Moto Mbeya: Yule Polisi kwa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto Mbeya: Yule Polisi kwa nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Majoja, Sep 17, 2011.

 1. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tumeona janga lingine la moto kwenye soko la Sido Mwanjelwa Mbeya mjini. Kwenye luninga ITV jana jioni na leo asubuhi sote tumeona kilichotokea. Kilichonisikitisha sana ni kitendo cha askari aliyevaa kiraia akimrukia kwa teke la ninja mtuhumiwa ambaye tayari alikuwa amwekwa chini ya ulinzi. Mtuhumiwa huyu alikuwa amezungukwa na askari karibu wanne na mara kutoka kusiko julikana anatokea huyu askarai anamrukia mtuhumiwa.

  Cha kusikitisha zaidi askari wengine badala ya kufuata sheria wanaingilia na kumpiga mtuhumiwa kwa mateke ngumi nakadhalika.
  HILI NI KOSA LA JINAI. ITV inaoneka sehemu nyingi tu duniani na natumaini hata wakuu wa Polisi wameona hili. Hatua lazima zichukuliwe.

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hahaaaa sikubahatika kuiona hii movie, CD zake nitazipata wapi??
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hao ndio polisi, jeshi la polisi ambalo ndio serikali ya ccm imelitengeneza na kulifanya hivyo lilivyo.
  Miaka hamsini ya uhuru wa utovu wa nidhamu wa jeshi la polisi. Miaka hamsini ya ukiukwaji wa haki za binadamu, 50 yrs ya jeshi la polisi kuua raia bila kuhojiwa wala kushtakiwa.

  hiyo ndio ccm haswa mnayotakiwa kuifahamu.
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Utawalaumu wakati wamefunzwa hivyo?
   
 5. M

  Marco Mwaimu Member

  #5
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena hili ni kosa na hapo ndio jaribu jingine la kuona kama serikali yetu ni makini au laaa
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Elimu ndogo nayo inachangia..wengi wao ni std 7 walofoji vyeti..
   
 7. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi wanaiba na vibaka wanaiba, polisi wanapozidiwa ujanja ni kutumia nguvu ili kutengeneza mazingira mazuri ya wao kuiba. Baada ya kushindika polisi waliamua kusimamia vibanda vyote viteketee mota.
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Inaelekea elimu ya utawala bora inaishia kwenye semina za kina IGP Mwema na maofisa wengine.
  Huko chini sheria haijulikani ni nini
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,257
  Trophy Points: 280
  Polisi wa CCM hao unadhani watakuwa na jipya??
   
 10. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ni tatizo la kisaikolojia,wana maisha magumu,posho ni kutokana na rushwa tu,mishahara haitoshi,wako bize kuonyesha kazi yao ni nzuri na inalipa wakati sio,hawajui wamlilie nani,wanaishi na hasira na msongo wa mawazo kila siku,huishi wakitafuta wapi pa kupunguzia hasira zao,ghafla wanakutana na mtuhumiwa then wanapata faraja kwa kumpiga ili kupunguza hasira zao.MUNGU IBARIKI TZ
   
 11. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umenena! Ingawa polisi duniani kote mishara si mikubwa ila nchi nyingi zilichofanya ni kupunguza gap! Na lingine tatizo la bongo polisi wengi ni std 7 a.k.a LY wa enzi zile je sasa tukifikiria mishara yao tufanyeje?
   
 12. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  kumbe hii imewatach hata nyie yan da
   
 13. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Bwana mukubwa Nkwesa Makambo, nakubaiana na wewe lakini kitendo cha kumpiga mtuhumiwa AMBAYE YUKO CHINI YA ULINZI NI KITENDO CHA KIHUNI.
  Natumaini IGP Mwema naye amiona hiyo picha toka stting room yake na naomba achukue hatua za kinidhamu juu ya hili.
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kile kitendo kimesitikisha watu wote wanajua haki za binadamu....naungana na wote kulaani kile kitendo kwa nguvu zote, kama inawezekana aliejeruhiwa anastahili kufungua mashtaka na ushahidi upo wazi itv
   
 15. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Ni washenzi tena washenzi wavuta bangi wakubwa na wahuni wale, hawana tofauti na genge la majambazi, niliumia sana maana juzi iliripotiwa kuwa walimpiga bibi kizee na kumpora tena maskini wa MUNGU alikua nyumbani kisa wanadai eti kahusika kwenye maandamano! Narudia tena ni washenzi na siku ni afadhali kujilipua nife kuliko kuona dhuluma ile, nilishindwa kuangalia matukio yale, je vipi kwa yale ambayo hayajaripotiwa??? Ni mangapi? ni wangapi wanafia mikononi mwao? I hate them to death!
   
 16. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  daaah...............sheria wanazifahamu lakini hawazifuati
   
 17. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  I dont think your fair at all! kipigo unachokisema na lawama unazotaka kusema hujaangalia kwa upande wa pili namna ambavyo vibaka hao walipelekea zoezi lenyewe kuwa gumu katka kuzima moto. kwa lugha rahisi, mwenendo uliojitokeza kwa baadhi ya watu asilimia kubwa wa kuthubutu kuiba na wakati huo huo kufanya zoezi la kuzima moto kuwa gumu ni uhaini tena ni kiashiria kitakachopelekea soko lingine kuchomwa tena ili waweze kujichukulia mali za watu kwa kupora. niwaombe enyi wapigania haki za wahalifu kwa madai ni haki za binadamu mkumbuke hata siku moja mtu/binadamu hawezi kuwa na majina mawili yaani mhalifu/mwizi na wakati huo huo ukamwita binadamu. lakini pia kumbuka umeona kwenye tv tu na unajenga hoja na siye tuliopokonywa na kunyanganywa mali zetu kimachomacho tutafika wapi? ambao kwa sasa tunakazi ya kuwatafuta wanyanganyi wetu ili tuwakate vichwa?
   
 18. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  mmm? kweli pana kazi hajo inajadiliwa na watu kana kwamba iwalikuwepo na waliona kilichokuwa kinaendelea? wenzenu vibaka walituumiza vibaya na kama kundi mliloliona kwenye televisheni wasingekuja zoezi la kuzima lilikuwa rahisi sana. sisi wafanyabiashara tunalaumu jeshi la polisi kwanza kwa kushindwa kuwadhibiti raia na vibaka kuingia sokoni, na kusababisha msongamano mkubwa wa bila sababu na kupelekea zimamoto na kushindwa kufanya kazi kirahisi na mbaya zaidi hata namna ya kuokoa mali zetu kushindikana kwani ukitoa nje wao wanafaulisha, ukipakia kwenye gari wananyanganya, na mbaya zaidi hata ambako moto haujafika walithubutu kuvunja makufuli, mfano ni huyo jamaa aliyepigwa na polisi kwa kupora mali za watu.
   
Loading...