Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,951
- Thread starter
- #41
Ilipoishia
Katarina ni mwanamke mrefu mwenye shingo ya twiga, pua yake imechongoka kidogo na anaumbo la namba nane. Nimwamke mwenye mazoezi, ukimwangalia tu hakika utatamani japo umkumbatie.
PART V Mafunzo ya Kijeshi
Monica alikuwa akiwaza sana sasa "Hivi kweli ndoto yangu yakusoma ndio imezimika hivyo!!, Na wazazi wangu sijui sasa wanafikiria nini" Monica alipiga moyo konde na kujipa matumaini siku moja ataonana na wazazi wake na kurudia maisha yenye furaha.
Hakuna mtu aliye kuwa anaongea wakati huo, Katarina alikuwa yuko kimya lakini macho yake yalikuwa yakipepesa pepesa.
Baada ya muda wa masaa 14 walikuwa tayari wamekaribia kwenye kambi No3 ya A13.
Walipofika walishuka huku Monica akichechemea. Walipewa chakula pamoja na wenzake.
Kuseakweli chakula kilikuwa kizuri chenye afya.
Baada ya kumaliza kula kilammoja alipewa mavazi. Walipewa Sare, nguo zenye langi ya kijivu aina ya kadeti (Suruali na shati).
Eneo lile nilikua na askari kila mmoja alikuwa na kazi anafanya. Wengine walionekana wakikimbia kimbia huku na kule. Magari ya kivita yalikuwa yamepaki eneo fulani. Vifaru vya aina tofauti tofauti vilionekana pale.
Monica aliona kama ndoto vile. Maana vitu hivyo alikuwa anaviona kwenye video tu. Sasa hapa anaona kwa macho yake.
Walielekezwa sehemu ya kuoga na kuamriwa baada ya kuoga wabadilishe nguo na wavae zile sare. Walifanya hivyo.
Monica alipendeza sana.
Katarina aliwaita nakuanza kuwaeleza:
Kesho mtaandikishwa kwenye daftari majina yenu. Mtakaa siku tatu baada ya hapo mtaondoka eneo hili na kupelekwa sehemu ya mazoezi.
Walielekezwa sehemu ya kulala.
Kusema kweli eneo lile lilikuwa zuri na walihudumiwa vizuri sana.
Katika kundi hilo la akina Monica wakuwemo wasichana 5 aikiwemo na Monica. walielekezwa sehemu ya kulala wanawake. Baada ya kufika kula walitambulishana majina yao.
Monica, Alice, Tekra, Sofia na Vivian.
Monica alieleza yeye anatoka Maganzo. Hawakuelewa Maganzo iko wapi maana wote hao walikuwa sio watanzania. Monica aliwashangaa sana yaani hawajui maganzo!!.
Aliwaeleza maganzo iko wapi na wakaelewa.
Alice alikuwa akiongea kiswahili kibovu kibovu alisema yeye anatokea Somalia
Tekra yeye alisema anatokea Sudani.
Sofia aliongea kiswahili cha kikenya akasema yeye ametokea machakosi
Vivian akasema yeye ametokea Ethiopia.
Walitambulishana na kujuana zaidi.
Baada ya muda kama wa dakika 30 hivi askari akapita na kuwaambia wasiongee walale. walikaa kimya na hawakuongea tena.
Mpendwa msomaji wa JF unaionaje hii stori. Endelea kuisoma na utashangaa namna Monica alivyo jifunza biashara ile.......