Modem ya tigo inanitatiza

Modem ya tigo inanitatiza

Ms Judith

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2010
Posts
2,563
Reaction score
932
wapendwa, habari za siku nyingi.

kwa sasa niko dar na katika kujiweka sawa na mambo ya mtandao nikanunua modem ya tigo ya kutumia kwenye laptop yangu. ila cha kwa kweli sijaifurahia huduma hii. niliponunu waliniambia ina GB 3 ila katika kuitumia haina hata KB 1! hilo si la kusumbua sana ila lililonisikitisha ni kuwa, haina kasi kabisa licha ya kuwa mtandao unaonekana strong! kuna wakati nafungua website inatumia zaidi ya dk 10 na hatimaye inashindwa kabisa kufungua.

nimewapigia tigo simu mara kadha ila wameshindwa ku-fix tatizo na pia nimwatembelea kama mara mbili hivi pale mlimani city. kwa kweli najisikia kuitupa kabisa hii modem!

wapendwa, naombeni ushauri wa nini cha kufanya zaidi.

mbarikiwe sana,

Glory to God!!​

Sijawahi kufurahia huduma za tigo hata siku moja ...ni majanga hawa jamaa!! Nakushauri Nunua Modem ya zantel hiyo itupie chooni ya tigo!! Hata airtel kwa mazingira ya dar ni mzuka pia!! Na kama kabla ya kununua ungekuja kuomba ushauri hapa hamna ambaye angekuambia ukannue modem za tiGO
 
wapendwa, habari za siku nyingi.

kwa sasa niko dar na katika kujiweka sawa na mambo ya mtandao nikanunua modem ya tigo ya kutumia kwenye laptop yangu. ila cha kwa kweli sijaifurahia huduma hii. niliponunu waliniambia ina GB 3 ila katika kuitumia haina hata KB 1! hilo si la kusumbua sana ila lililonisikitisha ni kuwa, haina kasi kabisa licha ya kuwa mtandao unaonekana strong! kuna wakati nafungua website inatumia zaidi ya dk 10 na hatimaye inashindwa kabisa kufungua.

nimewapigia tigo simu mara kadha ila wameshindwa ku-fix tatizo na pia nimwatembelea kama mara mbili hivi pale mlimani city. kwa kweli najisikia kuitupa kabisa hii modem!

wapendwa, naombeni ushauri wa nini cha kufanya zaidi.

mbarikiwe sana,

Glory to God!!​

  • Pole sana ndugu.
  • Taja model ya modem mfano HUAWEI E303 au HUAWEI E173 ili tukupe njia sahihi ya kuchakachua ili utumie laini yeyote.
 
I meant model na namba yake! Like Huawei E177, ama Huawee E220....kuna model number somewhere angalia ndo tuanzie hapo.

  • Pole sana ndugu.
  • Taja model ya modem mfano HUAWEI E303 au HUAWEI E173 ili tukupe njia sahihi ya kuchakachua ili utumie laini yeyote.

asanteni sana wapendwa, ni E 303 na chini yake kidogo imeandikwa CE 0682

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
 
asanteni sana wapendwa, ni E 303 na chini yake kidogo imeandikwa CE 0682

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
  • Huawei E303 ni moja kati ya modem bora na ni rahisi kuichakachua. Fuata hii link soma maelkezo kwa umakini. ( Credit to Kimox Kimokole )
    Code:
    [URL]https://www.jamiiforums.com/tech-gadgets-and-science-forum/303310-finally-huawei-e303-unlocked.html[/URL]
Karibu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom