MORE PRESSURE: CDM Wasiposhinda Arumeru East Uongozi mzima wa Taifa LAZIMA Ujiuzulu

MMK sikubaliani na hoja ya uongozi mzima wa juu kujiuzulu kwa sababu huwezi kumhukumu mtu bila kuangalia historia na kufanya tathmini. Je kabla walikuwa na mtaji wa watu wangapi? Na sasa idadi hiyo imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani? Na kwa nini? Ndipo utaweza kufanya maamuzi sahihi. Kama walikuwa na watu 10 na sasa ni 11 hapo kazi imefanyika na kama watapungua watueleze tatizo ni nini na itafutiwe suluhu.
 
Good article ever nimeisoma nimeilewa lakini najua kwakuwa umeyasema wewe basi yatakuwa changamoto kwa chama lakini yangesemwa na mwingine ingeonekana ni pumba especial ulipogusia ikiwa chama kikishindwa basi uongozi ujiuzulu!

Jambo jingine umenifurahisha sana uliposema
Wengi ambao tuliunga mkono na wale ambao ni mashabiki wa CDM tulitarajia kwa CDM kufanya vizuri zaidi

Nadhani ifike wakati waandishi wengine wa makala mbalimbali za siasa wafunguke ilitunapowasoma tujue rangi zao jambo ambalo litasaidia kupata maudhui ya nasaha za mwandishi.

nakutakia kila la kheri na ujumbe wangu kwako ni kuwa chama hujengwa na wanachama na kunawakati mwingine kwenye kujenga inakubidi ubomoe.
 
MM Demokrasia katika nchi zetu hizi za dunia ya tatu bado sana na kusema usishiriki uchaguzi bado itakuwa sio dawa, na ukishiriki ukashidwa bado sio kigezo cha kujiuzulu, maanda MM ujue hata haya leo tunayaona ni matokeo ya ushiriki usiokuwa na kikomo wa CDM katika chaguzi hizo ndogo.

Zaidi ya hayo yote Majimbo hayo 23 waliyoyapata katika uchaguzi mkuu 2010 ni matokea ya kutokata tamaa, na hata kama ikitokea wameshindwa Arumeru Mashariki bado watakuwa kunakitu wamekijenga katika chama.

Pia tuwape pongezi kwa kitendo chao cha kutokata tamaa kwa muda wote huo katika mizizi ya fitna za kila aina toka kwa watawala.

umemaliza all of my opinion against mwanakijiji,chadema inayo lead sasa ni matokeo ya ubishi wa viongozi kushiriki ktk matukio bila kujali system mbovu iliopo..kwanza makofi kwao tafadhali.ila kuna mazuri ya kuokota kwako
 
akili yako ni mbovu umeangalia upande mmoja tu lakini kwa mtazamo wangu ni viongozi bora hawa waliopo huwezi kupima mtu kwa kuangalia kitu kimoja tu eti ushindi wa ubunge wakati hatuna tume huru na wewe unajuwa lakini je umetizama cdm ilikuwa wapi na sasa ipo wapi. Tumia akili usitumie ujanja, umeme hakuna toka jana mchana
 
Ukiendaa kucheza mpira ukichezewa rafu ukaja kushindwa husingizii nilichezewa rafu, vaa shin guard. Hayo malalamiko unayoyasema tunayasikia hata CCM wanalalamika. Mwisho wa siku, umelambwa magoli.

Sasa wewe unasema nini kuhusu Josephine kuwa kinara makao makuu mpaka "software za mahesabu" kuweka yeye? walinzi wa kanisa lake kulipiwa na chama, posho ya hausigeli wake kuliko yako. Halafu anadanganya umma kuwa mkewe, hata akiwa mkewe ndyo yafikie hayo? hapo hajaolewa bado, akiolewa?

Duh yamekuwa hayo tena? hili swala si linaongelewa kuleee hapa nadhani Mwanakijiji anazungumzia suala la uchaguzi mdogo wa Arumeru na jinsi ya timu ya cdm ilivyojipanga! Nadhani ifike wakati tuwe aligned na maudhui ya mada ili kuweza kuleta hoja za msingi unachokifanya wewe ni kutoka kwenye mstari ili watu waiyumbishe mada. Ni kweli uakubaliana na Mwanakijiji kuwa rato ya chaguzi ndogo ni 1:7 ? na je kipi kifanywe ili hiyo ratio iwe na uwiano. Hebu ifike wakati hizi chuki ziwekwe pembeni tujadili hoja zinazoletwa barazani.
 
Uchambuzi wako umejikita upande mmoja tu. Umezungumzia weakness za viongozi pekee bila kuangalia na success zao!. Hivi ni kweli weakness zao ni kubwa zaidi kuliko success zao?
 
Kuna faida nyingi sana unapokuwa na chama cha upinzani ambacho ni imara.
1. Chama tawala na serikali yake vinaacha kuwa legelege.
2. Maslahi ya inchi yanalindwa na serikali iliyoko madarakani kwa kuogopa kuumbuliwa na chama cha upinazi.
3. Demokrasia inakuwa kwa maslahi ya inchi.
4.Ufisadi unapungua mpaka kwenye mabaraza ya halmashauri kwani hayaundwi na chama kimoja.
5. Wanainchi wanaonyesha jinsi wanavyokipenda chama tawala au kukichukia kwa kuangalia mwitikio wao kwenye mikutano yao hata kama hawastahili kupiga kura.
Ni vyema tukaridhika na uwepo wa viongozi hawa wa upinzani kwani wanafanya chama Tawala kisilale na manufaa yao ni makubwa sana kitaifa. Grear thinker hatakiwi kuwahukumu watu.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna namna moja tu ya kumfanya Nassari kuwa Mbunge – kupiga kura! Siyo kuzomea, siyo kulumbana, siyo kulipiza kisasi, siyo kukashifu wengine – kupiga kura. Kashfa haipigi kura, kuzomea hakupigi kura na malumbano hayapigi kura. Chama ambacho kitahamasisha mashabiki wake kupiga kura kwa wingi ndicho kitakachoshinda. Ngoja niwape mahesabu ya haraka haraka:
Mgombea wa CCM mwaka 2010 marehemu Jeremiah Sumari alipata kura 34,661 wakati mgombea wa CDM ambaye anagombea sasa Joshua Nassari alipata kura 19,123. Tofauti kati yao ni kura 15,538.


Kwa kweli hapa CCM bado wana mtaji mkubwa tu, kazi kwenu CHADEMA kuendelea kujipanga na kutafuta mbinu na mikakati ya kuendelea kuwashawishi watu kuwapigia kura, ni miezi kumi na sita (16) imepita toka uchaguzi mkuu umepita kwa hiyo tofauti ya kura elfu kumi na tano sio mchezo hata kama kuna wana CCM wameasi hawazidi hiyo idadi... hata kama watakua wamezidi tukumbuke CCM wana mbinu chafu za kununua shahada za kupigia kadi, tusijipe moyo wana CHADEMA bado ngoma ngumu
 
Mkuu MM,

Kwa nini hoja yako imejikita kwenye performance ya CDM kwenye chaguzi ndogo tu? Naona hapa kuna udhaifu mkubwa...unapima vipi udhaifu wa chama kwa kushindwa kwenye uchaguzi mdogo na sio kwenye chaguzi zote kwa ujumla pamoja na uchaguzi mkuu? Weka analysis ya chama katika chaguzi kuu toka 1995 mpaka sasa na uweke analysis ya chaguzi ndogo ndio uweze kutoa hitimisho lako. Sidhani kama ni kuwatendea haki CDM kwa kuwahukumu kwa kufanya vibaya kwenye chaguzi ndogo wakati ni hao hao wamefanya vema ktk uchaguzi mkuu!!
 
Ni kweli ushindi unapatikana kwa kutumia mikakati ilyopangwa kimkakati. Ushauri wa MK una asilimia kubwa ya mambo ya kufanyia kazi ili kulichukua jimbo la Arumeru Mashariki.

Ndugu hebu isome vizuri hii post yake, Arumeru mashariki ndo imeshatoka wameshachemka, anaongelea future, we mbona upo nyuma kiiivyo?
 
Huo ujumbe tayari unaeleweka tunataka ushindi - nothing but victory. Kama watu wanataka kutuma ujumbe kwa magamba wanaweza kuwaandikia barua ndefu ya kuwakataa.

Mwanakijiji, samahani, nahisi mwangwi wa dhana ya ushindi ni lazima kwenye posts zako. am I wrong?
 
bahati mbaya sana siasa si soka. Soka inachezwa dakika, hardly, 90 tena mbele ya macho ya watu. Siasa ni jambo la siri na linalochukua uwanja mpana sana. Mfumo wa soka na mfumo wa siasa ni vitu viwili tofauti. Unaweza kuweka 4-4-2, n.k kwenye soka na ukiona mambo hayaendi unabadili tena mfumo. Mfumo wa siasa ni zaidi ya 4-4-2. Tatizo ni mfumo wa KURA! Hata uwalete kina Slaa 10 na Mbowe kadhaa bado watashindwa tu ikiwa michezo michafu inafanyika na malalamiko yanapelekwa na vyombo vya dola vinachangia kuhujumu. Shahidi zipo. CDM wakisema waende kwa wananchi kushitaki dola inaingia kati, wananchi wanapatwa na hofu, taratibu zinavurugika tena. Ni rahisi kukaa na kuandika na kulaumu. Pamoja na hayo ni changamoto nzuri
 
Unapoenda na timu au uongozi wa timu ambao unaenda kwenye mechi 8 za kimataifa na katika hizo zote timu inafungwa kuendelea na kocha
kwani hizi ni chaguzi za kimataifa? hahahahahaaaa....

halafu si umesema wameshinda mechi moja, kwa hiyo hawajashindwa zote nane,au?

nikishafika hapo tu naona hauko makini na unachotuandikia, nashindwa kuendelea
 
la kujiuzulu halina nafasi hapa kwa kuwa bodo tuna mkoloni ccm anafanya anavyotaka ukibishi jela, misukosuko hadi kifo
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Rekodi ya uongozi wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
linapokuja suala la uchaguzi mdogo ni rekodi mbaya na ambayo ingetosha kabisa kusababisha uongozi huo kujiuzulu mapema zaidi.

Niandikie:
mwanakijiji@jamiiforums.com

Kaka MMM hapo penye rangi ya red pana shida ktk hukumu yako.

Hata wewe umeshaona ni suala la chaguzi ndogo viongozi wana record mbaya. Je MMM unaweza geukia upande mwingine wa record nzuri za viongozi hao? Je una mifano mingine ya record nzuri na mbaya za viongozi hawa ili tuwahukumu kwa haki? Je ukipima record mbaya zao (hasa ya chaguzi ndogo) na record nzuri zao ktk kuongoza cdm changa na kwa muda mfupi ukizingatia viongozi wengine pale bado ni vijana sana, zikiwekwa kwenye minzani zipi zitazidi uzito. Je hadi sasa una la kuendelea kutoa hukumu hiyo au umeghairi hukumu yako?

Siwatetei kuwa hawana record mbaya la hasha ila shida yangu ni hiyo hukumu kubwa mno kwa chama kinachojengwa kama cdm. Hukumu kama hii inawastahili ccm na serikali yake maana ni chama kikongwe, kinarasilmali zote, vyombo vyote vya dola, sheira, jamii, fursa nyingi, n.k Viongozi wao wakishindwa kutuletea tunayotarajia hao lazima wajiuzuru tuu.

Ila tutoe ushauri wetu kwa viongozi wa cdm kurekebisha mammbo wakikataa tuwatose kwa hatua
 
MMJ,kitu kimoja kilichodhahiri ni kwamba,imejionyesha ktk chaguzi zote ndogo,chama kilichokuwa kinaongoza kinatetea kiti chake!hata hiyo mara moja waliyoshinda chadema jimbo lilikuwa lao wakatetea!kuna siri kubwa hapo!na kwa vile arumeru ilikuwa ya ccm naona ni kuwaonea tu viongozi wa juu kutaka wajiuzulu!ingelikuwa ni kupoteza jimbo labda ningekuunga mkono!
 
Back
Top Bottom