Money can't buy love. Tusidanganyane

Money can't buy love. Tusidanganyane

Kwenye noti ndio mahali watoto wazuri wanapo kaa. wewe usitafute pesa utaona unapo kwamia
 
Nyie ndio wale wale wakusema "Education is better than money" [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Money can't buy love yes....but it can rent it!!
 
Kumekuwa na mitazamo kadhaa wa kadhaa kwa sasa katika jamii kuhusu mahusiano na wengi wamekuwa wakisema pesa Ina nguvu Sana katika mapenzi.

Wengi wanaamini kuwa pasipo kuwa na Pesa kwa sasa huwezi kuyafurahia mapenzi utakuwa Kama mwizi aliyeiba naye akaibiwa kariakoo.

Bila Pesa utasikia wanasema huwezi pata mpenzi la hasha. Hata ukimpata mpenzi mapenzi yenu hayawezi dumu ni Kama kujisumbua

Wanawake wa sasa ni Pesa tu. Piga kazi utafute pesa upate penzi ufurahie lakini imani yangu ni kuwa mapenzi ni hisia za kweli kwa mwenza. Pesa inaweza kuwa kigezo cha kupata penzi.

Kwa uzoefu wangu watu wengi wanapokuwa katika mahusiano mapya na wanawake wapya hujiona wapo sehemu Salama kwani haoni dalili za kupigwa mizinga kuombwa hela hivyo hujiaminisha hakuna mapenzi ya pesa

Lakini naomba niseme jambo hili hakuna Kiumbe anaetumia akiri ndani ya mahusiano kama mwanamke na akiri ya mwanamke ndani ya mahusiano yeye hutumia kukusoma Tabia, mienendo yako na kiuchumi uko vipi .

Akiona mtu mwenyewe hoe haee tegemea kubreak up nae siku akikutana na mtu ambae ni bora kuliko wewe tegemea kuachwa tuu broo kwa visa vituko na vitimbwiiii
 
Back
Top Bottom