Moses Lijenje aliyetajwa kutupwa na Polisi kesi ya ugaidi ya Mbowe na wenzake ni nani?

Kesi isifutwe ili tujue mengi
Hii kesi badala ya kuleta amani uraiani kwa kuwafungia gaidi mbowe na wenzake inakoelekea italeta machafuko nchini, kwa sababu hii kesi inaeleweka ni ya kisiasa, sasa haya mambo ya jeshi la polisi kuanza kuonekana linaua watu litawaletea shida hawa askari huku vituoni kwao mitaani.

huyu mama wa kizanzibar nimeishasema afute hii kesi, haya mambo ya askari kuua watu yalikuwa awamu ya tano huko, sasa hawa kina kingai wanataka kuanza kuyaambatanisha na awamu ya sita.
 
Hakuna cha kunuka wala nini jeshi lenyewe ni sehemu ya CCM
I wish I cud b aijipi....naanza kuelewa. Kweli polisi wetu wanawatesa jwtz...tena ile torturing kwenye killing zone. Huu ni udhalilishaji....jw ni jeshi lenye heshima sana kwa wananchi....rejea vita vya uganda. Kwa vyovyote hii kesi itakavyoisha......kitanuka
 
Wakati shahidi namba mbili na mshitakiwa namba tatu Mohammed Abdilah Ling'wenya wa kesi ndogo katika kesi ya Ugaidi inayowakabili kina Mbowe alimtaja Mosses Lijenje kudaiwa kutupwa na polisi wakati akifanyiwa vitisho.

Mallya: Kitu gani Kiliendelea..?

Shahidi: Maaskari wakasema Mwenzenu Moses Lijenje tumeshamtupa, Ameshatangulia huku wakinigusa Kichwani na Kitu nilichokuwa nahisi kuwa ni Bastola, Ukileta Ujanja Ujanja na wewe tunakutupa

Mallya: Maneno haya ulikuwa unaambiwa wakati gani wakati wa Safari au baada ya Kufika


Huyu Moses Lijenje ni nani?

Je yupo wapi?

Je yupo hai?

Je anahusika vipi na hawa makomando?

Je anahusika vipi na hii kesi ya Mbowe?

Shahidi anaposema polisi kudai wameshamtupa wanamaanisha nini?

Hili limeniacha na maswali mengi sana ya kutafakari.
Plc wanatesa jw duh cjawai kusikia hii ni dharau
 
Kwanza, unamuomba rais kuingilia mahakama. Kama Mbowe na wenzake hawana hatia, ni kazi ya mahakamas kuamuwa kuwa hawana hatia. Je, kumshauri raisi aingilkie huo ni utawala bora. Kwani wewe una wasiwasi gani? Kama Mbowe hakutenda kosa la ugaidi, ataachiwa.
Tanzania hakuna separation of power kati ya mhimili wa mahakama na mhimili wa executive.Unaelewa kuwa DPP ni mkono wa Rais katika mahakama?

Katiba tuliyo nayo ni useless na ni ya hovyo sana ndiyo maana tunahitaji katiba mpya.Kwa katiba tuliyonayo kusema kuwa Rais huwa haingilii mahakama ni kujidanganya.
 
Back
Top Bottom