MOROGORO: Bondia Francis Cheka ashikiliwa na Polisi

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,660
2,000
Mkuu..alisema kuwa aliwahi kucheza pambano na Mthailand ambapo Promota Siraji hakumalizia hela yake mpaka leo ndo maana alikosa imani naye

Kiufupi wanajuana watayamaliza tu ili wanawavuruga mashabiki..!
Kwann alikubali kufanya nae kazi tena?!

Asingessini mkataba
 

chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,394
2,000
64f912b11272150c5e008e36ba768909.jpg

Bondia Francis Cheka ashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 28

Bondia huyo ambaye yuko rumande kwa sasa, anakabiliwa na kosa la kukataa kupanda ulingoni Desemba 25 dhidi ya Bondia Abdallah Pazi (Dulla Mbabe)

Kwa mujibu wa Promota wake, Kaiki Siraji, akifungua kesi katika Kituo cha polisi cha Kawe kwakuwa Cheka alimbadilikia dakika za mwisho wakati walikuwa na makubaliano kimkataba ulio kwa mujibu wa sheria za ngumi

Hata hivyo, Bondia Cheka atapelekwa Dar es salaam kesho akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kesi hiyo katika kituo cha Kawe ambako kesi ilifunguliwa Desemba 25.

Chanzo: Mtanzania
Breach of contract na polisi wapi na wapi...

Hawa polisi wa Tz kuna tatizo kubwa sana mahali...
 

CHAZA

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
7,937
2,000
Wanachofanya wanabadilisha kesi. Inakua kujipatia hela kwa njia ya udanganyifu. Ukinyoosha mkono hata mdaiwa anafungwa. Only tz
Lakini mwisho wa siku hiyo ni contractual, ambapo upande mmoja umeshindwa ku comply na terms na hivyo mwisho wa siku atapaswa kulipa na riba, only kama akipata watetez wazuri watapangua hoja ya kujipatia pesa kwa udanganyifu.
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,366
2,000
Lakini mwisho wa siku hiyo ni contractual, ambapo upande mmoja umeshindwa ku comply na terms na hivyo mwisho wa siku atapaswa kulipa na riba, only kama akipata watetez wazuri watapangua hoja ya kujipatia pesa kwa udanganyifu.

Hivi tunaongelea dunia ya kwanza au ''huku kwetu?''

Mpaka hilo la kukamatwa na polisi tu tayari ni taa nyekundu
 

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
1,682
2,000
Kwa mujibu wa Promota Siraji ni kuwa alipewa pesa za mwanzo, ambapo zingine angemaliziwa kabla ya kupanda ulingoni kama inavyokuwa wameahidiana ambapo Cheka alionyesha kutokuwa na imani na mpango huo
Bado hiyo sio sababu ya kumpeleka polisi. Angemfungulia kesi ya madai. Cheka anachohitaji ni Mwanasheria tu. Tena akipelekwa mahakamani anaweza kushinda na aliyemshtaki akapoteza kila kitu.
 

Pota

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
1,985
2,000
Mbona yeye anadai huyo promota wake kuna hela hajamlipa mpaka kesho?
Yaani kuna pambano alishacheza...akapewa advance tu...but baada ya pambano hakumaliziwa...hivo juzi alitska alipwe mpunga wote ndo apande ulingoni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom