Hivi toka lini Watanzania tumepoteza haki ya msingi, inayosema mtu hana hatia mpaka pale yule anayemshutumu aweze kudhibitisha kwamba ana hatia mbele ya mahakama? Lakini kwenye suala hili la IPTL, baadhi ya wabunge wetu walisimama bungeni na kuwahukumu watu mbalimbali waliopata misaada kutoka Kampuni ya VIP kwamba ni mafisadi na wakwepa kodi n.k., pasipo uthibitisho wowote wala fursa ya watuhumiwa kujitetea.
Je, wao wanaweza kuweka rekodi za account zao wazi zikachambuliwa? Kila kukicha wanasiasa wanatoa na kupokea misaada ya kifedha na hakuna hata mmoja ana ripoti hiyo misaada kwenye Mamlaka husika. Ni dhahiri kwamba tatizo lingine tulilonalo hapa ni jamii kutokuzoea watu wa aina ya Mr. James Burchard Rugemalira ambao wana moyo wa kutoa kwa kiasi kikubwa na kwa uwazi pale wanapo amini mchango wao utakuwa unasaidia jamii au una maslahi ya kitaifa/umma.