Lazima tutambue kwamba pamoja na matatizo yote ambayo yamekuwa yakiikabili IPTL, na vilevile pamoja na kwamba mitambo ya IPTL bado haijabadilishwa kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kutumia gesi, ukweli ni kwamba IPTL imekuwa inauza Umeme kwa bei ya chini kuliko wazalishaji wengine binafsi hapa nchini. Umeme wa IPTL unauzwa US$ 1.06 kwa unit moja ya umeme, ukilinagnisha na Songas US$ 4.31 au Symbion US$ 4.99 au Aggreko US$ 5.70. Ukweli huu ni tofauti kabisa na propaganda iliyoeneza uongo kwamba mradi wa Umeme wa IPTL ndiyo umekuwa ukiwanyonya watanzania kwa kutoza bei kubwa ya Umeme kwa TANESCO
Hivi Watanzania tunafahamu kwamba Muwekezaji Mzalendo katika ubia wa IPTL, Kampuni ya VIP ya Bw. James Rugemalira, ndiyo walianzisha vita ya kudai haki kwa niaba ya Watanzania dhidi ya wawekezaji wa nje, Mechmar na baadaye Benki ya Standard Charter, baada ya kugundua wamefanya udanganyifu kwenye gharama za uwekezaji na madeni, vile vile Mechmar walikataa kugundua mchango wa VIP kwenye uanzishwaji wa IPTL na kushirikiana na benki kuingiza madeni yasiyohalali kwenye vitabu vya hesabu vya IPTL. Vita hii VIP ilipigana kwa takriban miaka yote 20 ya uhai wa IPTL kwa kutumia nguvu na gharama kubwa. Kwa miaka yote 20, hadi VIP ilipouza hisa zake 3, ndiyo mara ya kwanza imefaidika na ubia wake katika mradi wa IPTL.
Lazima tutambue kwamba pamoja na matatizo yote ambayo yamekuwa yakiikabili IPTL, na vilevile pamoja na kwamba mitambo ya IPTL bado haijabadilishwa kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kutumia gesi, ukweli ni kwamba IPTL imekuwa inauza Umeme kwa bei ya chini kuliko wazalishaji wengine binafsi hapa nchini. Umeme wa IPTL unauzwa US$ 1.06 kwa unit moja ya umeme, ukilinagnisha na Songas US$ 4.31 au Symbion US$ 4.99 au Aggreko US$ 5.70. Ukweli huu ni tofauti kabisa na propaganda iliyoeneza uongo kwamba mradi wa Umeme wa IPTL ndiyo umekuwa ukiwanyonya watanzania kwa kutoza bei kubwa ya Umeme kwa TANESCO
Hivi toka lini Watanzania tumepoteza haki ya msingi, inayosema mtu hana hatia mpaka pale yule anayemshutumu aweze kudhibitisha kwamba ana hatia mbele ya mahakama? Lakini kwenye suala hili la IPTL, baadhi ya wabunge wetu walisimama bungeni na kuwahukumu watu mbalimbali waliopata misaada kutoka Kampuni ya VIP kwamba ni mafisadi na wakwepa kodi n.k., pasipo uthibitisho wowote wala fursa ya watuhumiwa kujitetea. Je, wao wanaweza kuweka rekodi za account zao wazi zikachambuliwa? Kila kukicha wanasiasa wanatoa na kupokea misaada ya kifedha na hakuna hata mmoja ana ripoti hiyo misaada kwenye Mamlaka husika. Ni dhahiri kwamba tatizo lingine tulilonalo hapa ni jamii kutokuzoea watu wa aina ya Mr. James Burchard Rugemalira ambao wana moyo wa kutoa kwa kiasi kikubwa na kwa uwazi pale wanapo amini mchango wao utakuwa unasaidia jamii au una maslahi ya kitaifa/umma.
Mbona unatetea kwa nguvu sana hawa wezi wenzako au na wewe mgao umekupitia nini sisi tunataka ccm warudishe pesa zetu za escrow na watuhumiwa wote wafikishwa mahakamani
humu hoja pesa ni za nani jibu limeshapatikana zilikuwa za umma .Sumu ya kina Zitto na washirika wake inaelekea imekuingia sana. Hata CAG mwenyewe amesita kutamka kwamba fedha zile ni za umma bali ni za IPTL baada ya Tanesco kutumia umeme wake. This issue has been blown out of proportion, tena kwa malengo mahsusi!