Ilipo ishia
Monica alikuwa kama kichaa sasa, na alipata nguvu za ajabu.
PART IV Maisha ya Kishujaa Porini Inaendelea....
Monica alibadilika kabisa na kuonekana kama mnyama. Hakuwa muoga tena maana vitendo alivyovifanya sasa ni vya ajabu mwanadamu wa kawaida hawezi kuvifanya. Sauti yake nyororo ya kirembo ilibadilika na kuwa sauti nzito. Monica hakuwa na akili tena za binadamu wa kawaida.
Baada ya kurarua rarua mzoga wa simba, Monica aliishiwa nguvu na kujikuta anaanguka chini. Macho yake hayakuweza kuona vizuri tena. Japo kuwa kulikuwepo na mwanga wa mwezi giza nene lilitanda kwenye macho yake. Alishindwa kabisa kufanya chochote.
Baada kama dakika tano hivi, aliona viumbe mithili ya mwanadamu vikitokea kwa mbali. Monica alijaribu kunyanyuka hakuweza kabisa maana nguvu zilimwishia. Viumbe wale walizidi kumkaribia. Akili za Monica zilikuwa zinafanya kazi lakini viungo vyake vya mwili havikuweza kabisa kufanya kazi.
Viumbe vile vilikuwa na miguu miwili kama ya mwanadamu, mikono yake ilikuwa mirefu sana, uso wake ulifanana kabisa na punda maana mdomo wake ulichongoka. Cha ajabu viumbe hao walikuwa na manyoya ya rangi tofauti tofauti. Lakini kwenye shingo yao walikuwa na rangi ya kijani. Urefu wao ulikuwa kama futi 12 mpaka 15. Alikuwa wamejipanga mistari miwili kama askari waendao vitani. kadri walivyo karibia aliwaona dhahili kuwa wakotofauti na mwanadamu maana walikuwa na mapembe 6 kwenye vichwa vyao.
Wanyama hao walikuwa wanakuja kwa kasi ya ajabu. Walionekana wenye hasira sana maana nyuso zao zilikunjamana. Alisikia sauti kutoka kwa mmoja wao "Uliokoka wakati ule leo tumejiandaa na hakuna wa kukusaidia" Monica hakuwa na nguvu, hakuweza kabisa kujisogeza, kinywa chake kilikuwa kizito, hakuweza kuongea chochote.
Wanyama wale walifika sehemu alipokuwa Monica, wakamzunguka wote kwa pamoja wakapiga kelele "Wuuuuuuuuuuuuuuuu Woooooooooo tutakuchukua tutakuchukua".
Baada ya hapo walianza kuimba wimbo:-
Kamwana, kamwana tukachukue tukapeleke kwa mtemi x2
kataweza kuwa ka mwali kamwali ka mwana ka mtemi x2
kamwana, kamwana tukachukue tukapeleke kwa mtemi x2
Wakati wanyama hao wakiendelea kuimba wakiwa wamemzunguka Monica na Monica hawezi kufanya kitu chochote ulitokea upepo mkubwa, ngurumo za radi zilisikika, mwezi ulipotelea kwenye mawingu.
Monica alipoteza fahamu na hakuelewa kabisa kitugani kiliendelea baada ya hapo.
Mbwa walisikika wakibweka, ndege wakiimba. Mwanga wajua wa asubuhi ndio ulimuamsha Monica.
Mpenzi msomaji hebu endelea kusoma hii stori ya kusisimua usiondoke hapa JF.......