Tetesi: MOSSAD wafanya yao

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
6,838
14,221
Muda si mrefu, majasusi, wa, MOSSAD, wamefanya assassination kwenye viunga vya Lebanon, maeneo ya Hezbollah, wamemuua kiongozi, mkubwa wa, Hamas, sasa, ni Vita kila eneo, militarily, na covert operations, ubaya, wake, Hamas, na, wanaomuunga mkono, watalipa kisasi popote yalipo maslahi, ya Israel duniani.

Kazi, ya, intelijensia ndio hiyo, unakuwa, na, mkono mrefu, wakati army wanapigana kwa bunduki kwa kuona na, wewe unakwenda, "behind enemy lines"

Vita ndio kwanza imeanza.

Sio TISS wetu,tunaonyanganya mademu baa, kila siku, wanagombana na daladala, na mbwembwe za kuwasha vingora.
 
Wameshindwa kuokoa mateka Gaza hadi leo , wameshindwa kuishauri serikali yao kuepuka kupata aibu kutokea Gaza hadi sasa maana kuepuka vita ya aibu nao ni ushindi.
 
Hao mosad tangu washindwe kujua ni wapi walipo mateka wakati wamezuiliwa sebureni kwake watu wamejua kuwa uwezo wao uko kipropaganda zaidi kuliko uhalisia.
Hilo shambulizi halina weredi wowote wa kijasusi ni shambulizi la kuvizia sababu ofisi za jamaa zilikuwa zinajulikana zilipo na alikuwa anasafiri sana tu hivyo Israel wangetaka kumuuwa wangemuuwa tangu zamani tu hivyo suala la kumuuwa lilikuwa lina subiri amri itolewe tu.

Haya mauaji yamefanywa kwa lengo fulani tu la kisiasa ndani Israel.
 
Saleh al-Arouri moja ya waanzilishi na kiongozi wa juu kabisa wa Hamas amelambwa kichwa Lebanon.
Israel covert operations hazitowasaidia muda huu, wakubali wameshindwa basi yaishe, wameshindwa kutumia ujasusi wao kuokoa mateka pale Gaza wanakwenda Lebanon kuua watu.
 
Hamas Kuja kushtuka watakuta viongozi wote hawapo na Gaza Imeteketea🤔
Hamas mwasisi Ahmad Yasini , akina Al rantisi walikuwa assasinated ila leo hii wamepata viongozi wengine wakali zaidi hata hao watapigwa wataibuka wengine wenye misimamo mikali suluhu ni dialogue na two state solution basi ili kuwe na amani ila kuua viongozi wa watu millioni 2 ni rahisi kupata mwingine historia imeonyesha hivyo.
 
Sijui wamewaza nini lakini lazima Hamas na Hezbollah wajibu.
Usijitoe Akili.
Israel tangu tukio la 7 oktoba walisema haya.
1. Kila aliyehusika katika kupanga au kushiriki mauaji ya 7 oktoba popote pale alipo duniani ajiandae kufikiwa na kuuwawa.

2. Operesheni ya sasa huko Gaza imelenga kulifuta kabisa kundi la Hamas.

Katika hali hiyo unategemea kuna kiongozi wa Hamas atakayebakia hai?
 
Hamas mwasisi Ahmad Yasini , akina Al rantisi walikuwa assasinated ila leo hii wamepata viongozi wengine wakali zaidi hata hao watapigwa wataibuka wengine wenye misimamo mikali suluhu ni dialogue na two state solution basi ili kuwe na amani ila kuua viongozi wa watu millioni 2 ni rahisi kupata mwingine historia imeonyesha hivyo.
Naona kama unawaza kinyume. Sasa hapo Gaza ambapo watu zaidi ya million 2 wapo displaced na hawana chakula mpaka jumuiya za kimataifa zinapiga kelele. Nani kanyooshwa hapo?
 
Jamani tuwe wakweli, hamas hana namna ya kushinda Israel, hamas wanapoteza muda, na hili itawagharimu sana hamas na wapalestina, two states ni too rate, na haitawezekana, dai la hamas na Iran ni kuifuta Israel kwenye tamani ya dunia( yaani kuliangamiza taifa la Israel ili wapalestina wachukue ardhi)
Kwa mazingira hayo Israel hana chaguo lingine ni vita na kuwaangamiza hamasi.
 
Ila kuuawawa kwa huyu jamaa kumewashtua sana hadi kina Ayatollah hawatoki nje. Tena huyu jamaa alikuwa na appointment na Nasrallah bosi wa kundi la kigaidi la Hezbollah kesho jumatano.

Na huyu balozi wa Palestina tz naye awe makini asijiachie tu kina Ponda wanaweza kuwa Mossad.

God bless and protect Israel

ISRAEL FOREVER
 
Usijitoe Akili.
Israel tangu tukio la 7 oktoba walisema haya.
1. Kila aliyehusika katika kupanga au kushiriki mauaji ya 7 oktoba popote pale alipo duniani ajiandae kufikiwa na kuuwawa.

2. Operesheni ya sasa huko Gaza imelenga kulifuta kabisa kundi la Hamas.

Katika hali hiyo unategemea kuna kiongozi wa Hamas atakayebakia hai?
Hamas ipo tangu 1987, miaka yote hio waje waifute leo, hizo tunaita ni kauli za kuwatia moyo wananchi na kutaka sifa, lakini hawana huwezo kuifuta Hamas.
 
Ila kuuawawa kwa huyu jamaa kumewashtua sana hadi kina Ayatollah hawatoki nje. Tena huyu jamaa alikuwa na appointment na Nasrallah bosi wa kundi la kigaidi la Hezbollah kesho jumatano.

Na huyu balozi wa Palestina tz naye awe makini asijiachie tu kina Ponda wanaweza kuwa Mossad.

God bless and protect Israel

ISRAEL FOREVER
Toka 1987 Israel imeua viongozi wengi wa Hamas, ndio maana tunasema hii sio solution, covert opertaion sio wakati wake huu a focus na vita Gaza.
 
Back
Top Bottom