TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 5,722
- 10,226
TUSILALE USINGIZI PASIPO KUJUA MOSES LIJENJE YUKO WAPI NA ANA HALI GANI!
Kamanda Kingai na Afande Mahita katika nyakati tofauti kila mmoja akiwa chini ya kiapo, walitoa ushahidi Mahakamani kuwa walikuwa wakimtafuta mtuhumiwa Moses Lijenje kule Moshi. Lakini mmoja wa watuhumiwa hao (aliyesadikiwa kuwa pamoja na Moses Lijenje katika program ya VIP Protection ya Mbowe); akiongozwa na Mawakili wa Utetezi, ameieleza Mahakama mara kadhaa juu ya Moses Lijenje.
Shahidi (mtuhumiwa) huyo ameieleza Mahakama kuwa alipokuwa akiteswa, alitishwa na mmoja wa wasulubu (Polisi) wake huku akigusishwa bastola kichwani kuwa na yeye angelitupwa kama alivyotupwa Moses Lijenje bila kutaja alitupwaje na alitupwa wapi na kwa sababu gani. Kwa maneno mengine, wasulubu (Polisi) hao ndio 'walimtupa Moses Lijenje'!
Mambo mengine ni ya Jaji na Mahakama, sisi watetezi wa haki tuna jambo letu. Kama watetezi wa haki ni lazima tutake kujua Moses Lijenje yuko wapi na hali yake ikoje huko aliko. Kama kweli ametupwa, ametupwa na nani na kwa sababu gani na ametupwa wapi na hali yake ikoje huko aliko? Kutupwa huko kuna maana gani? Kesi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu kuisha, lakini hiyo haituzuii sisi watetezi wa haki kutafuta kujua wapi aliko mtu anayeitwa Moses Lijenje na hali yake ikoje.
Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito wa kila Mtanzania kufanya 'manhunt' yaani kuanza kumtafuta mtu aitwaye Moses Lijenje kuanzia muda huu. Jeshi la Polisi linao wajibu wa kuuambia umma ni wapi alipo ndugu Moses Lijenje! Paza sauti yako kwa kusema, kuandika na kusambaza ujumbe hadi uwafikie walio karibu na Lijenje, wanaomhifadhi, alikokimbilia au waliomtupa!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula