MORE PRESSURE: CDM Wasiposhinda Arumeru East Uongozi mzima wa Taifa LAZIMA Ujiuzulu

Mwanakijiji madai yako yana msingi sana lakini binafsi yangu nimeona vitu viwili vikubwa ambavyo vinaiangusha CDM katika chaguzi nyingi.

1.0 Wafuasi wake wengi ni vijana ambao walikuwa hawajapata hamasisho la kujiandikisha. Hawa ndiyo wanakiangusha sana chama.

2.0 Tume kuwa biased kabisa. Yaani imekaa kuhakikisha CCM inashinda huku ikijivuna nguvu ya jeshi endapo itavurunda. Na kwa tanzania bado hatujafikia hatua ya kujitoa mhanga kudai haki zetu. Kwa mbali madokta wameonyesha njia.

Hivyo huwezi kukilaimu sana chama, kwa matokeo mabovu.

Mwisho chama bado kina safari ndefu kabla ya kukabidhiwa watu wengine. Bado sina imani sana na baadhi ya watu pale juu naona wamekaa kimamluki lakini.

Kwangu hilo la pili silijali sana kwa sababu tayari liko presumed. Hilo la vijana ni suala la mikakati tu. Kwanini CDM inaenda kushiriki chaguzi abazo inajua ngome yake - vijana - hawana kadi za kupigia kura? Uchaguzi huu unafanyika zaidi ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu kwanini hakukuwa na zoezi la kuandikisha wapiga kura wapya? Well.. "You go to war with the army you got" alisema Rumsfeld.
 
Hata kama wakishindwa,ila kwa Magamba unakuwaga ni ujumbe tosha kuwa hawakubaliki.
Go on go on CDM na crew nzima ya wapenda mabadiliko, Mwanakijiji leo umeteleza na lazima tukwambie, ukibisha basi umetumwa
 
Zaidi ya hayo yote Majimbo hayo 23 waliyoyapata katika uchaguzi mkuu 2010 ni matokea ya kutokata tamaa, na hata kama ikitokea wameshindwa Arumeru Mashariki bado watakuwa kunakitu wamekijenga katika chama.

Hili ndilo nataka tuachane nalo; kama CDM wanataka kukijenga chama waende Mtwara, Lindi, Tabora n.k au mahali ambapo hakuna uchaguzi! WAnapoenda kwenye uchaguzi wanataka kushinda. Timu haiendi uwanjani ili ipate mashabiki wengi; inaenda uwanjani ili ishinde! Njia bora ya kukijenga chama ni kushinda uchaguzi siyo kushiriki uchaguzi!
 
Mkuu, watu wamekubali kwenda kwenye uchaguzi wakijua NEC ni ile ile - basi hiyo inakuwa assumed kwenye equation. Hakuna chochote kilichobadilika kati ya uchaguzi wa Igunda, Uvini na huu wa Arumeru.
Mkuu MMM akili zikizidi sana wakati mwingine hazimsaidii binadamu, nakubaliana na uwezo mkubwa ulionao kama Political analyst mzuri, lakini bandiko lako limejaa vitu vingi vya kufikirika zaidi, kwanza awali ya yote ungeonesha ni chaguzi ipi ndogo ambayo imefanyika na CCM ikashinda ili hali jimbo halikuwa lao?

Pili kama utakumbuka mwaka 2010 ulituambia hapa hapa uchaguzi ule mkuu kwa namna yoyote matokeo yake hayachakachuliki? je walikumbuka hili!? na kama unakumbuka ulichokisema je uchakachuwaji ulikuwepo au lah?

Tatu kama unazungumzia swala la viongozi kuwajibika hebu nipe tathmini yako tangu Mwenyekiti akiwa Edwin Mtei, Bob Makani na sasa hivi Freeman Mbowe je ni uongozi upi ambao umefanikiwa kukijenga chama? kama utakumbuka Mbowe huyu mwaka 2005 alikubali kupoteza Ubunge wa Hai ili akijenge chama chake kwa kusimama ulingoni na Jakaya Kikwete tena wakati huo JK akiwa ni chaguo la Mungu (Ni dhahiri Mbowe aligombea huku akijuwa ni ndoto kumshinda JK) je huyu sio mpiganaji wa kweli?

MMM nadhani unajuwa fika kabisa ni namna gani ilivyokuwa ngumu kuanzisha chama cha siasa na kukifikisha ngazi kama iliyofikia CHADEMA? nadhani wewe binafsi ni shahidi mzuri wa hili maana Mlipoanzisha chama chenu CCJ kilikufa hata kabla hakijapata usajili wa kudumu na Makamanda wenzako waanzilishi ambao uliwaamini wengine wamejisalimisha CCM, je hapa huoni kwamba si kazi rahisi kujenga Chama kama unavyotaka kutuaminisha?

Hitimisho: Nina imani na uongozi wa CHADEMA na nina Imani na CHADEMA kama taasisi, na nionavyo mimi uongozi huu unastahili pongezi kwa kukifikisha chama katika stage hii ingawa changamoto ni nyingi, lakini kusema CHADEMA ni lazima ishinde Arumeru bila kuwa na utafiti wa kisayansi ni kupotoka.

305650_10150602915896156_687191155_9755398_2030581143_n.jpg
 
MMM ,
Umefanya uchambuzi mzuri... la muhimu ni hili jimbo la Arumeru Mashariki, Chadema wanapaswa kushinda katika jimbo hili.
Pamoja na kuulaumu uongozi wa juu kwa kushindwa chaguzi takribani zote ndogo, nafarijika kwamba umeelezea pia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo, nyingine zikiwa nje kabisa ya uwezo wao. Pale wanapoweza kujivuta, tunawasihi wafanye hivyo.
Wakati huo huo, napenda kuupongeza huu uongozi kwa kuweza kuongeza majimbo mwaka 2010.
Hofu yangu kubwa, ni mwaka 2015... maandalizi yanapaswa kuanza mapema, lakini wamejipangaje? Ndio sababu nimesikitishwa sana na jinsi uongozi huu ulivyoshindwa kutekeleza mkakati wake wa kutenga 20% ya ruzuku wanayoipokea kwa ajili ya uchaguzi wa 2015, napata hofu kubwa sana juu ya hili!! 2015 sio mbali hata kidogo
 
Hata kama wakishindwa,ila kwa Magamba unakuwaga ni ujumbe tosha kuwa hawakubaliki.
Go on go on CDM na crew nzima ya wapenda mabadiliko, Mwanakijiji leo umeteleza na lazima tukwambie, ukibisha basi umetumwa

Huo ujumbe tayari unaeleweka tunataka ushindi - nothing but victory. Kama watu wanataka kutuma ujumbe kwa magamba wanaweza kuwaandikia barua ndefu ya kuwakataa.
 
MMM ,
Umefanya uchambuzi mzuri... la muhimu ni hili jimbo la Arumeru Mashariki, Chadema wanapaswa kushinda katika jimbo hili.
Pamoja na kuulaumu uongozi wa juu kwa kushinda chaguzi takribani zote ndogo, nafarijika kwamba umeelezea pia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo, nyingine zikiwa nje kabisa ya uwezo wao. Pale wanapoweza kujivuta, tunawasihi wafanye hivyo.
Wakati huo huo, napenda kuupongeza huu uongozi kwa kuweza kuongeza majimbo mwaka 2010.
Hofu yangu kubwa, ni mwaka 2015... maandalizi yanapaswa kuanza mapema, lakini wamejipangaje? Ndio sababu nimesikitishwa sana na jinsi uongozi huu ulivyoshindwa kutekeleza mkakati wake wa kutenga 20% ya ruzuku wanayoipokea kwa ajili ya uchaguzi wa 2015, napata hofu kubwa sana juu ya hili!! 2015 sio mbali hata kidogo

Kinyume na wengi wanavyochukulia majimbo waliyoyapata 2010 - mengine kwa mbinde sana - ni jambo la kujivunia kwa kiasi tu lakini it was way below mathematical projections kama wangefanya vizuri. CDM wasingepata less than 90 seats..
 
Huu uandishi wa kibongo umekaa kimapenzi sana. Yaani mtu anaonesha kabisa kuwa yeye ni mshabiki wa CHADEMA which thing grossly prostitutes 'journalism ethics'. A serious and committed journalist never alludes his political inclination to his work.
 
Uchambuzi mzuri Mzee Mwanakijiji.
Arumeru chadema tutashinda, ushindi wa chadema Arumeru ni ushindi wa wapenda mabadiliko nchi nzima.
 
Mkuu MMM akili zikizidi sana wakati mwingine hazimsaidii binadamu, nakubaliana na uwezo mkubwa ulionao kama Political analyst mzuri, lakini bandiko lako limejaa vitu vingi vya kufikirika zaidi, kwanza awali ya yote ungeonesha ni chaguzi ipi ndogo ambayo imefanyika na CCM ikashinda ili hali jimbo halikuwa lao?

Haya yote yanaeleweka na najua wasomaji wanajua. Tarime ilikuwa jiimbo la CDM chini ya Wangwe likatetewa lakini uchaguzi wa 2010 likarudi CCM. Uchaguzi ule wa 2010 ulichukua majimbo kadha wa kadha yaliyokuwa ya CCM ukaleta CDM kwa hiyo kwamba CDM haiwezi kwenye majimbo yaliyokuwa ya CCM haina msingi.

Pili kama utakumbuka mwaka 2010 ulituambia hapa hapa uchaguzi ule mkuu kwa namna yoyote matokeo yake hayachakachuliki? je walikumbuka hili!? na kama unakumbuka ulichokisema je uchakachuwaji ulikuwepo au lah?

NIna kumbukumbu nzuri sana - Sijawahi kusema kitu kama hicho.

Tatu kama unazungumzia swala la viongozi kuwajibika hebu nipe tathmini yako tangu Mwenyekiti akiwa Edwin Mtei, Bob Makani na sasa hivi Freeman Mbowe je ni uongozi upi ambao umefanikiwa kukijenga chama? kama utakumbuka Mbowe huyu mwaka 2005 alikubali kupoteza Ubunge wa Hai ili akijenge chama chake kwa kusimama ulingoni na Jakaya Kikwete tena wakati huo JK akiwa ni chaguo la Mungu (Ni dhahiri Mbowe aligombea huku akijuwa ni ndoto kumshinda JK) je huyu sio mpiganaji wa kweli?

Hapana, sijasema kiongozi yeyote atakayewajibika siyo mpiganaji. NInawaheshimu sana hawa wote - mmoja mmoja na kwa ujumla wao na ni viongozi wa kihistoria lakini haitaondoa ukweli kuwa itabidi wawajibike wakishindwa Arumeru. Jamani, hata kocha mzuri akishindwa kuifanya timu ishinde au kufanya vizuri anawajibishwa. Haiondoi ukweli kwamba ni kocha mzuri au ana uwezo wa kufundisha timu ikashinda. Its not personal.

MMM nadhani unajuwa fika kabisa ni namna gani ilivyokuwa ngumu kuanzisha chama cha siasa na kukifikisha ngazi kama iliyofikia CHADEMA? nadhani wewe binafsi ni shahidi mzuri wa hili maana Mlipoanzisha chama chenu CCJ kilikufa hata kabla hakijapata usajili wa kudumu na Makamanda wenzako waanzilishi ambao uliwaamini wengine wamejisalimisha CCM, je hapa huoni kwamba si kazi rahisi kujenga Chama kama unavyotaka kutuaminisha?

Miaka 17 ya uzoefu wa vyama vingi CDM haiko sawa kwa kipimo chochote na CCJ. Angalia CCK imeweza kusajiliwa baada ya kubadilisha mkakati kabisa na kuwaondoa watu waliokuwa kikwazo. Mambo ni mikakati tu - hakuna mtu aliyejua CCK inapata usajili wa kudumu hadi dakika ya mwisho. Niambie hilo.

Hitimisho: Nina imani na uongozi wa CHADEMA na nina Imani na CHADEMA kama taasisi, na nionavyo mimi uongozi huu unastahili pongezi kwa kukifikisha chama katika stage hii ingawa changamoto ni nyingi, lakini kusema CHADEMA ni lazima ishinde Arumeru bila kuwa na utafiti wa kisayansi ni kupotoka.

Unaenda mbali sana - sijasema mahali popote kuwa nimekosa imani nao hata kidogo. Kwanza ninaamini kwa kuwajibika endapo watashindwa Arumeru watazaidi kuwa na imani. Sijawaambia wavuliwe uanachama au wajiondoe kwenye chama. Usiende mbali sana kwenye kuwaza ndugu yangu. Nawatakiwa washinde Arumeru ndio maana nimewaongezea presha.

305650_10150602915896156_687191155_9755398_2030581143_n.jpg
[/QUOTE]
 
Huu uandishi wa kibongo umekaa kimapenzi sana. Yaani mtu anaonesha kabisa kuwa yeye ni mshabiki wa CHADEMA which thing grossly prostitutes 'journalism ethics'. A serious and committed journalist never alludes his political inclination to his work.

Miye ni mwanamaoni - columnist - na mwelekeo wangu wa kisiasa hauna utata.
 
Wrong analysis.
Off course huwezi kufanya analysis ukiwa unakula Burruto la Chipotle ndani ya Obamaland halafu unataka uzungumzie current affairs za Arumeru,......hapa mkuu MMM amepotoka, nilidhani angekuwa mjanja angejiuliza ni kwa nini Meneja kampeni wa CHADEMA ni mchungaji Natse na ni kwa nini kule hakuna kelele za Bakwata bali chokochoko za Washiri? hizi siasa za kwenye Mtandao hazipo Applicable katika kila nchi, huwezi kujuwa hali halisi ya Arumeru kwa online politics bali lazima uwepo kwenye Battle ground.
 
Kuna mambo ambayo wanaweza kufanya ili kuipa nafasi CDM ishinde:

a. Kwanza, watafute vitambulisho vyao vya kupigia kura. Kama hauna kitambulisho – tayari umepunguza kura!

b. Kama una kitambulisho hakikisha kiko salama. Kitambulisho cha kupiga kura ni kitambulisho cha haki yako kuzungumza na kusema. Kumbuka watawala hawaelewi Kiswahili wala Kiingereza! Wanaelewa kura tu! Kama hutopiga kura hawatajua umesema nini!

c. Muulize rafiki yako, ndugu na jamaa yako kama ana kitambulisho chake. Hakikisha kimepatikana kama. Kamwe usiuze au kumpa mtu mwingine kitambulisho chako. Kumpa mtu mwingine kitambulisho chako cha kupigia kura ni kumpa mtu sauti yako! Fikiria unampa mtu sauti yako halafu anaamua kutukana au kutozungumza kabisa! Usikubali mtu mwingine achukue kitambulisho cha ndugu au rafiki yako hata kama ikibidi kupigana pigana kutetea kitambulisho chako. Hakuna kiasi cha fedha katika dunia hii kinachoweza kulinganishwa na haki yako ya kuzungumza. Anayekubali kuuza kitambulisho chake ni mtumwa! Kwani ni mtumwa peke yake ambaye hana sauti mbele ya mtawala!

d. Siku ya kupiga kura usiondoke peke yako; hamasisha ndugu zako na jamaa zako na hata ikibidi kusaidiana usafiri kwenda kupiga kura. Hakuna ubaya kwa watu ambao mnampigia kura mtu mmoja kwenda pamoja, sheria haikatazi. Hata hivyo, unapoenda kwenye eneo la kupigia kura unaenda mwenyewe na utakapopiga kura utapiga mwenyewe! Usifikirie mwingine atapiga kura unayotamania wewe!

MM sina la kusema kuhusu mengine uliyoyasema bali hayo machache hapo juu. Katika hayo machache hapo juu nadhani hayo majukumu ya kila raia. Viongozi wa chama wanachoweza kufanya ni kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kuwachagua viongozi na chama wanachokipenda (hata kama mwamba ngozi huvutia kwake). Wananchi wakikubali kutekeleza wajibu wao watatunza kadi zao na kuzitumia kupiga kura.

Kingine kibaya zaidi ni kuwa hata tukiwalaumu vipi viongozi wa CDM watawezaje kazi unayotaka waifanye? Mfano, mafisadi wanawataja na kupeleka ushahidi kunakostahili, kama CCM inaiagiza serikali yake isipeleke kesi mahakamini viongozi wafanyeje? Wakiwakamata wanaonunua vitambulisho vya kupigia kura, vyombo vya dola vinawaacha huru, viongozi wafanye nini?

MM suala siyo CDM tu ishinde bali mshindi apatikane kihalali kwani hata CCM wanastahili kushinda lakini kihalali. Katika kesi moja ya uchaguzi katika Jimbo la Babati Magharibi mgombea wa NCCR - Mageuzi (Laurent Tara) alipinga ushindi wa mgombea wa CCM ( Jitu) na aliomba atangazwe mshindi. Msimamizi wa uchaguzi (mkurugenzi wa Wilaya Babati) alihojiwa katika kesi hiyo kuhusu idadi ya vituo vya kupigia kura na akataja kuwa ni vituo 323. Baadaye akaonyeshewa barua aliyoiandika mwenyewe yenye kutaja vituo 325 na alikiri kuwa ni barua yake. Akaulizwa kuwa ipi iliyo sahihi kati ya anayoyatamka na aliyoandika katika barua yake. Akawa bubu. Jambo la pili ni kuwa alikuwa na amejitengenezea fomu za matokeo aliyotumia kutangaza matokeo ambayo hayakusainiwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi. Hilo nalo alishindwa kulitolea maelezo na huko aliyefungua kesi alikuwa na nakala ya fomu ya matokeo katika vituo vinavyolalamikiwa.

Wananchi hawaporwi haki yao kwa kufanya ujinga wa kuuza shahada bali kuna hujuma kubwa toka tume ya uchaguzi katika kuwatangaza. Wananchi wakisubiri matokeo wanapigwa na polisi. Tutasema kuwa aende mahakamani ili aweze kupata haki. Huko nako tuna wasiwasi kwa sababu Mh. Jaji mkuu ameanza kulalamika kuwa mahakama haipo huru kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya wamaenza kupewa jukumu la kuwa viongozi wa mabaraza ya nidhamu ya mahakimu. Tunakumbuka sote kuwa wabunge wengi wa CDM walilipenga sana suala la mahakama kuwekwa chini wa wakuu wa mikoa na wilaya lakini wabunge wa CCM kwa uwingi wao walipitisha sheria hiyo ya ajabu.

Vita ya wananchi kupata haki yao ni kila mwananchi na wapenda haki wote ukiwemo wewe MM. Hayo ya mikakati ya vyama vya upinzani ni kwa ajili ya kuwaongezea nguvu wananchi na wapenda haki.
 
Lakini walipata majimbo ambayo hata hayakutarajiwa kabisa na kama yalitarajiwa ni kwa sababu ya mgombea maarufu aliyekuwa CCM akajiunga na CDM. CDM ilichukua Ukerewe, Biharamulo Magharibi, Bukombe, Meatu, Mbulu, na Mbozi Magharibi. CDM ikaonesha kuwa ni chama kinachokubalika nchi nzima na siyo cha Kaskazini kama ambavyo kilikuwa kinatuhumiwa. Ni wazi kabisa kama uongozi wa kitaifa ungekuwa umejipanga vizuri na kuamua kuweka msisitizo wa kushinda viti zaidi badala ya wao wenyewe kugombea CDM ingeweza kujikuta inafanya vizuri kupita hivyo. Lakini pamoja na matokeo yale bado hakuna kuwajibika kwa sababu wapo walioamini kuwa matokeo yale yaliakisi kweli hali halisi.

CCM, NEC na Serikali kulaumiwa

Nimewahi kuandika huko nyuma kuwa madai ya kuwa CCM na serikali inawaonea na kuwa inachakachua yana nguvu kwenye uchaguzi mmoja au miwili lakini kwenye chaguzi nane madai haya sasa yamepoteza nguvu. Inakuwaje timu inaenda kucheza na timu ile ile wanafungwa na kila siku wanalalamikia refarii? Wakati kila wakati wanajua refarii ni nani na wanaenda wakiamini labda atakuwa amebadilika? Hivi, Tume ya TAifa ya Uchaguzi imebadilishwa lini? Inaongozwa vipi? Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi ambao utasimamiwa na tume tofauti lakini ikiwa na sheria ile ile na tamaduni zile zile na hili CDM wanalifahamu!

CDM haiwezi kushinda kwa kujifananisha na CCM

Leo tumeshuhudia jinsi – katika hali ya kuchanganyikiwa – viongozi wa juu wa CCM wakitumia mbinu za kashfa za kutunga na kushambulia watu badala ya hoja na matokeo yake CDM nao wanaanza kujibu hivyo hivyo. Lakini msajili anapokuja kuzungummza anazungumza kana kwamba CDM ndio wabaya na kwa kufanya hivyo anaipigia debe CCM kiaina. Angalia Mkapa anasema vitu vya ajabu kuhusu Vincent Nyerere lakini ni Vincent anayeonekana kukosa adabu huku Waziri wa Serikali akitumia ujiko wake kusema mambo ya ajabu zaidi!

Kwa ufupi CDM inatakiwa ishinde Arumeru kwa kuwashangaza CCM kwa kwenda kinyume na matarajio ya CCM. Natumaini viongozi hawa wa taifa watatafuta na kupata mbinu ambayo hatujaiona katika chaguzi nane ndogo zilizopita za kuweza kuishangaza CCM. Sasa hivi vyama hivi vinafanana sana kwenye mikakati yake na kampenzi zake kiasikwamba kimahesabu matokeo bado yanaipendelea CCM! Haijalishi maelfu ya watu wanaotokea, haijalishi watu wanaonyosha vidole viwili na haijalishi maneno ya kujiamini uchaguzi unashindwa kwa mikakati na mbinu! Huwezi kushinda vita kwa mavazi na nyimbo bali kwa mikakati na mbinu. Kama mavazi peke yake yangekuwa yanashinda vita hakuna jeshi lililokuwa linaonekana vizuri kama jeshi la Gaddafi! Fikiria!

Mashabiki wakigeuka wapiga kura CDM itashinda!

Binafsi napuuzia kabisa picha na mikutano ya maelfu kwani kwangu haina maana yoyote ile. Sote tunajua hata kikija kikundi cha wachekeshaji watu watajaa, ikitokea ajali watu wanajaa, ikitokea umbea fulani watu watajaa. Haijalishi watu wanaojaa kwenye mikutani kwani kwa wengi hizo ni nafasi za kuwaona viongozi wanaowasoma na kuwasikia kwenye radio au kuwaona kwenye luninga. Kwa wengine hiyo ni nafasi nyingine ya kukutana na watu mbalimbali baada ya kazi kwani hakuna mambo mengi ya kufanya - kama isingekuwa kampeni labda watu wangeenda kwenye mpira, burudani n.k Kwa hiyo kampeni ni muda wa kuburudika tu. Watu wakishangilia na kupiga kelele za "people's power" haisaidii kumchagua Nassari!

Kuna mambo ambayo wanaweza kufanya ili kuipa nafasi CDM ishinde:

Lakini mwisho wa siku kama nilivyosema uongozi wa CDM unatakiwa uwe umefanya mabadiliko muhimu kujipanga vizuri ili kushinda Arumeru. Lakini kama wataenda wanavyoenda sasa na kwamba hivi wanavyofanya ndio kikomo cha uwezo wao basi wakishindwa – NI LAZIMA WAJIUZULU. Na hapa nina maana wote lazima wajiuzulu kutoa nafasi nyingine kwa viongozi wengine kuinuka kuweza kuongoza kuelekea 2015. Jamani, hata kocha anayefungwa kila mechi anafukuzwa. Ikumbukwe hawagombei "kura nyingi" kuliko uchaguzi wa 2010 - wanagombea kushinda!

Thread inapokwa ya hisia binafsi za mtu na si mtazamo wa wapiga kura wenyewe inakuwa haina maana tena. Hivi unategemea MBOWE, SLAA wa-step down kisa eti Wwameshindwa Arumeru Mashariki? watamwambia nini Mzee mtei eti mkwe wake kakosa nini mpaka awajibishwe? Tume ya Uchaguzi pateni somo kutokana na thread hii, ni mbinu gani CDM wanashauriwa kuzitumia ili kujipatia ushindi huko Arumeru Mashariki? wale wasiyo na shahada za kutopigia kura wahakikishe wanakua nazo, wazitoe wapi?

  • Binafsi napuuzia kabisa picha na mikutano ya maelfu kwani kwangu haina maana yoyote ile
  • Lakini walipata majimbo ambayo hata hayakutarajiwa kabisa na kama yalitarajiwa ni kwa sababu ya mgombea maarufu aliyekuwa CCM akajiunga na CDM. CDM ilichukua Ukerewe, Biharamulo Magharibi, Bukombe, Meatu, Mbulu, na Mbozi Magharibi
  • Inakuwaje timu inaenda kucheza na timu ile ile wanafungwa na kila siku wanalalamikia refarii?
  • Leo tumeshuhudia jinsi – katika hali ya kuchanganyikiwa – viongozi wa juu wa CCM wakitumia mbinu za kashfa za kutunga na kushambulia watu badala ya hoja na matokeo yake CDM nao wanaanza kujibu hivyo hivyo;
  • Haijalishi maelfu ya watu wanaotokea, haijalishi watu wanaonyosha vidole viwili na haijalishi maneno ya kujiamini uchaguzi unashindwa kwa mikakati na mbinu! Huwezi kushinda vita kwa mavazi na nyimbo bali kwa mikakati na mbinu. Kama mavazi peke yake yangekuwa yanashinda vita hakuna jeshi lililokuwa linaonekana vizuri kama jeshi la Gaddafi! Fikiria!
  • Kwa haki kabisa huwezi kuzungumzia kupigania haki za wananchi wetu kabla ya uhuru bila kugusia Meru katika ule Mgogoro wa Ardhi Meru. Wameru walitambua kuwa haki zao zilikuwa zimevunjwa na utu wao kudharauliwa. Hawakuwa tayari kupiga magoti mbele ya watawala wa zama hizo. Siyo chini ya tishio la bunduki za Wajerumaini au kutii utawala wa Mwingereza. Walijitahidi kupinga na walipinga kweli kweli.

Sitaki kuendelea na kunukuu maneno mengi sana ila nadhani CHADEMA si chama cha siasa hata kikitetewa vipi na mwisho wake utakuja kuonekana pale ambapo kitaliingiza taifa katika matatizo kama ambavyo vikundi vilijifanya vinatetea haki kule Tunia, Libya na kwingineko, na sasa tunashuhudia wananchi wa nchi hizo wakibaki wanajuta. Lakini pia tumshukuru mungu kwa vile sasa baadhi ya watu wanaanza kutambua kuwa baadhi ya viongozi wa Kikundi hiki (siwezi kukiita chama) kuwa wanatakiwa kupisha ili taifa libaki slama. Watu wameanza kutambua kuwa umaarufu wa kikundi hiki unachangiwa na zile pumba ambazo zinaondolewa CCM ambazo zina tamaa na damu ya wazalendo wa nchi hii.

Watu wanaanza kutambua kuwa wingi wa watu wanaokwenda kuangalia helikopta na kufurahia matusi majukwaani si wote ambao mwisho wa siku watapiga kura.

Watanzania tuendelee kuwaunga mkono watanzania ambao sasa wazinduka na kugundua kuwa CHADEMA si chama cha SIASA bali kikundi ambacho kinalalama siku zote kwa kutaka tu damu ya watanzania utadhani ni majni.

Kinyume na wengi wanavyochukulia majimbo waliyoyapata 2010 - mengine kwa mbinde sana - ni jambo la kujivunia kwa kiasi tu lakini it was way below mathematical projections kama wangefanya vizuri. CDM wasingepata less than 90 seats..

MMM
Na tukiangali maandalizi ya 2015 je? unaonaje uongozi huu ulivyoshindwa kusimamia mkakati wake wa kutenga 20% ya ruzuku kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi ujao?
 
Thread inapokwa ya hisia binafsi za mtu na si mtazamo wa wapiga kura wenyewe inakuwa haina maana tena. Hivi unategemea MBOWE, SLAA wa-step down kisa eti Wwameshindwa Arumeru Mashariki? watamwambia nini Mzee mtei eti mkwe wake kakosa nini mpaka awajibishwe? Tume ya Uchaguzi pateni somo kutokana na thread hii, ni mbinu gani CDM wanashauriwa kuzitumia ili kujipatia ushindi huko Arumeru Mashariki? wale wasiyo na shahada za kutopigia kura wahakikishe wanakua nazo, wazitoe wapi?
umekosea treni buddy..
 
Mkuu, watu wamekubali kwenda kwenye uchaguzi wakijua NEC ni ile ile - basi hiyo inakuwa assumed kwenye equation. Hakuna chochote kilichobadilika kati ya uchaguzi wa Igunda, Uvini na huu wa Arumeru.

MM, mbona na wewe umeanza kutoa maoni yako na NEC ikiwa ile ile? kwa hivyo hakuna kilichobadika. Kutokwenda kwenye uchaguzi kutamgharimu nani kati ya chama (CDM) na mwananchi? Hapo naona kama huna hoja vile.
 
MMM
Na tukiangali maandalizi ya 2015 je? unaonaje uongozi huu ulivyoshindwa kusimamia mkakati wake wa kutenga 20% ya ruzuku kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi ujao?

Kwa kweli sijui internal dynamics za chama. I'm the wrong person kujaribu kujibu hili.
 
Back
Top Bottom