Siku moja mida ya jioni hivi napita maeneo ya Karume mbele kidogo baada ya kuvuka mataa nikishika njia ya kwenda Kinondoni, ilikuwa mida ya sa 1 jioni kuangalia barabarani katikati Polisi amemkamata mwendesha Boda akitaka asimame, lakini jamaa kagoma hivyo anaendesha boda lakini kashikwa na kukatokea mvutano hatari pale kiasi kwamba hata magari yanapita kwa tabu, na rahisi sana kusababisha ajali.
Abiria wakiwa ndani ya gari walitaka waruke kupitia dirishani ili wakampe kipigo yule polisi maana walikuwa wakimtukana na kumpigia kelele lakini wapi. Na jinsi nilivyoona yule polisi alikuwa na roho mbaya sana huwezi kumshika mwenzio vile katikati ya barabara, na hata jinsi alivyoact aisee nilimuona ni zaidi ya gaidi au jitu la ajabu sana, wana roho nyeusi hawa viumbe, sijui wakikutana na marafiki au ndugu zao waendesha boda sijui kama wanafanya hivi.