Moto wafukuta ndani ya CCM Sitta kushitakiwa NEC

[QUOTE

Watanzania tuwaombee sana tena sana Dr Hosea wa PCCB (japo kafungwa mikono kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi, ni mpambanaji wa uhakika), tumuombee Samuel Sitta na wapiganaji wetu wengine wengi mle ndani ya Sisiem ambao hatuna haja ya kuwataja majina. Na tangu sasa muangalie sana mienendo ya akina Mgeja hawa dhidi yao.

[/SIZE][/QUOTE]

Naunga mkono kwa mia, hamna kamati ama kikao cha CCM kinachoongozwa na asiye fisadi. NEC ndio kabisa, maana huko ndio kwenye mafisadi papa. Huyo mbunge ajipendekeza tu na hiyo hoja feki ili aongezewe mgawo wa keki ya UFISADI.

Lakini kuhusu Hosea na Sitta, ntatofautiana nawe. Hosea alisema ili kuwazuga wazungu tu, kimsingi kashindwa kazi na pia ni fisadi sawa tu na Sitta. Hamna cha kuwaombea. Inasikitisha kua mpaka leo Hosea analipwa mshahara tokana na pesa yetu. Kama kweli alichoema ni cha kweli si angejiuzulu kuliko kuendelea kuachia back yake inaendele kubusiwa na Kikwete na kundi lake la mafisadi - anajidhalilisha yeye na elimu yake.

Hivi Hosea na elemu yake aliyonayo ina maana hawezi kazi nyingine yeyote zaidi ya hiyo aliyopewa na MAFISADI ambayo anailalamikia kua makucha yake yamekatwa na Mafisadi.
 
Kama anasema maamuzi hufanywa na vikao halali, hilo agizo lake kwamba 6 afute kauli limepitishwa na kikao gani? Je huko shinyanga hakuna vyombo vya habari?
 
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amemjia juu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akimtuhumu kwa kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

Kutokana na hatua hiyo, ameeleza nia ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili Sitta athibitishe madai yake.

Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

"Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja.

Mgeja ambaye kwa wadhifa wake ni Mjumbe wa NEC Taifa, alisema CCM hakuna mwanachama aliye juu ya chama na kuwa maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya chama yanapaswa kuheshimiwa.

"Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika," alisisitiza Mgeja.

Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

"Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.

......................................................

Huyu ni mmojawapo wa 'viongozi' waliokunywa maji ya bendera ya kijani!

Huyu ngeja anatusaidia sana sisi CDM maana ilibaki kidogo majimbo yote tuyachukue kama si uchakachuaji sijui angekuwa na nguvu gani kwenye hiyo NEC. Tunaomba aendelee kuwa mwenyekiti mkoa wa Shinyanga 2015 tunachukua na halimashauri yote.
 
Six anavyoonekana CCM ni kama Nyepesi anavyoonekana CHADEMA. Hawa jamaa hawaaminiki, wanaweza wakaongea lolote!
 
Mgeja anatafuta pa kujifichia baada ya kuisambaratisha CCM shinyanga kwa mkono wake kama Mwenyekiti wa mkoa.Mgeja huko shinyanga anajulikana kwa jina la TRA kwa maana kwamba usipompa sehemu ya mapato yako huna chako ndiyo maana alishindana na Shibuda.CCM mkoani shinyanga kiko mbioni kufa kwa sababu ya mgeja, ni bahati mbaya sana kwa ccm kwani mwenyekiti wao JK anazo taarifa za udhaifu wa uongozi wa mgeja lakini hana la kusema kwani watu aina ya mgeja ndiyo vipenzi kwa JK.POLENI CCM .Sisi na CDM tunapeta, peopleeeeees
 
Mkoa wa shinyanga ni moja ya mikoa ambayo chama cha mapinduzi kimepata tabu ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambapo kilipoteza majimbo mawili na ilibakia kidogo kupoteza jimbo la shinyanga mjini jimbo ambalo ni makao makuu ya ofisi za Mgeja. Mwenyekiti wa mkoa huu ni Mgeja mwenyewe, wafuasi wengi wa CCM huko shinyanga wanadai chanzo ni Mgeja kukumbatia makundi, ni muhimu akaangalia namna ya kuunganisha makundi pinzani ndani ya chama kuliko kuongeza mgawanyiko kwa kuongea na waandishi wa habari. hapa hajengi anabomoa.

Hata hivyo, Ni kweli kwa nafasi yake ya sasa Siita alikuwa na nafasi ya kulizungumzia kwanza jambo hilo ndani ya chama chake ingawa pengine alilazimika kulitolea ufafanuzi kutokana na masuala hayo kuwa sehemu ya maazimio aliyoyatolea maamuzi alipokuwa spika hivyo kuna watu walitaka kujua msimamo wake kwa sasa.

Ndugu ccm kimepoteza majimbo yafuatayo katika mkoa wa shinyanga: bukombe, bariadi mashariki, maswa magharibi, maswa mashariki na meatu hivyo si mawili tu na huyu mgeja ni mzee wa fitina sana na hana lolote
 
Kama anasema maamuzi hufanywa na vikao halali, hilo agizo lake kwamba 6 afute kauli limepitishwa na kikao gani? Je huko shinyanga hakuna vyombo vya habari?

Hapo umesema kweli. Watu wengine wanakurupuka wakidhani wataonekana wana akili kumbe hakuna lolote. Mantiki ya kawaida haikibali pale mtu anapomtuhumu mwenzake kwenda kinyume na maamuzi ya vikao na kukigawa chama wakati huo huo yeye akifanya kitendo kinachofanana na hicho.

Nilivyoelewa Sitta alitoa kauli inayopingana na utaratibu wa chama kwa kutoa matamshi ambayo yanaonekana kupinga maazimio ya vikao. Mheshimiwa huyo kutoka Shinyanga alikwenda kufanya nini na waandishi wa habari wakati suala analozungumzia linaonekana kuwa lilistahili kuwa kwenye vikao vya chama?
 
Ni kwa moyo mzito sana nalazimika kumjadili huyu mpuuzi MGEJA. Nasema hivyo kwa sababu Mgeja hana hadhi ya kujadiliwa maana yeye ni kama mlipuaji wa kujitoa mhanga ambaye kazi yake ni kutumwa kupayuka anavyojisikia ili kuwafurahisha hao mabwana zake wanaomtuma. Uchambuzi wake ni kielelezo cha ukosefu wa elimu alionao na ndiyo maana anadiriki kusema Sitta angekata rufaa as if kuna mechanism ya rufaa katika maamuzi ya Kamati Kuu na hasa katika masuala kama haya. Kuna wakati watu wadhalimu huwa wanajificha kwenye kivuli cha sheria ili waonekane ni conformists wakati nia yao hasa ni kumfungia milango ya haki mtu. Mimi binafsi najua Mgeja na wenyeviti kadhaa wa mikoa wa hicho chama ni vipaza sauti vya mafisadi ambao bila kucheza ngoma hiyo wanayoicheza hawawezi kupata kula yao ya siku. mimi nina matumaini watu wa aina ya Mgeja siku zao kwenye medani ya siasa ziko ukingoni kwa sababu wananchi wa leo siyo wapumbavu!
 
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amemjia juu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akimtuhumu kwa kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

Kutokana na hatua hiyo, ameeleza nia ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili Sitta athibitishe madai yake.

Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

"Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja.

Mgeja ambaye kwa wadhifa wake ni Mjumbe wa NEC Taifa, alisema CCM hakuna mwanachama aliye juu ya chama na kuwa maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya chama yanapaswa kuheshimiwa.

"Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika," alisisitiza Mgeja.

Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

"Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.

......................................................

Huyu ni mmojawapo wa 'viongozi' waliokunywa maji ya bendera ya kijani!
Khamis Mgeja ni muumini mzuri wa sisiem, hata wakati wa kutaka kumvua uanachama six alikuwa msitari wa mbele. Hongera , sana Mgeja kwa kupigania maslahi ya chama chako, kwa kuwa inaonekana chama kina imani na wewe basi peleka na ajenda ya ongezeko la bei zs umeme kwenye hicho kikao watakusikiliza na wananchi wa feel uwepo wako
 
Tatizo kubwa ni unafiki wa huyu mzee sitta kila wakati atakuwa kwenye hii hali, ukiamua usafi ni kwa asilimia 100, yeye analaumu tu kila kukicha, hili hali wengine ideology zetu ni 'no one is clean in ccm' aondoke tu ccm atafute sehemu nyingine, akishindwa akae kimya!!!!! yeye hana usafi wowote ule kutaka tu publicity, aacha upropaganda wake. unalaumu weee unabaki humo humo, akili hizo!!

Sikubaliani na hoja hii. Ndugu yangu unatakiwa ujue ya kwamba, huwezi kuibomoa CCM kisawa-sawa ukiwa umehamia CDM, CUF au kwingineko. Kumbuka msemo huu, FIMBO YA MBALI . . . .
Na hata JK ameshawahi kukiri ya kuwa, watu wanaoikosesha raha na usingizi mtamu CCM ni wapiganaji waliopo CCM, na wala sio walioko nje ya CCM. Watu kama hawa ndio tunaowahitaji sana wabaki CCM mpaka pale tutakapoona imeishiwa nguvu kabisa. Sitta akihama CCM atapoteza nguvu zoooote alizonazo, na CCM watafurahi sana. Hakuna aliyehama CCM akaenda kwingine halafu akaiyumbisha CCM. Abaki humo humo huku akichokonoa-chokonoa
 
Lakini mafisadi (JK na CCM yake) si ndio hao hao wamempa cheo alichonacho sasa. Sitta ni fisadi, kelele zake ni mbinu za kuomba apewe zaidi.

Six sio fisadi. Na ataendelea kuwa hivyo. Kupambana na ufisadi hutakiwi kususia vyeo. Wakikupa chukua, lakin endelea kupambana. Cheo wamempa kama njia ya kumtuliza na kumpooza kumtosa uspika.
 
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amemjia juu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akimtuhumu kwa kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

Kutokana na hatua hiyo, ameeleza nia ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili Sitta athibitishe madai yake.

Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

"Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja.

Mgeja ambaye kwa wadhifa wake ni Mjumbe wa NEC Taifa, alisema CCM hakuna mwanachama aliye juu ya chama na kuwa maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya chama yanapaswa kuheshimiwa.

"Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika," alisisitiza Mgeja.

Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

"Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.

......................................................

Huyu ni mmojawapo wa 'viongozi' waliokunywa maji ya bendera ya kijani!

A learned fool is more a fool than an ignorant fool.
 
Huyu Khamis Mgeja ni kama mshiba kunde, hayo ni mashuzi tu.
Kamati kuu ya CCM wamo Mafisadi tena wenye PhD za ufisadi watakosa kuwa n hila?
Vikao vya CCM vimetawaliwa na umbea utadhani ni vikao vya Machangu malaya wa Mtaa wa Ohio.
CCM kweli mmepatikana mwaka huu mmebana mmeshindwa sasa mmeamua kuachia tu tutaona mengi hasa yale yasiyoonyeshwa hadharani

Mkuu najua una uchungu sana na nchi yako lakini jitahidi kutumia tafsida ili kupunguza ukali wa meneno yako!!
 
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amemjia juu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akimtuhumu kwa kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

Kutokana na hatua hiyo, ameeleza nia ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili Sitta athibitishe madai yake.

Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

"Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja.

Mgeja ambaye kwa wadhifa wake ni Mjumbe wa NEC Taifa, alisema CCM hakuna mwanachama aliye juu ya chama na kuwa maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya chama yanapaswa kuheshimiwa.

"Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika," alisisitiza Mgeja.

Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

"Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.

......................................................

Huyu ni mmojawapo wa 'viongozi' waliokunywa maji ya bendera ya kijani!
mwenye CV yake kwanza ailete hapa.... hawa watu wanotaka umaaarufu kwa sababu ya 2015...wasitupotezee muda humu...!
 
Mgeja is an ignorant fool, hopeless kazi yake kubwa ni fitina na majungu ndani ya chama na kutumiwa na mafisadi kwa manufaa ya mafisadi, apeleke hiyo hoja yake ambayo itamuongezea Sitta umaarufu wa kisiasa. CCM mkoa wa Shinyanga iko taabani kwa kuongozwa na Mgeja na bila kuchakachua kura mwaka huu mkoa mzima walikuwa wamepata jimbo moja tu
 
Nasikia ukienda Muhimbili National Hospital kitengo cha PSY utakuta CV yake.
 
Yaani post zako ndio zile zile zinazo assume kuwa Kikwete ni SAFI, na kuwa Kikwete na hao mafisadi hawana mawasiliano, nani kawaroga nyie?? There is no way ukamtaja EL, RA JK asiwemo katika hii three cord company, no..way, tuache kudanganyana.

Logic ndogo tu, kama JK angeamua awaondoe mafisadi anaweza, aidha kawashindwa au yuko pamoja nao, na kama ameshindwa basi sio rais kuna rais wa siri!! ni hizo possibility mbili tu, HAWAWEZI AU YUKO NAO!! na kama hawawezi na kuna rais wa siri basi Sitta asingepewa hata uwaziri kwa mujibu wa post yako. TUAMKE JAMANI hizi logic zenu zimekufa na wala hazilipi kabisa, inakuwa kama mateja wanasimuliana bwana
Jk sio mjinga kiasi hicho (kwenye red) Anajua yaliyomkuta Umar Yaradua wa Nigeria alipopambana na mafisadi. Lakini mwaka huu kama mngempa sapoti ya kutosha basi angefanya hivyo, lakini mlichofanya ni kumhujumu ambapo ilipelekea kusaidiwa na hao mafisadi tena kuingia ikulu, sas haina haja ya kulalamika, na JK kula zako good time ikulu kwani watu wenyewe hawana shukurani hata ungefanya nini, na ikiwezekana nenda zako kabembee huko Trinidad and Tobaco. Waache waendelee kurap.
 
Sina nia ya kumtetea Sitta linapokuja suala la uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama chochote, kwa mfano kauli za Zitto pia zimeonekana kukikwaza chama chake cha chadema lakini natofautiana na Mgeja kuongea suala hilo na vyombo vya habari.Badala ya kuongea na vyombo vya habari, Mgeja angelipeleka suala hilo ndani ya chama chake kwanza au kuwajulisha viongozi wake wa kitaifa kwanza juu ya kusudio lake hilo.

Hapa ni kama anarumbana na Sitta hadharani bila kujua msimamo wa chama chake juu ya suala hilo na njia ya kufanya namna ya kumshauri bwana Sitta.

Pili, Mgeja ameongea na vyombo vya habari kuhusu ajenda ambayo pengine angetakiwa kuongea katibu mkuu wa chama Yusuf Makamba ili kukiepusha chama na malalamiko kwamba kila mtu siku hizi anataka kuwa msemaji wa chama bila kuzingatia taratibu. Njia hii mara nyingi husababisha marumbano kwenye vyombo vya habari kati ya wanachama kama kila mmoja ataamua kuongea na vyombo vya habari kuelezea msimamo wake juu ya matamshi ya Sitta au jambo lingine lolote.

Hivi unafikiri ni bahati mbaya au amekulupuka kuja kuongeaa?
ITS A WELL CALCULATED MOVE, Na uwakika hao wote wanajua kinachoendelea na sio kukurupuka!

KIfupi KATUMWA.
 
CCM wangekuwa makini wangeanza na huyu Mgeja. Upeo wake finyu ndio uliosababisha wakapoteza majimbo yote mawili Maswa.

Uko wapi wewe,majimbo yaliyoenda Upinzani ni,

Maswa mashariki-CDM

Maswa magharibi-CDM

Bukombe-CDM

Meatu-CDM

Bariadi-UDP
 
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amemjia juu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akimtuhumu kwa kuendeleza mgawanyiko ndani ya chama na sasa anamtaka afute kauli yake kuwa aliondolewa uspika kwa mizengwe na Kamati Kuu ya chama hicho tawala.

Kutokana na hatua hiyo, ameeleza nia ya kuwasilisha hoja binafsi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ili Sitta athibitishe madai yake.

Mgeja aliyasema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Sitta kuwa aliondolewa uspika kwa hila.

"Sitta anapaswa kufuta kauli yake kuwa aliondolewa kwa hila…kikao kilichofanya maamuzi kuhusu nafasi ya uspika ni Kamati Kuu ya CCM, kwa hiyo anamaanisha wajumbe wa kikao hicho wana hila naye.

Kusema hivyo kutasababisha baadhi ya wanachama kukosa imani na kikao hicho," alisema Mgeja.

Mgeja ambaye kwa wadhifa wake ni Mjumbe wa NEC Taifa, alisema CCM hakuna mwanachama aliye juu ya chama na kuwa maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya chama yanapaswa kuheshimiwa.

"Nitawasilisha hoja binafsi kwenye NEC ili kumtaka Sitta athibitishe kuwa amefanyiwa hila kwa kuwa kama hakuridhika na uamuzi, alipaswa kukata rufani kwenye vikao husika," alisisitiza Mgeja.

Alimlaumu spika huyo wa zamani kwa kuwa na kauli anayodai zinasababisha mgawanyiko na kuendeleza makundi kwenye chama.

Akizidi kumkosoa, Mgeja alisema hata kauli aliyoitoa Sitta juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans lilikuwa na lengo la kuibua chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo halikupaswa kufanywa na kiongozi kama huyo mwenye fursa ya kumshauri Rais kutokana na kuwa waziri.

"Uamuzi uliotolewa wa kuilipa Dowans fedha zote hizo kila Mtanzania unamuuma, lakini kauli za kukataa au kupinga huku ikijulikana suala hilo ni la kisheria, ni kutaka kuwapotosha wananchi kuhusu ukweli halisi," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Shinyanga.

Alimpongeza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa alivyolifafanua suala hilo mbele ya wahariri,
akieleza taratibu na sheria zinapaswa kufuatwa katika masuala yanayohusu sheria, kwani serikali inajali utawala bora.

......................................................

Huyu ni mmojawapo wa 'viongozi' waliokunywa maji ya bendera ya kijani!

Khamoooo Khamis Mgeja, Mbhehi ulelya manjemm shiii?????? Nene Natubhagha ghete na Mbhehi huyo!!!!!

Hivi kweli viongozi walioko ndani ya CCM wengine nadhani wanatakiwa kujua hii ni karne tofauti na zilizo pita huu ni wakati wa siasa za wazi na ukweli,

Mgeja kama kweli Sitta alifanya kazi nzuri bungeni na wananchi walimkubali kwanini CCM msimrudisheeee?? kama kweli mwahitaji siasa za kweli viongozi wengi wa CCM ndio wananafiki na wazandiki kuanzia na wewe Khamis Mgeja.

Viongozi wa CCM wengi wao wanakasumba mabaya sana wanashindwa tofautisha uwajibikaji na siasa za majukwaani, Plz watofautishe Siasa na Utendaji kazi, CCM mtu akikosoa chama ni dhambi kwani chama si kinaongozwa na watu ambao nao hukosea sasa tatizo liko wapi? chama kinaongozwa na taratibu zake na kanuni zake naka kama waliopewa wajibu wa kusimamia hizo taratibu na kanuni na hawazifuati lazima tu kuna mtu tu huko atasema iliyo wazi na utasikia watu kama wakina Mgeja wanajifanya wao ndio wamekunywa maji ya bendera ya Chama.

Sitta alichokisema ni sahihi kabisa.

Hiki chama mwakiua kabisa kwa tabia hizi hizi za kukataa ukweli na kutaka uongo, na kinakufa mikononi mwenu bila hata ya kubisha ngojeni

Pinda nae asiwapoteshe wananchi kwanini nasema hivyo anaposema ati utawala wa sheria ni hupi huo KATIBA ya nchi inasemaje?? mikataba yoyote ni lazima ipitishwe bungeni na ibalikiwa au hapana sasa huo Mkataba wa Richmond /Dowans nani aliupeleka Bungeni? na lini ulipelekwa? Nani ni muhusika majina yao yakuwapi mbona hapo kuna kuwa na ububu? ndio Utawala bora huo na sheria leo ndio mwakumbuka kuwa kuna utawala wa sheria na utawala bora??

Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa wapi kuiangalia hii mikataba na Tanesco? wanataka kutufanya sio ma zuzu? kuwa hatujui Utawala bora na wa sheria?

Me nasema na iko wazi na atakama mtu akiniuliza live ntaseam kiongozi yeyote anayesema mikataba ati ya kuhusu Dowans na Richmond ilifanyika kisheria huyo ni mnafki na mzandiki kwani hawajui katiba ya nchi inasemaje kuhusu mikataba? je hao sio wao ndio walio vunja sheria na katiba ya nchi kwanini wao leo wasema ati nchi ina utawala bora na washeria!! Sheria ipi hiyo?? ni upuuzi mtupu tuache haya mambo ya kuwafanya watanzania kuwa ni mazuzu mwa mlinda nani hapo kwa mikataba hiyo mibovu isiyo halali na ya kisheria na isiyofuata katiba ya nchi??
 
Back
Top Bottom