwani HUMO NDANI YA SISIEM YA SASA KUNA WABUNGE WETU (Nguvu ya Umma) kibao ambao hawakubaliani na MAFISADI ktofauti na jinsi ulivyoukumbatia wewe. Cha msingi kazipitieni kadi zao za uanachama CCM ambayo kwa sasa si dili tena na kesho yake utaona VIJANA WENYE UCHUNGU tukiwachagua siku inayofuatia.

  Na vilevile Mgeja, mauaji ya ajabu ajabu nchini kichinichini hatutaki kuyasikia tena hapa nchini. Na ukayafanyie kazi haya maneno vizuri kwani yeyote atakayevumishwa hata kidogo tu kuhusika na kifo cha Mtanzania yeyote tunaye ama ukoo wake jicho kwa jicho. Uchonganishi hatutaki tena.

  Watanzania tuwaombee sana tena sana Dr Hosea wa PCCB (japo kafungwa mikono kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi, ni mpambanaji wa uhakika), tumuombee Samuel Sitta na wapiganaji wetu wengine wengi mle ndani ya Sisiem ambao hatuna haja ya kuwataja majina. Na tangu sasa muangalie sana mienendo ya akina Mgeja hawa dhidi yao.

  Ukiangalia Dr Hosea anachodaiwa kusema hakuisema ili apate utajiri wowote bali ni kwamba ALIUSEMA KWA UCHUNGU jinsi anavyoshindwa kufanya kazi ambayo kwa uhakika anajua fika ufanyike vipi na kwa ufanisi zaidi. Na huyo Mhadhiri wa UDSM aliyeonekana kumchochea moto Dr Hosea asisubiri kuomba radhi baada ya mambo mabaya kutokea. Ni unafiki mkubwa!!

  JK mwenyewe aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akionyesha kuwagwaya MAFISADI kwamba wengine wao ni wa hatari zaidi na kwamba vita dhidi yao yahitaji UMAKINI zaidi sasa hili la Wikiliki ndio ije ionekane nongwa leo??? Sembuse yeye tumempa mamlaka yote juu ya vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama na akadai hivyo je afisa wa chini tu kama Hosea anapokosa ushirikiano kwenye kazi yake aseme nini??? Tuache unafiki!!
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Huyu Khamis Mgeja ni kama mshiba kunde, hayo ni mashuzi tu.
  Kamati kuu ya CCM wamo Mafisadi tena wenye PhD za ufisadi watakosa kuwa n hila?
  Vikao vya CCM vimetawaliwa na umbea utadhani ni vikao vya Machangu malaya wa Mtaa wa Ohio.
  CCM kweli mmepatikana mwaka huu mmebana mmeshindwa sasa mmeamua kuachia tu tutaona mengi hasa yale yasiyoonyeshwa hadharani
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Neno 'tena' linabeba uzito mkubwa wa sentensi yako inamaana tayari kuna kitu kilikuwa kinafanyika na wewe umeshasikia, au nimekosea.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Baada ya Kolimba kudai chama anachokiongoza mwenyewe kama mtendaji wake mkuu KUKOSA DIRA, kilichofuatia????
   
 12. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwa kweli ni hapo tu ndipo anaponichosha mzee 6, ila kwa huo mwendo wake nadhani anatafuta sababu ya kuondoka kwa kutimuliwa ccm ili ajizolee umaarufu zaidi kwa wananchi kwa malengo ya kugombea uongozi wa nchi kupitia upinzani 2015, ni suala la muda tu.
   
 13. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kusema kweli sioni kama ni tatizo, SSM sio ya wafanyakazi na wakulima siku hizi wameinunua wafanyabiashara wakubwa wenye mapesa mengi ambao hata Rais wamemyanganya madaraka kiasi kwamba hawezi kuongea chochote tena zaidi ya kuendesha serikali kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wafanyabiashara wakubwa. Hakuna jinsi ambayo Mkapa, Ed na RA wanaweza kuchunguzwa ilihali wameshikilia serikali, hakuna jinsi ambayo serikali itakwepa kulipa Dowans wakati hawajapata pesa ya kumrudisha EL kugombea Urais 2015, tumeona kesi ya Rada UK ilivyoendeshwa! Hakuna haki inayoweza kupatikana kwa kesi za aina hile, hawa watu mtandao hata mafia hawafai.

  Then what should be done? Hilo ndilo la kujiuliza sasa! Nchi imetekwa na watu wachache walioigeuza kuwa shamba la bibi wanajichotea kama wanavyotaka.

  Lakini haya yote yana mwisho
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sina nia ya kumtetea Sitta linapokuja suala la uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama chochote, kwa mfano kauli za Zitto pia zimeonekana kukikwaza chama chake cha chadema lakini natofautiana na Mgeja kuongea suala hilo na vyombo vya habari.Badala ya kuongea na vyombo vya habari, Mgeja angelipeleka suala hilo ndani ya chama chake kwanza au kuwajulisha viongozi wake wa kitaifa kwanza juu ya kusudio lake hilo.

  Hapa ni kama anarumbana na Sitta hadharani bila kujua msimamo wa chama chake juu ya suala hilo na njia ya kufanya namna ya kumshauri bwana Sitta.

  Pili, Mgeja ameongea na vyombo vya habari kuhusu ajenda ambayo pengine angetakiwa kuongea katibu mkuu wa chama Yusuf Makamba ili kukiepusha chama na malalamiko kwamba kila mtu siku hizi anataka kuwa msemaji wa chama bila kuzingatia taratibu. Njia hii mara nyingi husababisha marumbano kwenye vyombo vya habari kati ya wanachama kama kila mmoja ataamua kuongea na vyombo vya habari kuelezea msimamo wake juu ya matamshi ya Sitta au jambo lingine lolote.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkoa wa shinyanga ni moja ya mikoa ambayo chama cha mapinduzi kimepata tabu ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambapo kilipoteza majimbo mawili na ilibakia kidogo kupoteza jimbo la shinyanga mjini jimbo ambalo ni makao makuu ya ofisi za Mgeja. Mwenyekiti wa mkoa huu ni Mgeja mwenyewe, wafuasi wengi wa CCM huko shinyanga wanadai chanzo ni Mgeja kukumbatia makundi, ni muhimu akaangalia namna ya kuunganisha makundi pinzani ndani ya chama kuliko kuongeza mgawanyiko kwa kuongea na waandishi wa habari. hapa hajengi anabomoa.

  Hata hivyo, Ni kweli kwa nafasi yake ya sasa Siita alikuwa na nafasi ya kulizungumzia kwanza jambo hilo ndani ya chama chake ingawa pengine alilazimika kulitolea ufafanuzi kutokana na masuala hayo kuwa sehemu ya maazimio aliyoyatolea maamuzi alipokuwa spika hivyo kuna watu walitaka kujua msimamo wake kwa sasa.
   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  CCM wangekuwa makini wangeanza na huyu Mgeja. Upeo wake finyu ndio uliosababisha wakapoteza majimbo yote mawili Maswa.
   
 17. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwangu mimi naona sitta ni mfano wa kiongozi ambaye tanzania ya leo inawahitaji lakini nahc kuna mizengwe ndani ya chama kumbana asifurukute na huenda wakubwa wa chama wakamtupa nje kwa kuwa wanatofautiana mitazamo.
   
 18. T

  Taso JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Hivi kwa nini tusisikie "nimewasilisha" hoja binafsi badala ya mikwara ya "nitawasilisha"?

  Mara ooh, Mnyika ana hoja binafsi ya kikatiba, mara Mwenyekiti wa CCM Shinyanga ana hoja binafsi, na kuna Mbunge mmoja aliwahi kuchimba mkwara na hoja binafsi kwamba iwe marufuku kuongelea dini bungeni, hivi yuko wapi? Give me a bleeping break with these fake hoja binafsi

  fikisheni hizo hoja binafsi kwanza ndio mwende kwenye vyombo vya habari
   
 19. T

  Tom JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini mafisadi (JK na CCM yake) si ndio hao hao wamempa cheo alichonacho sasa. Sitta ni fisadi, kelele zake ni mbinu za kuomba apewe zaidi.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,394
  Trophy Points: 280
  Athibitishe nini wakati suala lipo wazi hivyo?

  Hivi kuwazuia wanaumme wasiigombee nafasi hiyo siyo mizengwe............na ukiukwaji wa katiba ya nchi kwa uwazi kabisa? Katiba inakataza kunyanyapaa kwa kijinsia na CCM ndicho walichokifanya hapo..................

  Huyu Mgeja ndiyo chanzo cha mifarakano kwa kumzuia mtu asitoe maoni yake..................
   
Loading...