Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
810
Matumaini yangu mmeamka salama wana JF

Bila kuchelewesha muda hapa nataka kumzungumzia Katibu Mwenezi wa Chama cha Ccm ndg/Mh P. Makonda.

Huyu Jamaa ni mtu sana nimekuja kumfuatilia siku moja kwenye mitandao na anavyoongea hapa CCM wamempata mtu kweli kweli.

Poul makonda ana sifa nyingi sana Huwezi Kuzielezea Zote Ukamaliza. CCM Wafungue Moyo bila kumuwekea roho ya kwanini baadhi yao huwa naona kabisa Hawakubaliani naye Kwa kitu anachokifanya Makonda.

Kutokana kwa sasa ndani ya Tz na nje ya Tz wanamzungumzia makonda huyu jamaa Mungu aendelee Kumueka kama mbegu ni mbegu Bora Zaidi.

Huyu jamaa ana kipawa sana(IQ) kubwa mno na huwa anajua Nini anafanya na nini afanye. Makonda Kaifanya vyama vya upinzani Vipoteane Tanzania husani CHADEMA na ACT WAZALENDO.

Huyuhuyu makonda Kamrudisha mh.raisi Kwenye uso Wa wananchi Wa Tanzania na Kuwajenga Kiimani Na kumkubali mh.samia suluhu.

Ombi Langu Kwa Wanaomzunguka Makonda;

Kama itawapendeza zaidi muendelee Kumpa nguvu kuliko kumtilia kinyongo na kumuwekea kiuzebe.

Wana CCM wote huyu makonda ni mtu kweli hii ni lulu ingawa binadamu tumeumbwa chuki na husda naombeni sana huyu Mh. P Makonda mfungulie moyo ili awanyooshe upinzani anachokifanya ni kitu kiliitajika sana kwa kipindi hichi kwa sasa.

Mwisho.
Ukweli ni kwamba mimi sio mwana CCM wala mwana CHADEMA kiujmla sichangamani na CHAMA chochote Ila kwenye Ukweli Siwezi kupepesa macho.

Makonda kwa Sasa ni bora sana. Kila la heri makonda,kila la heri katika Shughuli zako za kitaifa. MUNGU akupe maisha marefu wewe kwa sasa kama ni kiungo popote unacheza.

Ahsante.
 
Katika mwaka wa 2024 kutakuwa na uchaguzi mwingi zaidi wa kisiasa duniani kote kuliko mwaka mwingine wowote. Hata hivyo, watu wengi wameacha kuwaamini wanasiasa.

  • Katika uchunguzi uliofanywa nchini Marekani, watu wengi zaidi walisema kwamba “wanasiasa wengi wanaongozwa na sababu zenye ubinafsi” badala ya kuongozwa na tamaa ya kuwatumikia watu. a—Kituo cha Utafiti cha Pew, Septemba 19, 2023.
Vijana wengi pia hawawaamini wanasiasa.

  • “Leo matineja wengi wanapendezwa zaidi kupata suluhisho la matatizo muhimu, lakini uchunguzi unaonyesha kwamba wanasiasa hawatafuti suluhisho hilo.”—The New York Times, Januari 29, 2024.
  • “Uchunguzi mmoja ulionyesha kwamba vijana wanawaamini zaidi watu kwenye YouTube kuliko wanavyowaamini wanasiasa.”—The Korea Times, Januari 22, 2024.
Je, tunaweza kuamini kwamba wanasiasa watafanya mambo yawe mazuri wakati ujao?
 
Kuna yule mwamba atakuja aseme; Natumai utapata muongozo kiongozi. Sasa sijui Ni Muongozo Kuhusu huyo Bwana Makonda au Lah ila atakuja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom