MOROGORO: Ajali yatokea, mabasi mawili na lori la mafuta yagongana

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
1,232
1,192
Abood.jpg
BM.jpg

Ajali ya magari iliyotokea asubuhi ya leo sa 06:46 asubuhi hii maeneo ya Maseyi Morogoro iliyosababisha mabasi mawili na lori la mafuta, Mabasi yote yakielekea upande wa mashariki kama sitakosea Dar es salam. Na lory likiwa linaelekea upande wa Morogoro.

MABASI yaliyopata ajali hiyo ni basi la kampuni ya ABOOD na basi la kampuni ya BM COACH na lori ambapo mabasi haya yalitupita sisi tukiwa kwenye basi la SARATOGA tukitoka Kigoma kwa speed sana yakifukuzana ambapo basi la ABOOD likiwa mbele na basi la kampuni ya BM likifuata hapo nyuma .

Tulipofika mbele tulikuta basi la BM likiwa limepinduka, ambapo watu wote wamenusurika japo kuna majeruhi na kondakta kalaliwa na basi miguu na basi la Abood likiwa limeisha na kuharibika vibaya upande wa nyuma na mbele kwa dereva na baadhi ya majeruhi ,pamoja na lori kuvunjika kiasi kioo cha mbele.

MASHUHUDA: Basi la Abood ndo lililoanza kugongana na lori wakati aki overtake basi la BM ambapo basi lilimshinda nakuingia Ngorongoni dereva wa BM nakupinduka, nikiwa mmoja wawaokoaji sikuweza kupiga picha ila zitakuja maana huwa sina tabia ya kupiga picha ajali kabla ya kuokoa watu kwanza mpka naondoka eneo la tukio kuendelea na safari yangu tumeacha kondakta wa BM bado amebanwa chini ya basi upande wakushoto wa dereva.

Jambo la kumshukuru Mungu lori lile halikuweza kupasuka tank sababu kama lingepasuka tungekuwa tunaongea mengine kwasababu lilikuwa na mzigo wa mafuta kusafirishwa kuwelekea nchi za jirani.
 
Aise. Abiria ni haki ya kumkemea dereva unapoona anaendesha gari ndivyo sivyo.
"Mtu wa kulinda maisha yako ni ww na wala siyo polisi''
Kuna watu wanafurahia mwendo kasi. Mimi nikipanda bus namwambia dereva punguza mwendo ama la nakushtaki kwa traffic. Sipendi na nachukia mwendo kasi barabarani wananionaga muoga rafiki zangu ila kinga ni bora kuliko tiba
 
Sasa kama unalala hizo picha zitakuja lini?..eti yule kijana Nondo nae ni mtu wa kigoma?
Sijapiga picha mkuu mimi nilikuwa muokoaji huwa sinaga tabia ya kupiga picha kwenye ajali wakati wenzangu wanaumia huko chini nilichofanya nilipanda juu kuanza kuokoa watu, watu wengi wamepiga picha utaniona tu nanajua zitakuja muda si mrefu ni vile pia dereva wetu aliwahi kuondoka. Mimi nilikuwa kikazi kigoma kwahyo sifahamu kama Nondo ni wauko mkuu nisamehe bure.
 
Pole na safari.
Pole pia kwa majeruhi. Ni matumaini yangu kuwa hamna vifo....
Asante mkuu ,hamna vifo ila wale wale wanao mtia moyo yule kondakta aliyebanwa pale chini wanatakiwa wawe namaneno mazuri maana wanaweza muuwa kwa maneno wakafanya akapata presha na wale wanaopiga picha badala wafanye namna yakumuokoa kuvuta gari ili atolewe
 
Kuna watu wanafurahia mwendo kasi. Mimi nikipanda bus namwambia dereva punguza mwendo ama la nakushtaki kwa traffic. Sipendi na nachukia mwendo kasi barabarani wananionaga muoga rafiki zangu ila kinga ni bora kuliko tiba
Kinga kwenye speed tu sio vitu vingine
 
Aise. Abiria ni haki ya kumkemea dereva unapoona anaendesha gari ndivyo sivyo.
"Mtu wa kulinda maisha yako ni ww na wala siyo polisi''
Kweli kabisa ila walitupita kwa speed sana na asubuhi siunajua kale kaukungu uoni mbele vizuri, na tumewaacha stand.
 
Back
Top Bottom