Morogoro: Fire na Uokoaji hii Fedheha kwa Wizara Yenu

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,895
33,320
Inasikitisha sana kuwa na Askari wanaolipwa mishahara, wamenunuliwa vitendeakazi, wamepewa magari mazuri na serikali lakini wapowapo tu hawafanyi kazi yao. Kuna matukio mawili yanafanana ambayo kikosi hicho kimeshindwa kabisa kuyatendea haki.
  1. Mwaka 2022 katika eneo la Kihonda VETA mwanafunzi mmoja wa chuo hicho alitumbukia kwenye maji akazama na kufia humo, Fire walipelekewa taarifa wakafika kwenye eneo la tukio, lakini wakajitetea kuwa hawaruhusiwi kuingia kumtafuta maiti kwenye maji baada ya saa 12 jioni, hivyo waliondoka na kurejea siku ya pili asubuhi, walipofika kama kawaida yao wakaanza kutupiana mpira na hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia kufanya uokoaji, vijana wa mtaani hapo wakajitosa na kufanikiwa kuibuka na mwili wa mwanafunzi huyo aliyekwenda kuzikwa kwao Moshi.
  2. Jana tarehe 1.3.2024, kijana mwingine aliyekuwa anafua kandokando ya mto Ngerengere aliteleza na kuzama majini karibu na daraja la mwendokasi Tungi Morogoro, kama kawaida Fire wakapigiwa simu wakafika majira ya saa 9 alasiri, lakini hawakuweza kufanya chochote zaidi ya kuvaa na kuvua life jackets zao na kuzunguka huku na kule wakiongea na simu, walipoulizwa mbona hawafanyi chochote wakasema wanataka kufunga mashine wavute maji yapungue, ndipo kijana yuleyule aliyeopoa mwili wa mwanachuo wa Veta mwaka 2022 akaamua kuzama mara kadhaa na kufanikiwa kutoka na mwili wa mhanga huyo.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kitendo cha askari hao kuwapigia simu wakubwa wao kuwaarifu kuwa wao ndiyo wamefanikisha zoezi hilo, tabia za namna hii ndiyo zinashusha ari ya vijana wanaojitolea kusaidia kikosi hicho, ifahamike wazi kuwa kijana huyo hakulipwa hata senti, wao kama waajiriwa wa serikali wanalipwa mshahara kila mwezi lakini hawafanyi kazi yao, siyo uungwana kujisifu kwa kazi walizosumbukia watu wengine. Wito kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, utambue kwamba una wafanyakazi wanaolipwa kwa jasho la watu wengine.
 
duuh hao jamaa ni washenzi kabsa yaani aisee ilibidi wanachi wawafukuze kwa kuwarushia mawe ili ujumbe uwafikie viongozi wao
 
Tanzania Ina Majeshi Mengi Sana Ila Fire Na Uhamiaji Siyo Kama Walivyoyapa Hadhi Hiyo
 
Wito kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, utambue kwamba una wafanyakazi wanaolipwa kwa jasho la watu wengine.
Hawajui kuzamia hao sasa ulitaka na wao wafe? Hao wameenda tu darasani wakafaulu mtihani wa darasani Ila practical za kuzamia Majini Sifuri, huyo jamaa mzamiaji apewe kazi huko Jeshi la zimamoto tatizo ndio hilo Serekali Ina rasilimali watu kibao km hizo kibao zinaishia tu kushinda vijiweni kuvuta bangi na ugoro kisha zinaelekea kwenye mabanda ya kubet, hio rasilimali itakufa masikini kisa eti haijaenda Shule ya Zimamoto lakini Ina kipaji cha kuzamia

Serikali iwaangalie vijana km hao sio inawaacha tu mtaani wanazagaazagaa tu,
 
unazungumzia fire ya morogoro ambayo ilishuhudia mzee akiteketea kwa moto ndani ya nyumba iliyokuwa inawaka moto mbele ya ofisi zao makao makuu ya zima moto morogoro?
 
Ssahihi kabissa
 
unazungumzia fire ya morogoro ambayo ilishuhudia mzee akiteketea kwa moto ndani ya nyumba iliyokuwa inawaka moto mbele ya ofisi zao makao makuu ya zima moto morogoro?
Sijui serikali imesinzia usingizi wa namna gani haiyaoni hayo yote
 
Tanzania Ina Majeshi Mengi Sana Ila Fire Na Uhamiaji Siyo Kama Walivyoyapa Hadhi Hiyo
Wamejaa wahuni watupu, kazi yao kula rushwa za ukaguzi wa mitungi hamna kitu pale
 
duuh hao jamaa ni washenzi kabsa yaani aisee ilibidi wanachi wawafukuze kwa kuwarushia mawe ili ujumbe uwafikie viongozi wao
Viongozi wao nao mfu kabisa, ati wanawapongeza kwa kazi nzuri ya kutimiza agizo la Mh. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan la kuwataka kuwatumikia wananchi wakati hawakugusa chochote
 
Pale geita huwa wanapigiwa simu daily ili kuwasalimia na kuwauliza kama maji wanayo na maandalizi yapo.sio wajinga maana wanalijua hili jeshi linawapiga dili tu
 
Back
Top Bottom