Wadau nimeipata hii sehemu ila siiamini. Hebu someni na nyie.
TAARIFA ZA HIVI PUNDE
Askari was pikipki wa Jeshi LA police Morogoro waliokua wakitumia pikipiki no PT 823 Mali ya jeshi la police wamewekwa chini ya ulinzi na raia eneo la Mindu na raia wamemuua mmoja wao aitwae Ramadhani.
Chanzo cha sakata hili ni ajali ya pikipiki waliokua wakiifukuza ambapo ilimshinda dreva bodaboda na kuingia kwenye lori, ndipo raia walipoanza kuwatuhumu police ni chanzo cha ajali na police waliamua kufyatua risasi hewani. Hali ikawa tofauti, baadala ya raia kutawanyika waliongezeka na kuwazidi nguvu askari.
Cha kushangaza raia wamemuuwa kwa mawe askari mmoja na mwingine walimwambia yeye hana makosa. Aliyeuwawa ni yule anaedaiwa kumuua marehremu Ali Zona, muuza magazeti katika harakati za maandamano ya CHADEMA 2011.