Ukarabati wa ndege yetu ilolala Karume International Airport Zanzibar kwa siku kadhaa (sijui ngapi) unaendelea na sijui tatizo gani...
Labda Air Tanzania wauarifu umma na pia kazi inaendeleaje
Picha ya chini ni injini ya ndege ya Emirates ikifanyiwa service.
=======
UPDATES: Ufafanuzi
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema ndege aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo imeanza kufanya safari zake kama kawaida.
Ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Agosti 21, 2019 katika kipindi cha Power Breakfast cha Redio Clouds akizungumzia taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha picha ya ndege hiyo ikiwa katika matengenezo.
Zaidi, soma;
Mkurugenzi ATCL: Ndege ya ATCL ilitengenezwa kwa siku moja na tayari inaendelea na safari zake
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema ndege aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo imeanza kufanya safari zake kama kawaida. Ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Agosti 21, 2019 katika kipindi cha Power Breakfast cha Redio Clouds akizungumzia taarifa...
www.jamiiforums.com