Morogoro: Katibu CCM afariki dunia

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimepata pigo kutokana na kifo cha Katibu wa Mkoa huo, Asha Kipangula, aliyefariki leo asubuhi katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam.

Habari za kifo hicho zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhandisi Petro Kingu.

asha+kipangula.jpg

Hata hivyo, taarifa za awali zinasema mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda mkoani Iringa kwa maziko yatakayofanyika fanyika kesho kutwa.

Kipangula alihamia Morogoro mwaka 2009 akitokea Tabora, lakini wakati anahamia alikuwa na wadhifa wa Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa.
 
Asha Kipangula kwa kazi ulizofanya na kwa jinsi ulivyohishi na watu hapa duniani Mungu ndiye anayejua akuweke nafasi gani huko mbinguni: Poleni sana wanafamilia jamani kwa kuondokewa na kipenzi chenu.
 
Mungu amlaze mahali pema, poleni sana wafiwa

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Aliugua nini?isije ikawa homa ya M4C Awekwe anapostahili.amen
 
pressure za m4c pole dada ila umefia kwenye ufisadi haya bana kalazwe pema ufisadin amene!
 
Angekufa rejia mtema apo kila mtu angejifanya ana uchungu sana.chadema acheni ujinga kwenye mambo ya msingi yanayohitaji kuonyesha utaifa.kwa mtindio huu wa ubongo ndio mpewe nchi,mtasubiri sana.comment zenu hapa ni za kitoto mno.
 
Angekufa rejia mtema apo kila mtu angejifanya ana uchungu sana.chadema acheni ujinga kwenye mambo ya msingi yanayohitaji kuonyesha utaifa.kwa mtindio huu wa ubongo ndio mpewe nchi,mtasubiri sana.comment zenu hapa ni za kitoto mno.

Nawe pia umeingia kwenye mkumbo wa unaowaponda,! Pumzika Mama Kipangula
 
pressure za m4c pole dada ila umefia kwenye ufisadi haya bana kalazwe pema ufisadin amene!

Kwa hili umekosea sana,
Geuza upande wa pili wa shillingi, uwe unasikia maneno ya dhihaka chuki na shutuma kama hayo yakitolewa kwa ndugu yako aliyetangulia mbele za haki.
Tambua utu wako ndugu maana wahenga walisema ada ya mja hunena ungwana ni kitendo.
 
Inapokua kifo, wote bila kujali vyama tunakaa kimya. Hakuna profesor alietuambia kweli na tukahakikisha "life after death" . Bado ni giza nene! !. Hapa tuache siasa, R.I.P madam.
 
Back
Top Bottom