MOROGORO: Bondia Francis Cheka ashikiliwa na Polisi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,432
2,000
64f912b11272150c5e008e36ba768909.jpg

Bondia Francis Cheka ashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 28

Bondia huyo ambaye yuko rumande kwa sasa, anakabiliwa na kosa la kukataa kupanda ulingoni Desemba 25 dhidi ya Bondia Abdallah Pazi (Dulla Mbabe)

Kwa mujibu wa Promota wake, Kaiki Siraji, akifungua kesi katika Kituo cha polisi cha Kawe kwakuwa Cheka alimbadilikia dakika za mwisho wakati walikuwa na makubaliano kimkataba ulio kwa mujibu wa sheria za ngumi

Hata hivyo, Bondia Cheka atapelekwa Dar es salaam kesho akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kesi hiyo katika kituo cha Kawe ambako kesi ilifunguliwa Desemba 25.

Chanzo: Mtanzania
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
12,105
2,000
Duu Hawa watu hawana washauri wanajiendea tu,Akipashwa kuwa na "Cheka Team" ambayo humo Kuna wataalam wote,Hawa ndo wangemshauri kisheria katika mambo yote ya mkataba,kule India ukiangalia Iile pambano,unaona kabisa aliuza mechi!,mabondia wetu kutokana na njaa wajanja huwatumia kwa kupandisha rekodi za mabondia wa nje kwa kulipwa kiasi cha mboga kiduchu Ili kukubali kupigwa,..
 

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
1,680
2,000
watageuza mashtaka..itakuwa " kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu"
Hizo fedha hajalipwa. Hilo ni kosa lakuvunja mkataba. Ni kesi ya madai. Bahati mbaya kutokana na kipato na kukomolewa atasumbuliwa tu polisi.
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,432
2,000
Hizo fedha hajalipwa. Hilo ni kosa lakuvunja mkataba. Ni kesi ya madai. Bahati mbaya kutokana na kipato na kukomolewa atasumbuliwa tu polisi.
Kwa mujibu wa Promota Siraji ni kuwa alipewa pesa za mwanzo, ambapo zingine angemaliziwa kabla ya kupanda ulingoni kama inavyokuwa wameahidiana ambapo Cheka alionyesha kutokuwa na imani na mpango huo
 

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,658
2,000
Kwa mujibu wa Promota Siraji ni kuwa alipewa pesa za mwanzo, ambapo zingine angemaliziwa kabla ya kupanda ulingoni kama inavyokuwa wameahidiana ambapo Cheka alionyesha kutokuwa na imani na mpango huo
Kutokuwa na imani wakat kishasaini mkataba na sehem ya hela kachukua.

Subiri aisome namba
 

Joh Daisy

Senior Member
Jul 4, 2016
112
225
Hopeful haki itatendeka hawa mabondia huwa wanadhurumiwa sana aisee so pengine aliamua kujitoa muanga ili aweze kukwepa kudhurumiwa
 

cyrustheruler

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
2,048
2,000
Utapeli mwingine ni kule india pamoja na janja yake ya kukataa kupigana alivuna mamilioni
Huyu ni tapeli mzoefu sasa
 

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,432
2,000
Kutokuwa na imani wakat kishasaini mkataba na sehem ya hela kachukua.

Subiri aisome namba
Mkuu..alisema kuwa aliwahi kucheza pambano na Mthailand ambapo Promota Siraji hakumalizia hela yake mpaka leo ndo maana alikosa imani naye

Kiufupi wanajuana watayamaliza tu ila wanawavuruga mashabiki..!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom