Monica wa Maganzo

Monica wa Maganzo

Wapenzi wasomaji wangu nitakuwa natupia mwendelezo wa stori hii Monday, Tuesday na Wednesday
 
Ilipoishia
Mafunzo ya kutumia silaha yalifanyika vizuri na mwezi wapili uliisha haraka sana.

PART V Mafunzo ya Kijeshi inaendelea....

Ilikuwa jioni Katarina aliwakusanya na kuwaeleza kuwa watasafiri kwenda Lubutu mji huo mdogo uko karibu kabisa na pori la Maiko huko ndiko watafundishwa mambo saikolojia na kutunza siri.

Siku ilifuata walianza safari kuelekea Lubutu safari ilikuwa ndefu yapata kama kilomita 619 nikama mwendo wa saa nane na nusu hivi. ilipofika mida ya saa 7 za mchana tayari walikuwa wameshafika Lubutu.

Siku iliyofuata walianza mwalimu wa saikologia alianza somo. Alianza kwa kuwaeleza tutajifunza vitu vya msingi tu, baada ya hapo mtachukuliwa kwenda nchi ya urusi huko mtajifunza zaidi. Tutajifunza vitu vifuatavyo:-

1. Intelligence (Akili, Inteligensia)
2. Memory (Kumbukumbu)
3. Emotion (Hisia)
4. Brain and Behavior (Ubongo na Tabia)
5. Learning (Kusoma)

Basi mwalimu alianza kwa kuwaeleza kuwa tuna wiki 8 za kujifunza kuhusu saikolojia ninawaomba muwe makini na waelewa maana nitaenda taratibu kadri niwezavyo.
Usipoelewa basi usiste kuuliza swali.

Kwanza kabla ya kuendelea ningependa nijitambulishe kwanu, mimi ninaitwa mwalimu Albert Hansi
Sasa basi leo tunaanza kujifunza kuhusu Inteligensia, kwanza kwa kuanza kabisa ningependa kueleza nini maana ya inteligensia.
1. Ni uwezo wa kupata na kutumua maarifa na ujuzi.
2. Hapa nitaongea kwa kingeleza mtaenda kutafuta maana yake kwenye kiswahili (
An agency of the armed forces that procures, analyzes, and uses information of tactical and strategic military value.)

Wakati huo mwalimu alikuwa akiongea huku akiandika ubaoni. Wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.
Mwalimu aliendelea kufundisha na kueleza nadharia mbali mbali za inteligensia.
Alielezea nadhalia ya Charles Spearman.
Alieza kwa utangulizi kabisa tunatakiwa kujifunza nadharia hii maana ndio msingi wa saikolojia.
Siku hiyo alijikita sana katika nadharia ya Charles Spearman.

Kwa muda wa saa moja na nusu kipindi kiliisha.

Baada ya kama dakika 40 hivi mwalimu mwingine aliingia, yeye alijitabulisha kwa jina la Don Roony, yeye aliingia darasani na kuanza kufundisha kuhusu kutunza siri. Aliwaeleza mbinu za awali za utunzaji wa siri.

Vile vile alieleza kadri mnavyo zidi kujifunza somo la saikolojia ndio tutakavyo zidi kujifunza somo langu kwa undani zaidi. Alisema unajua masomo langu linategemea sana somo la saikolojia. Yaani kuwa na akili ya kusoma mazingira na kumsoma mtu.

Aliongeza kusema unaweza ukatumia taarifa zilizo mbele yako na kukuwezesha kutunza siri. eliendelea kusema sisi tuko na maadui wengi sana hapa duniani kwahiyo somo hili ni la muhimu sana. Unajua Adui yako akijua siri zako tayari atakuwa amekumaliza. Sasa basi ni muhimu sana kusikiliza masomo yote haya mawili kwa umakini wa hali ya juu.

Baada ya kipindi chake muda wa dakika 40 mapumziko yalianza. Baada ya mapumziko Katarina aliwachukua na kuwapeleka kwenye maktaba iliyokuwepo pale.

Wakati huo Monica alikuwa haelewi kabisa kitu gani sasa. Akawa anamuuliza Viviani hivi mbona naona mambo yote mageni hapa kwangu. Akili zangu zimegota sielewi kitu. Viviani naye akajibu hata mimi sijaambulia kitu chochote hebu ngoja tusubiri maana ndio kwanza tunaanza kujifunza.

Sikuhiyo ikapita kama upepo na wakajikuta ngiza linaingia kwa haraka mno

Mpenzi endelea kuisoma hii stori.








 
Ya leo fupi sana jamani tupe utamu huo, story yako ni nzuri sana Annaeli...

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Ilipoishia..
Sikuhiyo ikapita kama upepo na wakajikuta ngiza linaingia kwa haraka mno

PART V Mafunzo ya Kijeshi inaendelea....


Usiku huo Sofia alikuwa kinara wa maongezi alikuwa akiongea sana na kuwashangaa kwanini hawajaelewa wakati yeye alijitapa na kusema ameelewa kila kitu na anajua sana masomo hayo.

Wengine wote walikuwa wakokimya wakimsikiliza yeyetu. Sofia aliongea sana na kumcheka Monica kuwa kuchwa chake ni maji hakiwezi kuelewa chochote.

Ukweli Viviani na Monica hawakupendezwa na kitendo hicho na kwakuwa wamefundishwa japo kidogo utii walimchukulia kama mjinga fulani. Kunawakati Viviani alitaka kuwa kama mbogo ili amrarue Sofia kwa majigambo yake lakini Monica alimkataza na kumwambia achana na huyo mjinga.


Sikuiliyo fuata sasa kipindi cha kwanza kilikuwa ni kuhusu somo la kutunza siri. Mwalimu aliingia kama kawaida na wote wakafungua madaftari yao.

Mwalimu alianza kutoa mifano mingi ya watu waliokuwa mashujaa kwaajili ya kutunza siri.
Aliendelea kueleza kuwa mtambue kuwa nyie ni askari sasa kama nyie ni askari ni vyema kujua kuwa kunawaki utakuwa umetekwa na adui mara nyingine adui huwa hana uhakika na kwamba wewe ndie muhusika lakini mara nyingine adui anajua kuwa wewe ndie muhusika.

Sasa basi kwasababu mtajifuza kwenye saikolojia kuhusu kusoma (kusoma mazingira na kumsoma mtu) mtaelewa kabisa huyo mtu aliyekukamata anauhakika kiasi gani kuwa wewe ndie muhusika.

Kwakuwa mtakuwa askari mnaojihusisha na upelelezi na intelijensia kuna miiko. Na miiko hiyo inasaidia sana katika utunzaji wa siri.

Kitu cha kwanza kabisa ni huruhusiwi kumpenda kimapenzi mtu yeyote. Katika somo hili la kutunza siri tutajifunza kiundani zaidi tena kwa vitendo.

Kipindi cha mwalimu kiliisha haraka. Huku Monica alikuwa akitabasamu kuashiria kuwa ameelewa.

Sofia alipomtazama Monica alikasirika na kununa maana alikuwa hapendi kabisa kumuona akifurahi.
Baada ya kipindi alianza kujadiliana na kusimuliana stori mbali mbali za kwenye video alizoziona.

Yaani Monica alifurahi sana kuona kumbe hata yeye anaweza kufanya yale ya kwenye video aliyokuwa anayaona.

Baada yamuda kama dakika 40 hivi mwalimu wa saikolojia aliingia.
Alianza kwa kukumbushia pale walipoishia jana. Wakati anakumbushia Monica alijikuta akimuelewa vizuri sana mwalimu.

Baada ya mwalimu kuwakumbusha aliendelea kwa kusema kwakuwa sehemu kubwa ya saikolojia ni itelijensia sasa basi tutajikita ndani zaidi kwenye hili.

Sana sana tutajikita katika iteligensia za kijeshi. Hii inahusu na kujua mazingira ya sehemu husika. Aliendelea kusema, Mnajua mtaanza kutumwa sehemu mbali mbali kwaajili ya kazi kwahiyo ni muhimu sana kukusanya taarifa kwa umakini na haraka na kuelewa jinsi ya kuzitumia kwa uwepesi zaidi.

Aliendelea kuwafundisha mbinu mbalimbali za kupata taarifa kwa njia yakusoma, kusikiliza, kuangalia mazingira, kuhoji, kunusa, kugusa na kutumia tofauti tofauti kulingana na mazingira.

Mwalimu aliwafundisha siri mbali mbali kuhusu mwanadamu. Alijikita sana kwenye Siri za akili za binadamu (Secrete of Human Mind).

Aliendelea kusema kuwa mtu akifanya kitu kwa muda wa siku saba akiwa anakirudia rudia itakuwa tabia yake. Vile vile aliendelea kuwaeleza kuwa akili za mwanadamu zimejengwa katika msingi mmoja wa kutumainia. Alisema unajua kwanini watu wengi sana wa dini wanakuwa na wafuasi wengi, ni kwa sababu tu watu wanakuwa wamepewa tumaini flani. Na watu waliowengi huwa wanashindwa kuhoji na kuuliza itakuwaje.

Sasa basi kwa msingi huo kabisa utaweza kujua kua akili za watu huwa zinatafuta kuabudu kitu fulani ili kutimiza matakwa ya kutumainia.

Kwa mtazamo huo sasa utakuja kuelewa kuwa unaweza kuwajenga watu wakawa wa aina flani kwa kufuata kanuni hizi mbili nilizo zisema, nitakubushia kwanza mtu akifanya kitu kwa kukirudia siku saba mfulizo inakuwa tabia yake. Pili akili za mtu zimejengwa katika kutumainia.

Sasa basi nadhani mmenielewa hapa. Na haya mambo tutayaweka kwenye vitendo zaidi na kuyatumia kila tutakapotumwa kwenda.

Alisisitiza msisahau kabisa maana kitu hicho cha muhimu katika kazi yetu hii.

Aliendelea kusema kesho tutajifunza pia kuhusu namna gani ya kumfanya mtu aweze kuota kitu.

Mpenzi msomaji naona stori inanoga endelea kuisoma.....

 
JF Mnaionaje Stori hii (Baada ya kuisha hii nitawasimulia Hadith ya Amagedon war "Vita ya Amagedoni")
 
Hadithi yako nzuri ila unapotea sana

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hadithi ni nzuri hasa unapogusa maeneo yetu halisi ya maganzo
 
Wana JF nimerudi tena na stori yetu kaa mkao wa kula.
 
Ilipoishia
Mage alimuomba Monica awaombe wazazi ili wakifunga shule waende Sumbawanga. Monica alikubali. Monica aliwaambia wazazi wake.
PART II
Usiku wa Kuhangaika

Mzee Magina alikataa kata kata sababu tu kwamba Monica ni mtoto pekee wa kike lakini mama yake Monica alimbembeleza na kumsihi njinsi Monica alivyokuwa akielezea kuhusu wazazi wake Mage.

Mke wa pili wa Mzee Magina alijulikana kwa jina Kagole lakini jina lake halisi alikuwa akiitwa Nyandalo Ni mwanamke aliyejaliwa kiwa na ushawishi wa hali ya juu. Mzee Magina alikuwa anapenda sana kumwita Kogole. Yaani alikuwa anatamka kwa Lugha ya kisukuma Kagole wane
Ikiwa na maana ya Kagole wangu.

Mzee Magina alikubali na kuhakikisha kuwa anampatia vitu vyote vya muhimu ikiwamo vitu vya kimila.

Siku ya kufunga shule ikafika Monica alisema anakumbuka kabisa siku hiyo ilikuwa siku ya ijumaa. Mimi na Mage tulifungasha mizigo yetu na kwenda kuwaaga wazazi wangu Maganzo.

Siku ya jumamosi Mzee Magina aliwasindikiza stend ya mabasi yanayotoka Mwanza kuelekea Tabora.

Walipo panda basi tu, ndipo Mage alianza kumweleza vitu vilivyomfanya Mage ashangae na kutamani wafike haraka aweze kujionea kwa macho yake. Stori zilizidi kupamba moto huku Mage akiwa ndiye kinara wa kutoa stori.

Ilipofika mida ya saa 10 za jioni tayari walikuwa wameshapita Tabora. Na msitu mnene ukawa unawaita, msitu ule ulikuwa namiti mikubwa mikubwa na kufanya jua lisionekane.

Nyimbo za ndege na sauti za wanyama mbali mbali zilitanda kwenye msitu huo, na istoshe mda huo njio ndio inaingia. Ghafla kulisikika mlio mkumbwa na kishindo wa "Pwaaaaaauuuu!!!" na basi walilokuwa wakisafilia "Roho ya paka" likayumba kulia kushoto kulia kushoto baada ya hapo likaacha njia.

Kila mmoja ndani ya basi alikuwa akimuomba Mungu wake. Basi lilipoteza mwelekeo na kujita linaparamia miti, likagonga mti mmoja na kumbiringika.

Monica: Niliona watu wenye nguo nyeupe wakitokea pande nne za dunia na mmoja wao akasema "muacheni kwanza huyu ngoja wengine wote tuwachukue" Nilijaribu kuongea kuwa uliza nyie ni nani lakini mdomo wangu ulikuwa mzito sikuweza hata kuongea, akilini ninawaza cha kusema lakini siwezi.

Baada ya hapo kitu gani kilitoke endelea kufuatilia




inaanza namaumivu iv polen sana japo nstor sijajua nialisi au la ila inauma sana
 
Back
Top Bottom