Huifahamu vizuri historia ya hao kina Nyetanyahu wewe, halafu bahati mbaya sana sijui hua kwanini lazima uanze na kutukuna watu, kama kitu hukijui vizuri sio vibaya kujifunza. Ngoja tena nikwambie habari za hao kina Nyetanyahu; baba yake huyu jamaa anaeitwa Benyamini Nyetanyahu alikua mwalimu wa dini, kwa huku kwetu ungeweza kusema Sheikh au askofu, wao wanatumia neon RABI kwa lugha ya Kiebrania ( Kiisrael au ukipenda kwa leo sema Kiyahudi ). Yule jamaa aliyekua master mind wa ukombozi wa wale Wayahudi waliotekwa na Idd Amini miaka ya mwanzoni mwa 70 alikua kaka wa huyu waziri mkuu wa sasa, alikua anaitwa Jonathan Nyetanyahu, dogo alikua anasoma shule kwa kuahirisha ahirisha sana kwasababu ya vita na vita iliompotezea sana muda ni ile ya 1967 ile ya Waarabu dhidi ya taifa hilo, huyu dogo alizaliwa USA cause baba yake alikua akisafiri mara kwa mara kati ya USA na Israel wakati huyu Benyamini (soma Benjamini ) kazaliwa hapo hapo Israel, endelea kujidanganya kwamba jamaa ni mzungu. Hao watu hawana rangi moja, kuna Wazungu, waarabu, machotara wa Kiafrica na Kizungu nk; utofauti wao wa rangi ndio uliosaidia sana kuifana Mosaid kua strong hivyo ilivyo leo. Unakumbuka aliyeharibu ile misheni ya Waarabu pale Misri miaka hiyo hiyo ya 60 mwishoni? Kwa taarifa yako, alikua mke wa mkuu wa majeshi wa Misri, mkuu wa majeshi alijua mkewe ni Mwarabu (Mmisri ) mwenzie, kumbe nae alikua Myahudi vile vile. Hawa jamaa uwachukie, uwapende, ndivyo walivyo.