Moja ya ndege za ATCL Bombardia iko Zanzibar wiki ya pili sasa inatengenezwa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269


Ukarabati wa ndege yetu ilolala Karume International Airport Zanzibar kwa siku kadhaa (sijui ngapi) unaendelea na sijui tatizo gani...

Labda Air Tanzania wauarifu umma na pia kazi inaendeleaje
IMG_20190820_204722.jpg


IMG_20190821_085206 (1).jpg


Picha ya chini ni injini ya ndege ya Emirates ikifanyiwa service.

DU4MCUADWJEGBBR7I5T6JNSVPQ.jpg



=======

UPDATES: Ufafanuzi

Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema ndege aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo imeanza kufanya safari zake kama kawaida.

Ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Agosti 21, 2019 katika kipindi cha Power Breakfast cha Redio Clouds akizungumzia taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha picha ya ndege hiyo ikiwa katika matengenezo.

Zaidi, soma;


 
Hiyo kawaida tu kama ambavyo ndege ya Kenya Airways ilipokuwa imeegeshwa nchini siku kadhaa ikifanyiwa ukarabati baada ya kugonga kitu.

Hicho ni chombo cha moto kinatumika lazima kinapata itilafu, na kinachakaa. Hivyo lazima kifanyiwe ukarabati.
 
hata gari lako huwa unalifanyia service mtoa mada kama huna gari hata baiskeli lazima ifanyiwe service nacho kiona yani nyie kila kitu ni kukosoa vingine muwe mnaacha vipite jamani khaaa
Nani amekosoa.
 
Hiyo kawaida tu kama ambavyo ndege ya Kenya Airways ilipokuwa imeegeshwa nchi ikifanyiwa ukarabati baada ya kugonga kitu.

Hicho ni chombo cha moto kinatumika lazima kinapata itilafu, na kinachakaa. Hivyo lazima kifanyiwe ukarabati.
Hakuna mtu aliyesema siyo kawaida ndege kutengenezwa.
 
Hahaaa tunatunza tuu kumbu kumbu sie siku tutakapo mburuza Mbele ya mahakama ya ufisidi atalia na kusaga meno. Hatuja sahau kile Kivuko chake Fake alicho kificha kule jeshini na sasa kaongeza kununua li dege bovu.

Halafu utamsikia bwana Meko, "Watanzania tumeibiwa sanaa, wakati jenyewe ndio jizi kuu na genge lake linalo jificha ktk kivuli cha uzalendo.
 
Ndege ina muda maalumu na sehemu maalumu ya kufanyiwa service siyo kila siku iko chini ya mwembe kama DCM la Mbagala.
Umejuaje kama muda maalumu unaousema haujafika?. Na je kama ilipata hitilafu kiasi kwamba haiwezi kuruka kwenda garage ulitaka wafanyaje?. Wiki iliyopita tumeshuhudia ndege ya urusi ikipata hitalafu angani na kutua porini.
So nao wamenunua ndege mbovu!!?.
 
Back
Top Bottom