Mobile Phone Company (Provider) kuanzisha Tanzania

wanapolumbana

weakness


Hivi udhaifu wa mwingine utauchukuliaje kama "challenge to you"? Hahahahahha........ Mfano, mtu anasema hajui Kiswahili, hiyo ni challenge kwangu mimi? heheheheee...Duu!

Nimehoji swala lililoletwa na mtoa mada. Ni mtandao gani huo ambao 7,500/= haitoshi kuongea dakika kumi?

mkuu...yaani nimecheka mpaka basi tena......... hii kiboko
 
Jibu hoja, habari zako za "udaku" weka pembeni:
Mtandao gani umejaribu Tanzania ukashindwa kuongea dakika 10 kwa vocha ya 7,500/= ??

Huo ni udaku? Au huelewi kinachoandikwa, maana umesema lugha inakusumbua.

Mkuu nadhani kwetu Tanzania ishakuwa kawaida kusema dola tano ni shillingi elfu 5!!! Ni makosa kwa kuwa yanaendana na thamani ya pesa ya miaka ile ya nyuma wakati mashirika ya simu za mikononi yalipoingia. Lakini bado inabaki kuwa ni anasa kupiga simu kupitia makampuni yetu Tanzania.
 
hii ndo bongo mkuu tafuata fisadi uingie nae ubia au patia yeye hiyo deal la sivyo ten percent na kuzungushwa sana inakuhusu:msela:
 
Sasa we Taso wewe unaona 7500 shillingi ni ndogo? jamaa aliye anzisha topic yupo sawa simu ni aghali sana nchini chukua mfano huu Ukraine si nchi tajiri sana ukilinganisha na nchi zingine kama maekani ila kuna mtandao maarufu sana unalitwa LIFE AMBAO ma UKILIPITA DOLA 4 UNAONGEA BURE masaa 24/7 NA UNAPATA SMS 120 KWA MWEZI kwa hivyo 7500 hata kama dakika 20 au saa bado ni aghali sana sana
 
Mkuu usione hizo bei ukachanganyikiwa......hiyo kampuni ikija bongo itakuwa na bei za kibongo....unajua kwa nini?

INFRASTRUCTURE!!!!!

bei hizo zinawezekana marekani na kwingineko kwa sababu wana hi-tech fiber network, na wireless comminication ni kwa ajili ya end-point delivery tu. Hapa bongo tokea sauti inatoka kwa operator mpaka inamfikia mhusika ni hewani tu.....ambayo ni very expensive na very inefficient.

Infrastructure ya Tanzania hairuhusu bei za chini kama ulaya.......ndio maana ingawa tulikuwa na internet kwa muda, ni baada ya SEACOM kufika ndio bei zimeenda chini.....kwa sababu wired communications ni cheaper kuliko aerial.

Makandokando,

Nakubaliana na wewe kabisa.
Kwamba kwa Tanzania usitegemee hata siku moja bei ya Mobile na Data(Internet) ikawa chini.Kuna sababu ziko nyingi zinazosabaisha Tarrifs ziwe juu. Kwa uchache nitajaribu kuainisha hapa chini:

  1. Miundo mbinu ni mibovu sana kwa nchi yetu hasa Barabara. Lakini pia gharama kubwa kutokana na Kodi kubwa zinazotozwa na Serikali kupitia TRA na TCRA kujenga Minara ya Mawasiliano(Towers+Microwave systems+Power supply).
  2. Umeme ni tatizo kubwa. Umeme wetu hauna uhakika na hata unapopatikna ni ghali sana. Makampuni haya ya Mobile na Data yanatumia pesa nyingi sana kununua Mafuta ili kuendesha hiyo Minara umeme unapokuwa umekatika. Gharama hizo za mafuta lazima zilipiwe na mlaji/mtumiaji wa huduma hizi. Bei lazima iwe juu.
  3. Urasimu na Ukiritimba ulioko BRELA na TCRA katika kusajili Kampuni na kupata kibali cha kuendesha biashara husika. Hapa lazima michuzi ikutoke kwa BRELA na TCRA. Gharama zote mwisho wa siku operata atataka pesa yake irudi through a consumer.
  4. Vigogo walioko ndani ya Serikali wenye hisa zao kwenye makampuni yaliyowahi kwenye biashara hii wanatumiwa na the same companies kuweka vikwazo ili wengine wasiingie kwa wingi kwenye soko na hivo kufanya huduma iendelee kupatikana kwa taabu. Wanatumia principle ya Demand/ Supply curve. Kwamba DEMAND inapokuwa kubwa na SUPPLY ikaendelea kuwa kidogo automatically BEI itakuwa JUU.
Nakumbuka incidence moja wakti TCRA walitoa bei elekezi kwa Makampuni ya simu za mkonon. Kuna yaliyopunguza kwa kiasi kidogo sana. VODACOM wao walikataa wakasema kuwa GHARAMA WANAZOTUMIA KUJENGA MINARA NI KUBWA SANA KWA HIYO HAWAWEZI KUSHUSHA BEI!!!Na kweli hakuna aliyewagusa VODACOM, si TCRA wala WIZARA. Sababu ya kiburi hiki ni kuwa PIUS MSEKWA by then speaker wa Bunge ndiye alikuwa Board Chairman wa Vodacom.

Kuna case kama ya TTCL ambayo ni kampuni ya Serikali au tuseme ya Wazawa. Lakini imetelekezwa kama nyanya mbovu. TTCL wana INFRASTRUCTURE nzuri na iliyoenea nchi nzima lakini angalia TTCL wanavosuasua kama watoto yatima vile. Wanaidai serikali 7Billion lakini haitaki kuwalipa. WAKIOMBA MKOPO wanaambiwa HAWAKOPESHEKI! I believe Mobile customer base ya TTCL haizidi hata laki tano. Sababu kubwa ni KUWA WAMEPEWA LESENI YENYE LIMITATION YA KUFUNGA WATEJA 100,000 KWA KILA MWAKA KWA MAELEKEZO YA WIZARA NA TCRA!!!

Tuliambiwa kuna MKONGO WA TAIFA maarufu kwa jina la OFC -ICTBB(Optical Fibre Cable-Information Communication Technology Backbone) kwamba huo ukishakamilika BEI YA DATA NA MOBILE ITAKUWA CHINI. It's now almost a year BEI za tarrifs ziko palepale
It will take a century for Tanzania to have reasonable tariffs in Mobile and Data(Internet)services.
 
Sasa we Taso wewe unaona 7500 shillingi ni ndogo?... mfano huu Ukraine ... kwa hivyo 7500 hata kama dakika 20 au saa bado ni aghali sana sana
Naona ni nyingi sana, ndio maana namwomba anieleze ni mtandao gani ambao 7,500/= haitoshi kuongea dakika kumi? Na hizo "dakika 20 au saa moja" tusibahatishe namba tu, unajuaje haizidi saa moja? Unalinganisha TZ na Ukraine? Linganisha na Msumbiji na Malawi, ndio hali yao hali yetu.

Kuna sababu ziko nyingi

  1. Miundo mbinu ni mibovu sana kwa nchi yetu hasa Barabara.
Ndio, kwa mfano, labda, tungeimarisha barabara kuu ipi itusaidie kusafirisha mawimbi ya simu na internet na kupunguza gharama?


Tuliambiwa kuna MKONGO WA TAIFA maarufu kwa jina la OFC -ICTBB(Optical Fibre Cable-Information Communication Technology Backbone) kwamba huo ukishakamilika BEI YA DATA NA MOBILE ITAKUWA CHINI. It's now almost a year BEI za tarrifs ziko palepale
Unadhani kwa nini iwe hivyo Mkuu? Miundombinu mibaya ya barabara na kukatikatika kwa umeme na ugumu wa kusajili BRELA?
 
ana maanisha domestic and International call, internet etc
Dollar 5 ni shilingi 7,500 takriban. Vocha ya 7,500/= unaweza kuongea zaidi ya dakika kumi mtandao wowote ule. Sijui hesabu zako unafanyaje. Na lugha nayo unasema inakusumbua, sasa hapo sijui tusaidiane vipi.
 
ana maanisha domestic and International call, internet etc
internet access inapimwa kwa dakika toka lini na wewe? Tunaongelea simu, kasema 7,500/= hazitoshi kuongea kwa dakika kumi. Mtandao gani huo?

Rates zenyewe za kupiga simu mtu hajui, marketplace picture huijui hata chembe halafu unasema unataka kufungua kampuni ya simu, na lugha anadai hajui, si ndo hawa wababaishaji wa ki-Richmond Richmond hawa?
 
True story nina rafiki wawili kwa wakati tofauti tofauti wamejaribu kuingia kwenye Telecommunication market ya Tanzania na mpaka sasa kesi zao ziko mahakamani.

Mmoja alifanya partnership ya 30% + 5% kwa kigogo na 65% ya non Tanzanian investor ambao walikuwa na Know How zote necessary kurun biz under very low cost and effective management structure. Walifanikiwa kila mahala kwenye kupata leseni lakini mgogoro ukawa kwamba issue yao ika vuja kwenye voda, then wakapewa channel au frequency ambazo wasingeweza kufanya chochote. Waka file lawsuit mahakamani, na mpaka leo kesi ipo hai.

Wengine walitoka Seattle, hawa niliongea nao mwenyewe 2008 walikuwa wanataka business developer in African market. A small company ambayo ina run kama Cricket, boost au simple mobile. They don't own mitambo wala nini, walipofika bongo wakutana na kikwazo kwamba wao ni kampuni fake. Ukweli kampuni hiyo ni popular Seattle, basi wakakwamia hapo.

Tanzania bado Vodacom inatawala sana nani aingie kwenye market na nani asiingie.
 
do u have communications with them,nipe deal niwasilianr nao.
True story nina rafiki wawili kwa wakati tofauti tofauti wamejaribu kuingia kwenye Telecommunication market ya Tanzania na mpaka sasa kesi zao ziko mahakamani.

Mmoja alifanya partnership ya 30% + 5% kwa kigogo na 65% ya non Tanzanian investor ambao walikuwa na Know How zote necessary kurun biz under very low cost and effective management structure. Walifanikiwa kila mahala kwenye kupata leseni lakini mgogoro ukawa kwamba issue yao ika vuja kwenye voda, then wakapewa channel au frequency ambazo wasingeweza kufanya chochote. Waka file lawsuit mahakamani, na mpaka leo kesi ipo hai.

Wengine walitoka Seattle, hawa niliongea nao mwenyewe 2008 walikuwa wanataka business developer in African market. A small company ambayo ina run kama Cricket, boost au simple mobile. They don't own mitambo wala nini, walipofika bongo wakutana na kikwazo kwamba wao ni kampuni fake. Ukweli kampuni hiyo ni popular Seattle, basi wakakwamia hapo.

Tanzania bado Vodacom inatawala sana nani aingie kwenye market na nani asiingie.
 
Mh kweli haya ni mawazo ya busara sana Je akitokea m tu mbaye anaweza kuanzisha kampuni inayodeal na minara tu ambayo atakuwa akikodisha kwa makampuni yoyote ya hizi simu unahisi kuna faida je kuna sheria zozote zinzoregulate?


Sheria ya Ku-regulate Ipo Especially ile mpya ya 2010(EPOCA) na ina - enforce Infrastructure Sharing kwa lengo la kupunguza mlundikano wa Minara ktk eneo moja vile vile kupunguza Gharama za uwekezaji ktk Mawasiliano. Wazo la kuanzisha kampuni inayo deal na Minara ni Zuri lakini linahitaji Mkakati mkubwa, Kwenye Sheria mpya mapendekezo ya Wadau yalikuwa ni kuziwezesha Halmashauri za Miji kujenga Minara na kuikodisha kwa operators na kuwa chanzo cha mapato kwa hizo halmashauri Tatizo ni kukosa utaalam na Fedha za kuwekeza. Gharama za mawasiliano zitashuja ikizingatiwa kuwa Mkongo wa Taifa(National Optical Fibre Network) unaoendelea kujengwa utafika Kila wilaya ya Nchi Hii, hivi sasa umeweza kuunganisha Nchi Jirani (Cross- boarder Links) kama vile Rwanda, Zambia, Kenya nk.
 
Back
Top Bottom