MORE PRESSURE: CDM Wasiposhinda Arumeru East Uongozi mzima wa Taifa LAZIMA Ujiuzulu

We all face obstacles in pursuing our goals, whether they’re professional or personal.

We think we’re on the right track but realize we’ve chosen the wrong approach. We’re enthusiastic and hard-working, but our support system disintegrates when we need them the most. We’re just about to make significant progress when we run out of time or funding


before we complain we have to ask our selves how did we help.
 
2. VIONGOZI WOTE WA CDM NI WABUNGE
- Mfumo wa kuajiri makatibu wa CCM ni wakuigwa.Mtu akiwa na shida na chama anajua wapi pa kukipata. hata ile dhana ya wao kuwajibika kiutendaji mpaka wanaweza kuhamishwa vituo vya kazi kulingana na uhitaji ina maana katika kujenga chama. Leo viongozi wote wa CDM watagawa vipi majukumu ya chama na jimbo? kwa nini asiwepo mtu anayewajibika kwa shughuli za kilasiku za chama tu?
Sio sahihi sana kufananisha CCM na CDM hata kwa umri wa uzoefu na kazi, cha kukumbuka ni kwamba hata Mbuyu ulianza kama Mchicha!
 
mkuu hii ni kweli kama refa kila siku anawaumiza lazima siku nyingine mgomee mechi kupinga kuonewa hata kama mnafurahia mapato ya mlangoni..naami mpaka dakika hii ukiwauliza viongozi wa chadema kwamba je wanaimani na nec watajikubu hatuna imani..naweza kuamin kwamba chadema wanashiriki uchaguzi kuongeza fedha ya ruzuku tu.!!
 

CHADEMA HAIWEZI KUSHINDA ARUMERU MASHARIKI!
Mimi ni mwanachama hai wa CDM ninayekubali kukosoa na kukosolewa na kutafuta suluhisho la kudumu. Mimi nipo tofauti sana na wale ambao wanaipenda CDM mpaka hawataki kusikiliza changamoto maana ukileta tu changamoto wewe ni CCM! MZEE M.M mimi nakukubali sana na nakubaliana na analysis yako. Hizi ndizo sababu zangu kwa nini CDM haitashinda Arumeru:
1. ARUMERU KUNA VIJIJI VINGI SANA
Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba Ngome ya CDM ni kusini mwa barabara ya Moshi - Arusha ambako kuna mchanganyiko wa makabila. Lakini kwa Kaskazini huko ni CCM tu. CDM haijawahi kujiimarisha vijijini. Na kwa tanzania vijijini ambako hawana umeme, maji na chakula cha kutosha hawajawahi kuona faida ya kuiacha CCM. Je? haya mahaba ya CCM na wakazi wa vijijini (ambao ndio wengi nchini) yanaletwa na nini? Utagundua kumbe vijiji vingi havina wawakilishi.naomba muwaulize washabiki wengi wa CDM kama wanajua ofisi zao za mkoa na wilaya zilipo!

2. VIONGOZI WOTE WA CDM NI WABUNGE
- Mfumo wa kuajiri makatibu wa CCM ni wakuigwa.Mtu akiwa na shida na chama anajua wapi pa kukipata. hata ile dhana ya wao kuwajibika kiutendaji mpaka wanaweza kuhamishwa vituo vya kazi kulingana na uhitaji ina maana katika kujenga chama. Leo viongozi wote wa CDM watagawa vipi majukumu ya chama na jimbo? kwa nini asiwepo mtu anayewajibika kwa shughuli za kilasiku za chama tu?

3. HAKUNA MTANDAO
hebu fikiria wilaya ya Kondoa (km 160 tu kutoka dodoma!) haina mtandao wa CDM! hebu jiulize kuna vijiji vingapi vikubwa! sasa leo Arumeru kuna vijiji vingapi? CCM wanamtandao hadi wa nyumba kumi lakini CDM hatuna hata wa nyumba 100! CCM wanashinda kwa sababu ufisadi wao wanaueneza mpaka level ya familia wakati sisi wema wetu tuashindwa kuueneza hadi level ya kata!
TUNAWEZA KUSHINDA ARUMERU MASHARIKI LAKINI NI KAMA MUNGU WA MBINGUNI ATARIDHIA TUSHINDE LAKINI KWA SASA MATUMAINI HAKUNA!

Lakini kwani kwako wewe CCM ndiyo chama pekee? Hujui kuwa nguvu waliyonayo CCM inatokana na urithi wa mali tulizowachangia sisi wananchi wakati wa mfumo wa chama kimoja? Hilo la mtandao wa CCM kwa sehemu kubwa ya nchi kwa sasa ni nadharia kuliko uhalisia.
 
Magwanda na washabiki wao wanapoanza kujitetea.

Dahh, kumbe mmechapwa katika chaguzi ndogo 7. Halafu mna hamu ya kushinda tena? kwanza safisheni nyumba yenu kabla hamjaingia mitaani.

Jibuni maswali rahisi sana yanakiumiza chama chenu, hapo hapo makao makuu yenu. Leo mpaka kashfa za hawara kulipwa posho na hausigeli kulipwa posho na walinzi wa kanisa analokwenda hawara kulipwa na chadema. Mpaka kufikia hawara kuweka mtandao wa mahesabu ya chadema, nyie bado mnalalamika kuhusu Arumeru?

Hivi kinawashinda nini kuona uozo ulioko nyumbani kwenu? Ikiwa haya madogo ya nyumbani kwenu, makao makuu yenu yanawashinda, mtaweza kweli kwenda kutatua ya wananchi wa Arumeru? Walioyaleta humu JF ni watoto zenu wenyewe waliopo ndani, jikoni. Lakini mnawabeza na kuwafanya majuha. Inasikitisha sana.

Mambo mengine yanashangaza sana. Hivi hamsomi kinachoandikwa?
 
mkuu hii ni kweli kama refa kila siku anawaumiza lazima siku nyingine mgomee mechi kupinga kuonewa hata kama mnafurahia mapato ya mlangoni..naami mpaka dakika hii ukiwauliza viongozi wa chadema kwamba je wanaimani na nec watajikubu hatuna imani..naweza kuamin kwamba chadema wanashiriki uchaguzi kuongeza fedha ya ruzuku tu.!!

Kwa macho yako ya Ki-CCM lazima uone hivyo. uchaguzi usipokuwa na vyama vingine vinavyoshiriki utakuwa ni uchaguzi au uteuzi?
 
Nazungumzia kwenye hili suala la vitambulisho vya kupiga kura.

Ni kweli usiopingika kwa CHADEMA kuhakikisha wanao wapiga kura hapo jimboni na sio mashabiki ambao mwisho wa siku ni wale waliokwisha uza hivyo vitambulisho vyao, lakini pia wahakikishe wanakuwa na wahamasishaji makini siku ya kwenda kuchagua maana siku hiyo kuna njama nyingi mojawapo ni wale wapiga kura pinzani wanaenda mapema halafu wanalaghai wenzao kuwa wasubiri wataenda baadaye wanaanza kunywa pombe huku wao wakiwa wamepiga kura zao.

Jambo jingine kwa kuwa fomu namba 17 haitatumika kwa mujibu wa Mkurugenzi wa NEC, waelimishe watu manufaa ya kutunza vitambulisho vyao bila kumuuzia mtu, na wahamasishe ujasiri kwa wapiga kura wao wajitokeze kuchagua na ushabiki bila kitambulisho ni sawa na kuchota maji kwenye pakacha.

Mawazo ya kujiuzulu uongozi wa CHADEMA kwa kushindwa UCHAGUZI/CHAGUZI ndogo siyo hoja ya msingi maana asiyekubali kushindwa si mshindani na washindanapo wengi huwepo mshindi mmoja.

huwezi kila mara ukawa unaongonza timu kufanya vibaya then ukaendelea kuwa kocha.
 
Lakini kwani kwako wewe CCM ndiyo chama pekee? Hujui kuwa nguvu waliyonayo CCM walirithi mali tulizowachangia wananchi wakati wa mfumo wa chama kimoja? Hilo la mtandao wa CCM kwa sehemu kubwa ya nchi kwa sasa ni nadharia kuliko uhalisia.

Nadharia wakati nimesoma huko juu kuwa wameshawatandika mara 7 katika chaguzi ndogo, mlipojitutumuwa jimbo la Wangwe muda mchache baadae CCM wakalichukuwa tena! Uchaguzi mkuu ndio usiseme hata robo ya wabunge wa CCM hamjaifikia, hata robo ya madiwani wa CCM hamjaifikia. Halafu unasema mtandao ni nadharia? wewe kweli huutaki ukweli.

Sisi wengine tungependa kuona upinzani wote kwa pamoja unachukuwa hadi nusu ya viti vya ubunge na udiwani, hapo ndio tunajuwa sasa Tanzania ina "watch dog". Na kama hamuambiliki, basi msahau kabisa ushindi, mtabaki kulalama daima.
 
huwezi kila mara ukawa unaongonza timu kufanya vibaya then ukaendelea kuwa kocha.

Umenena vyema kabisa, tena madudu ya hao makocha yameanikwa humu, yanaanzia nyumbani. Lakini ni nani wa kumrithi Mbowe (mwana ukoo)? kama alivyorithishwa yeye? hapo sasa!
 
Magwanda na washabiki wao wanapoanza kujitetea.

Dahh, kumbe mmechapwa katika chaguzi ndogo 7. Halafu mna hamu ya kushinda tena? kwanza safisheni nyumba yenu kabla hamjaingia mitaani.

Jibuni maswali rahisi sana yanakiumiza chama chenu, hapo hapo makao makuu yenu. Leo mpaka kashfa za hawara kulipwa posho na hausigeli kulipwa posho na walinzi wa kanisa analokwenda hawara kulipwa na chadema. Mpaka kufikia hawara kuweka mtandao wa mahesabu ya chadema, nyie bado mnalalamika kuhusu Arumeru?

Hivi kinawashinda nini kuona uozo ulioko nyumbani kwenu? Ikiwa haya madogo ya nyumbani kwenu, makao makuu yenu yanawashinda, mtaweza kweli kwenda kutatua ya wananchi wa Arumeru? Walioyaleta humu JF ni watoto zenu wenyewe waliopo ndani, jikoni. Lakini mnawabeza na kuwafanya majuha. Inasikitisha sana.

Mambo mengine yanashangaza sana. Hivi hamsomi kinachoandikwa?

Hee. Hayo ya kashfa za viongozi wa CDM mliombwa kuleta ushahidi, bado wewe unaleta tuhuma na siyo ushahidi. Hizo ni fikra mfu kabisa ambazo zitakusaidia wewe kama mgonjwa aliyepewa dawa ya ganzi ili afanyiwe operesheni. Kutunga uwongo mmeuweza lakini ushahidi umewashinda. Ikakusaidia nini wewe kurudiarudia hilo.
 
Mwanakijiji
Kwanza hongera sana kwa uchambuzi wako wa kina pamoja na muda mwingi wote uliotumia.
Natofautiana na wewe kwenye hoja ya viongozi wa kitaifa kujiuzulu.uchambuzi huu kwa wakati kama huu wa uchaguzi mdogo unaweza ukawa demoralize viongozi wa CDM pamoja na jitihada wanazofanya ili kuweza kushinda huko arumeru.
Kwa wakati huu ningeshauri kama wewe ni mshauri wa CDM basi uendelea kuwashauri ili wafanikiwe kushinda ila sio kwa kuwawekea masharti.Tukumbuke kuwa sio kila wakati tunachopanga kwenye makaratasi/keyboard inakuwa relevant kwenye field of work ukiachilia mbali rafu zinazochezwa na CCM,NEC na ofisi ya msajili wa vyama.
 
Kikubwa CHADEMA wajipange kuhakikisha kipindi cha maboresho ya daftari la wapiga kura watu wengi wanajiandikisha
 
ndugu mwanakijiji kama ulivyosema kuna tatizo ambalo lipo la CDM kuiga CCM katika kampeni. mimi nimekuwa nakerwa na lugha/matamshi ya mtaani "kitaa" ya Joshua Nassari kwenye kampeni mfano kuna siku nilimsikia akisema

"kikataeni hicho chama cha magamba" nadhani huwezi kusema hii kwenye hadhara ya watu wengi na hasa kuonekana kwenye media. na hiyo nyingine ya kwamba "atamwoa Halima " .

Ningemshauri Nassari atumie maneno ya kiswahili fasaha na ajikite kwenye ahadi zitakazotekelezeka, hayo mengine awaachie akina Vicent na wengine. kumbuka kwamba kwa Lugha unaweza kuwavuta/kuwaudhi baadhi ya makundi ya watu hususani unapoongelea vijana/watu wazima/wazee ni vyema kutafuta balance
 
Nadharia wakati nimesoma huko juu kuwa wameshawatandika mara 7 katika chaguzi ndogo, mlipojitutumuwa jimbo la Wangwe muda mchache baadae CCM wakalichukuwa tena! Uchaguzi mkuu ndio usiseme hata robo ya wabunge wa CCM hamjaifikia, hata robo ya madiwani wa CCM hamjaifikia. Halafu unasema mtandao ni nadharia? wewe kweli huutaki ukweli.

Sisi wengine tungependa kuona upinzani wote kwa pamoja unachukuwa hadi nusu ya viti vya ubunge na udiwani, hapo ndio tunajuwa sasa Tanzania ina "watch dog". Na kama hamuambiliki, basi msahau kabisa ushindi, mtabaki kulalama daima.

Huko kwenye suala la uchaguzi hujaona hoja zinazoelezea ununuzi wa vitambulisho vya kura, kutokuboreshwa daftari la wapiga kura na uchakachuaji wa matokeo. labda macho yako yanaona unayopenda kuona?
 
Mkuu, CDM haiwezi kuishia kubeba matumaini ya watu ni lazima iyarejeshe matumaini hayo. Haiwezi kufurahia kushiriki chaguzi hizi bila kushinda, haiwezi kuendelea kufurahia maneno makali dhidi ya serikali - what matters ni ushindi. Hakuna shaka hata kidogo CDM inakubalika na inapendwa lakini ikumbukwe inakubalika na kupendwa siyo kwa sababu imeshinda bali kwa sababu ina ujumbe unaokubaliika. Well, its about transforming message into victory. Hapa ndio pamekuwa pagumu sana. Sasa, wapenzi, mashabiki, na wanachama wanatakiwa kuweka hiyo pressure kuwa kwa Arumeru Mashariki hatuwezi tena kuona status quo is maintained.

Watu wasikubali "tumepata kura nyingi" au "tumepata wanachama wengi" hayo yote hayajalishi kama mwisho wa siku mgombea wa CCM ndiye mshindi. HIvi watu wanakumbuka "kura nyingi" za Busanda, Kiteto au Biharamulo? Kwa hiyo ni bora tuwape sisi wenyewe pressure ili wajue kuwa vitu haviwezi kuwa kama vilivyokuwa baada ya chaguzi nyingine ndogo.

Mwanakijiji nisikufiche
nilikuwa nafikiria hili swala ila nadhani nilipungukiwa na ujasiri. Wewe umeweka standard ya juu sana.

Wakishindwa wajiudhuru, Ili tupate viongozi wengine wakutupeleka kwenye next level ya mashtaka yetu.Ni lazima tufikie mwisho, tunakoelekea ni kwenye kuzoea harakati, malalamiko na chaguzi zisizo kwisha, itafikia wakati tutasahau hata tunachokipagania ni nini.

Mwanamke gani huyu asiyezaa. Tusipopata mtoto sasa uondoke.
 
Binafsi mimi nilitaka uongozi wa juu ujiuzulu siku ya j3 mara baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza JK kama rais huku dr Slaa akipinga na kilichokuwa kikisubiliwa ni kutangaza maandamano yasiyo na kikomo! matokeo yake zikaanza kauli za ohhh hivi mara vile,katika hili la Arumeru mashariki kauli zote kinyume na ushindi hazipaswi kupewa nafasi,stori za ohh tumeibiwa lazima tupime majeraha sio unadai tumeibiwa wakati hata kovu huna hii haitakubalika.
 
Mkuu kwanza kabisa nimefurahishwa sana na jinsi ambavyo umekuwa ukichambua mada zako na zaidi ni kuhusisha matukio na takwimu ambazo ki msingi naona kabisa ni mfuatiliaji mzuri katika masuala ya kisiasa na kijamii kwa ujumla. Ki msingi nakubaliana sana na uchambuzi wako kwa mantiki ya kukubalika kwa chama na mbinu chafu ambazo CCM mara zote wamekuwa wakifanya katika chaguzi mbalimbali ili kuwapatia ushindi na hiyo si dhana ya CCM bali ni vyama karibu vyote tawala katika bara la Africa hutumia mbinu chafu kuhakikisha kuwa wanaendelea kutawala hata kama hawakubaliki kwa wananchi. Ni kweli kabisa naona CDM nayo imeanza kujisahau na kutumia mbinu nyingi kama za CCM kitu ambacho hakiihakikishii ushindi bali ni kushindwa. Ni kweli kabisa CDM ni lazima ije na mbinu mbadala ili kiweze kushinda chaguzi na pia iachane kabisa na tathmini ya kuangalia watu mikutanoni au ni wangapi wananyoosha vidole viwili juu na kupata imani ya ushindi kabla hata ya kupiga kura. Tuachane na tathmini ya kuangalia kwenye mikutano ya CCM wana watu wangapi au wameshindwa kufanya mikutano mingapi na kujihakikishia ushindi kabla ya kupiga kura. Uhakika wa namna hii unaifanya CDM kwa namna moja ama ingine kupunguza na mikakati mipya wakati wa kampeni matokeo yake mwisho tunakuja kupigwa butwaa kwa kuona CCM wanatangazwa washindi. Ni lazima CDM ijenge utaratibu wa kufanya utafiti wa kisayansi wa kuweza kutambua ni nani anawaunga mkono na wenye sifa zote za kupiga kura kwa mujibu wa demokrasia kwa maana ya kuwa na kitambulisha cha kupigia kura, uwezo wa kukihifadhi vizuri na spirit ya kwenda kupiga kura kwa kukichagua chama kile kile.

Mwisho nimelizie kwa kusema suala la KUJIUZURU kwa viongozi kwa mujibu wa tathmini ya mtoa mada si sidhani kama ni sahihi hasa kwa kuzingatia vigezo vya utendaji wa viongozi hawa kwa maana ya kukifikishwa chama hapa kilipo kwa kasi ya muda mfupi tu. CDM sasa ni LULU na hakuna mtu asiyependa kuwa CDM sasa aidha kwa kutamka hadharani au kwa kujificha kwa kuhofia kuonekana tofauti kwa watawala. Hakuna asiyejua kwa sasa NGUVU ya CDM ndani ya jamii ambayo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na mipango mizuri ya viongozi hawa. Hata kwenye timu ya mpira kama Barcelona huwezi kuwapumzisha MESSI na FABREGASI kwa sababu rahisi kabisa kama ulizotoa kwa viongozi wa taifa wa CDM. Inawezekana tukaona ni raisi sana kuwa na SLAA, MBOWE, ZITO, MNYIKA, LISU na wengineo katika chama hebu jaribu kutokuwa nao.
 
Thread inapokwa ya hisia binafsi za mtu na si mtazamo wa wapiga kura wenyewe inakuwa haina maana tena. Hivi unategemea MBOWE, SLAA wa-step down kisa eti Wwameshindwa Arumeru Mashariki? watamwambia nini Mzee mtei eti mkwe wake kakosa nini mpaka awajibishwe? Tume ya Uchaguzi pateni somo kutokana na thread hii, ni mbinu gani CDM wanashauriwa kuzitumia ili kujipatia ushindi huko Arumeru Mashariki? wale wasiyo na shahada za kutopigia kura wahakikishe wanakua nazo, wazitoe wapi?


  • Binafsi napuuzia kabisa picha na mikutano ya maelfu kwani kwangu haina maana yoyote ile
  • Lakini walipata majimbo ambayo hata hayakutarajiwa kabisa na kama yalitarajiwa ni kwa sababu ya mgombea maarufu aliyekuwa CCM akajiunga na CDM. CDM ilichukua Ukerewe, Biharamulo Magharibi, Bukombe, Meatu, Mbulu, na Mbozi Magharibi
  • Inakuwaje timu inaenda kucheza na timu ile ile wanafungwa na kila siku wanalalamikia refarii?
  • Leo tumeshuhudia jinsi – katika hali ya kuchanganyikiwa – viongozi wa juu wa CCM wakitumia mbinu za kashfa za kutunga na kushambulia watu badala ya hoja na matokeo yake CDM nao wanaanza kujibu hivyo hivyo;
  • Haijalishi maelfu ya watu wanaotokea, haijalishi watu wanaonyosha vidole viwili na haijalishi maneno ya kujiamini uchaguzi unashindwa kwa mikakati na mbinu! Huwezi kushinda vita kwa mavazi na nyimbo bali kwa mikakati na mbinu. Kama mavazi peke yake yangekuwa yanashinda vita hakuna jeshi lililokuwa linaonekana vizuri kama jeshi la Gaddafi! Fikiria!
  • Kwa haki kabisa huwezi kuzungumzia kupigania haki za wananchi wetu kabla ya uhuru bila kugusia Meru katika ule Mgogoro wa Ardhi Meru. Wameru walitambua kuwa haki zao zilikuwa zimevunjwa na utu wao kudharauliwa. Hawakuwa tayari kupiga magoti mbele ya watawala wa zama hizo. Siyo chini ya tishio la bunduki za Wajerumaini au kutii utawala wa Mwingereza. Walijitahidi kupinga na walipinga kweli kweli.

Sitaki kuendelea na kunukuu maneno mengi sana ila nadhani CHADEMA si chama cha siasa hata kikitetewa vipi na mwisho wake utakuja kuonekana pale ambapo kitaliingiza taifa katika matatizo kama ambavyo vikundi vilijifanya vinatetea haki kule Tunia, Libya na kwingineko, na sasa tunashuhudia wananchi wa nchi hizo wakibaki wanajuta. Lakini pia tumshukuru mungu kwa vile sasa baadhi ya watu wanaanza kutambua kuwa baadhi ya viongozi wa Kikundi hiki (siwezi kukiita chama) kuwa wanatakiwa kupisha ili taifa libaki slama. Watu wameanza kutambua kuwa umaarufu wa kikundi hiki unachangiwa na zile pumba ambazo zinaondolewa CCM ambazo zina tamaa na damu ya wazalendo wa nchi hii.

Watu wanaanza kutambua kuwa wingi wa watu wanaokwenda kuangalia helikopta na kufurahia matusi majukwaani si wote ambao mwisho wa siku watapiga kura.

Watanzania tuendelee kuwaunga mkono watanzania ambao sasa wazinduka na kugundua kuwa CHADEMA si chama cha SIASA bali kikundi ambacho kinalalama siku zote kwa kutaka tu damu ya watanzania utadhani ni majni.

Eti nae huyu ni mbunge wa ccm! yaani unashindwa kukubali kuwa dunia imebadilika na watu wamebadilika kifikra.
kwahiyo unataka kutuambia ccm itawale milele? Hakika nakuambia mtatokwa sana na mapovu lakini ukae ukijua kuwa
siku zenu zinahesabika! no matter today or tomorrow lakini lazima mtang'oka tu. Haki huwa haipotei bali ucheleweshwa
tu na watu kama nyinyi wenye mawazo mgando kama hayo uliyoyatapika hapo juu. Shame on u mbunge wa ccm....
Naheshimu name calling,vinginevyo ningekutaja jina hapa hapa
 
Back
Top Bottom