Moshi: Majeneza yaadimika

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,909
25,183
Na Mary Mosha, MOSHI

HUDUMA za mazishi na uuzaji wa majeneza kwenye Mji wa Moshi zimetajwa kuongezeka katika siku za karibuni.

Kutokana na ongezeko hilo, baadhi ya watoa huduma wameiomba serikali kuona namna ya kuwasaidia wasilipe kodi na tozo mbalimbali kwa kuzingatia wanatoa huduma na sio biashara.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti mjini hapa, baadhi ya watoa huduma hao, akiwamo France Temba wa Mtaa wa KCMC, walisema kwa sasa majeneza yamekuwa yakitoka kwa wingi kiasi cha kuwalazimu kufanya kazi mchana na usiku. "Kwa hapa kwetu majeneza yanaanzia Sh. 150,000 hadi 1,000,000.

Kwa sasa yanachukuliwa sana, yaani kwa siku yanatoka matano mpaka tisa hasa ya kuanzia Sh. 400,000 kurudi chini wakati huko nyuma yalikuwa yakitoka mawili hadi matatu kwa wiki. "Hii ina maana kwamba watu wanakwenda (wanafariki dunia) na ni wale wa hali za maisha ya kawaida," alibainisha.

Mtoa huduma huyo alisema upatikanaji wa malighafi, ikiwamo mbao, rangi na urembo, umekuwa mgumu, hivyo wanaomba serikali ifikirie kuwapunguzia gharama.

Elinasari Nkyini alisema: "Sisi hutengeneza majeneza usiku na mchana, tumeongeza vijana wa kazi, kuna siku watu wanakuja wanane hadi 14 wakitaka majeneza ya kesho yake na siku mbili mbeleni, hivyo inatulazimu ku-hakikisha huduma inapatikana lakini tunakabilica na matatizo mengi kwa sasa ikiwamo upati-kanaji wa malighafi."

Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya huduma za mazishi ya Godmark, Lucas Gondwe, alisema kwa takribani miezi miwili sasa, biashara imebadilika ghafla na uhitaji umekuwa mkubwa tofauti na kipindi cha nyuma. Alisema kwa sasa wanatoa majeneza matatu hadi manne kwa siku, ambapo awali walikuwa wanatoa idadi hiyo kwa wiki. "Katika kampuni yetu tunatoa huduma hiyo kwa gharama za kuanzia Sh. 400,000 hadi 4,000,000, inategemea na ubora na malighafi zilizotumika. "Kwa sasa ipo haja serikali kuona namna ya kuwasaidia watoa huduma za mazishi nchini ili watoe huduma bora kwa kwa wahitaji. "Kwa sasa tunachajivva kodi kubwa, malighafi zimekuwa ghali, ulipaji wa pango, leseni za biashara, watu huja hapa bila pesa na tunalazimika kuwapa huduma baada ya mazishi walete hela, cha ajabu wengine hata simu hawapokei tena," alisema.

Baadhi ya wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma ya majeneza katika barabara ya KCMC, akiwamo Faustina Kimario, walisema kwa sasa huduma ya majeneza imekuwa ngumu kuipata. "Sisi tuliweka oda ya jeneza la kumzika ndugu yetu juzi lakini tumefika hapa leo bado halijaandaliwa na tumelazimika kuahirisha shughuli yetu hadi Jumamosi, tumezunguka kutafuta hakuna yaliyopo tayari, Serikali iangalie suala hili. "Kwa sasa ukipatwa na msiba, kabla ya kwenda kutafuta viongozi wa dini na kukaa kikao cha familia, inabidi uende kwanza kutafuta jeneza, inasikitisha inahuzunisha, tunapoelekea watu wanaweza kuzikwa bila majeneza," alisema Zawad Mlay.

Pia unaweza kupitia, hali ilivyokuwa 2018👇
 
Miili mingi ya watu wa moshi kinga ni ndogo sana kwa sababu ya pombe.Mwenyezi mungu awaepushe na hili gonjwa waliobaki hai.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Unajua unaweza kuwa mpumbavu lakini watu wasijue wewe ni mpumbavu kwa sababu huonyeshi hadharani. Huko Ulaya, India, Brazil na Marekani kulikotokea vifo vingi nako miili yao haina kinga kwa sababu ya pombe? Idiot!
 


Watu wabishi sana ☝️ nyingine hiyo
 
Inaelekea wewe ni mnywaji pombe mzuri, acha pombe ndugu utakufa
Kitu chochote kikitumika zaidi na inavyotakiwa ni hatari? Hivi unajua hata ukizidisha ulaji wa nyama ni hatari? Unajua ukizidisha unwaji wa juisi nayo ni hatari? Kwa kifupi pombe as long as unatumia kwa kiasi siyo mbaya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom