Moses Machali amrithi David Kafulila NCCR Mageuzi

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
KATIBU Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi Samwel Ruhuza amemteua Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali kuwa Katibu wa Uenezi wa chama hicho akichukua nafasi iliyoachwa wazi na mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alivuliwa uanachama wa chama hicho Desemba 17 mwaka jana.

Katika hatua nyingine Ruhuza alisema leo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho(NEC) wakiongozwa na Peterson Mshenyerwa na Sebastian Sebeki watafanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Nguruka mjini ambayo ndio kambi kubwa ya Kafulila.

Mbona kazi ipo!!!

CHANZO:
Mwananchi
 
Hao NCCR hawana taarifa za kutosha kuhusu afya ya akili ya Mhe. Moses Machali. Yangu macho!
 
Machali aliitafuta nafasi hiyo siku nyingi sana kwa kinyume na Kafulila na kuambatana na Mbatia. Ngoja niwaulize washikaji wa Murufiti, Nyansha, Heru, Msambara nISIKIE MAONI YAO
 
Kufa kufaana machali aliongoza kambi ya kumfukuza kafulila uanachama sasa kachukua mikoba ya kafulila
 
Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NSSR Mageuzi Mh Moses Joseph Machali ameteuliwa rasmi kushika nafasi ya Katibu uenezi wa chama,
nafasi iliyoachwa wazi na David Kafulila ambae chama kilimvua wazifa huo mapema kabla ya kumfukuza uanachama.

Uteuzi huo umefanywa jana na Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi Bw Sam Luhuza.
 
Nape, Mnyika, Machali, WAENEZI wa nguvu kabisa. Bado CUF au Mtatiro na Jussa wanatosha?

patam hapo mi naomba waandaliwe mdahalo hasa juu ya dhna ya kuwajibishana maana inawahusu sana Nape anawadis mafisadi,mnyika anamdisi shibuda na machali anamdis kafulila.kaz ipo
 
Hao wajumbe wa NEC wanaokwenda kufanya mkutano nguruka nadhani kitakuwa kipimo halisi cha kukubalika kwa kafulila na ushawishi wa nccr mageuzi.
 
Mkuu WildCard kati ya hao ni yupe BORA kabisa
Nape. Anatumikia uongozi mgumu sana lakini anafurukuta kidogo. Mnyika hana akili inayojitegemea anapokuwa ndani ya CHADEMA. Machali ni mropokaji fulani hivi ambaye hatadumu kwenye nafasi hiyo.
 
Kwani NCCR nao ni tishio kwa chama kama CCM? mi naona vyama vyengine vipo tu havinaga ubaga!
 
Katika hili kaka Moses kachemka sana........yaani haitaji hata elimu ya darasa la saba kufahamu kua Moses alikua na lake jambo na amehusika sana katika kumshughulikia Kafulila...................................kumbe mbio zote hzi anataka nafasi ya Uenezi............................kweli siasa za bongo full Unafiki..................R.I.P NCCR Magazeti
 
Nape. Anatumikia uongozi mgumu sana lakini anafurukuta kidogo. Mnyika hana akili inayojitegemea anapokuwa ndani ya CHADEMA. Machali ni mropokaji fulani hivi ambaye hatadumu kwenye nafasi hiyo.

Ili uitwe kiongozi ni lazime kuwepo na zaidi ya watu wawili walio na safari moja, malengo yanayofanana n.k. Katika hali hiyo ili uitwe kiongozi bora ni muhimu uwe na akili inayothamini vilevile akili za hao unaowaongoza. Sasa naja kwenye maandishi mekundu, Mnyika ni kiongozi bora kwa kuwa anajenga hoja na hoja inapojadiliwa na wengi kutoa msimamo tofauti anayoamini, hujirudi na kukubali mawazo hayo. Tumeona wengi wanaharibu na kuvuruga utaratibu kwa kuwa tu mawazo yake yamekataliwa na wengi. Watu wa jinsi hiyo ni waanzilishi wa migogoro isiyoisha ndani ya jumuiya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom