Joseph Selasini atimuliwa NCCR Mageuzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,561
217,866
Imeripotiwa kwamba mamluki Joseph Selasini, aliyeongoza mapinduzi haramu ndani ya chama cha NCCR Mageuzi ametimuliwa rasmi baada ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kumtambua rasmi Mbatia kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho. Mwingine aliyetimuliwa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Usaliti ni laana.

Chanzo: Raia Mwema.
 
Hivi ni kwanini watu wa vyama vya siasa hapa nchini mtu waliyetofautiana naye itikadi wanamuita msaliti?

Watu wengi wa vyama vya siasa ni washabiki wa demokrasia lakini sio waumini wa demokrasia.......kwao demokrasia ni kuwa na mawazo na fikra wanazozipenda wao.......maoni au utashi wako ukienda kinyume na nafsi zao.....ndio unaziona rangi zao halisi.

Harakati za kupambania demokrasia hapa nchini bado Zina safari ndefu sana kwa kuwa hata hao wanaojipambanua kuwa Wana harakati wa demokrasia ndio watu kwa kwanza kuivunja demokrasia.

Sote tunaona matusi yanayoporomoshwa humu na watu wanaojiita watu demokrasia dhidi ya mtu au watu walioamua kuwaza tofauti matamanio ya nafsi zao.

NB; Hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye kukomaa kidemokrasia ni kuimarisha kiwango chako Cha uvumilivu.
 
Hivi ni kwanini watu wa vyama vya siasa hapa nchini mtu waliyetofautiana naye itikadi wanamuita msaliti......??

Watu wengi wa vyama vya siasa ni washabiki wa demokrasia lakini sio waumini wa demokrasia.......kwao demokrasia ni kuwa na mawazo na fikra wanazozipenda wao....
Hiyo NB yako nadhani ndio kitu ambacho Selasini hana .
 
Imeripotiwa kwamba Mamluki Joseph Selasini , aliyeongoza Mapinduzi haramu ndani ya Chama cha NCCR MAGEUZI ametimuliwa rasmi baada ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kumtambua rasmi Mbatia kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho.

Wengine kadhaa waliotimuliwa yumo Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Chanzo : Raia Mwema.

Usaliti ni laana.
Selasinni aungane na John Shibuda
 
Imeripotiwa kwamba Mamluki Joseph Selasini , aliyeongoza Mapinduzi haramu ndani ya Chama cha NCCR MAGEUZI ametimuliwa rasmi baada ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kumtambua rasmi Mbatia kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho.

Wengine kadhaa waliotimuliwa yumo Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Chanzo : Raia Mwema.

Usaliti ni laana.
Serikali inapaswa kuimarisha demokrasia ndani ya Chama cha Siasa na siyo kulea kea usalitu.

NCCR wajiimariahe kusonga mbele
 
π™°πš—πšŠπšžπšπšŠπš”πšŠ πšžπš πšŽπš—πš’πšŽπš”πš’πšπš’ πš”πš πšŠ πš–πšŠπš™πš’πš—πšπšžπš£πš’
Kama uchaguzi haulaeti matokeo sahihi, hakuna namna
 
Hivi ni kwanini watu wa vyama vya siasa hapa nchini mtu waliyetofautiana naye itikadi wanamuita msaliti......??

Watu wengi wa vyama vya siasa ni washabiki wa demokrasia lakini sio waumini wa demokrasia.......kwao demokrasia ni kuwa na mawazo na fikra wanazozipenda wao.......maoni au utashi wako ukienda kinyume na nafsi zao.....ndio unaziona rangi zao halisi............

Harakati za kupambania demokrasia hapa nchini bado Zina safari ndefu sana kwa kuwa hata hao wanaojipambanua kuwa Wana harakati wa demokrasia ndio watu kwa kwanza kuivunja demokrasia......

Sote tunaona matusi yanayoporomoshwa humu na watu wanaojiita watu demokrasia dhidi ya mtu au watu walioamua kuwaza tofauti matamanio ya nafsi zao.........

NB;
Hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye kukomaa kidemokrasia ni kuimarisha kiwango chako Cha uvumilivu.....
Tafta kamusi usome neno Msaliti then soma neno Demokrasia utapata jibu Thelasini yupo kundi gani
 
Ndugu, inaelekea kuwa maoni haya yanahisia za kuonewa kwa Selasin.

Labda tukumbashane kuwa siyo kwamba demokrasia ni kuongea lolote, popote kwa yeyote, la hasha. Demokrasia ina kanuni, taratibu na sheria pia.

Demokrasia ndani ya kundi huanzia pale mlipokubaliana taratibu na kanuni za uendeshaji wa demokrasia hiyo. Hivyo ukikiuka taratibu ulizozikubali kisha hizohizo zikatumika kukuhukumu hiyo Ndiyo haki yako.

Na ukienda kinyume na hizo taratibu ulizozikubali kuwa ndani yake basi neno MSALITI ni haki yako.

Nadhani utakuwa umeelewa dhana ya MSALITI ktk demokrasia.
 
Tafta kamusi usome neno Msaliti then soma neno Demokrasia utapata jibu Thelasini yupo kundi gani

Ndugu, inaelekea kuwa maoni haya yanahisia za kuonewa kwa Season.

Labda tukumbashane kuwa siyo kwamba demokrasia ni kuongea lolote, popote kwa yeyote, la hasha. Demokrasia ina kanuni, taratibu na sheria pia.

Demokrasia ndani ya kundi huanzia pale mlipokubaliana taratibu na kanuni za uendeshaji wa demokrasia hiyo. Hivyo ukikiuka taratibu ulizozikubali kisha hizohizo zikatumika kukuhukumu hiyo Ndiyo haki yako.

Na ukienda kinyume na hizo taratibu ulizozikubali kuwa ndani yake basi neno MSALITI ni haki yako.

Nadhani utakuwa umeelewa dhana ya MSALITI ktk demokrasia.
Nimekuelewa vyema ndugu na Asante kwa kuchukua muda wako kumuelewesha......kwa namna moja au nyingine anaweza kuwa msaliti lakini tafsri ya neno msaliti nadhani Kuna baadhi ya watu wanalitafsiri vibaya......kwa mfano mnaweza kulipinga jambo ambalo limepita kwa mfumo wa wengi wape lakini wewe ukaamua kubakia msimamo wako na bado ukaonekana msaliti....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom