Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,414
1,195
Hivi toka lini Watanzania tumepoteza haki ya msingi, inayosema mtu hana hatia mpaka pale yule anayemshutumu aweze kudhibitisha kwamba ana hatia mbele ya mahakama? Lakini kwenye suala hili la IPTL, baadhi ya wabunge wetu walisimama bungeni na kuwahukumu watu mbalimbali waliopata misaada kutoka Kampuni ya VIP kwamba ni mafisadi na wakwepa kodi n.k., pasipo uthibitisho wowote wala fursa ya watuhumiwa kujitetea.

Je, wao wanaweza kuweka rekodi za account zao wazi zikachambuliwa? Kila kukicha wanasiasa wanatoa na kupokea misaada ya kifedha na hakuna hata mmoja ana ripoti hiyo misaada kwenye Mamlaka husika. Ni dhahiri kwamba tatizo lingine tulilonalo hapa ni jamii kutokuzoea watu wa aina ya Mr. James Burchard Rugemalira ambao wana moyo wa kutoa kwa kiasi kikubwa na kwa uwazi pale wanapo amini mchango wao utakuwa unasaidia jamii au una maslahi ya kitaifa/umma.
 
ulelema

Member
Dec 5, 2014
6
0
Ni kweli, huyo bwana ni miongoni mwa wazalendo wanaowawezesha sana watanzania wegine kupitia misaada ya kijamii. Ni vema wanaomtuhumu wakafuatilia historia yake kwani watagundua kwamba amewasaidia watu wengi sana, hasa pale anapogundua kwamba misaada ile inalenga kuendeleza jamii. Si haki kumdhihaki mzalendo wa aina hii pale anapojitoa kwa ajili ya wengine.
 
Maduhu2

Member
Mar 10, 2012
25
45
Tatizo kubwa la wanasiasa wetu huwa wanakurupuka bila kufanya tafiti.Hata Waziri anayejiita msomi wa daraja la kwanza anasema peza hizo ni chafu.Wakaiti huohuo ansema waliopewa na Rugemalira walipe kodi.Sheria za Kodi pesa Chafu huwa haitozwi Kodi(Je huyo waziri alikuwa anamanisha nini) au ndio ASHIKI Majumuni!
PAC wanasema mitambo itaifishwe,kutoka kwa nani? Wametuambia PAP ni kampuni feki.Masikini wabunge wetu wamedandia hoja bila ufikili kube Zito na wenzake walikuwa wanatetea Maslahi ya Nje.
 
Hongasuta

Member
Sep 10, 2006
81
0
Hivi Watanzania tunafahamu kwamba Muwekezaji Mzalendo katika ubia wa IPTL, Kampuni ya VIP ya Bw. James Rugemalira, ndiyo walianzisha vita ya kudai haki kwa niaba ya Watanzania dhidi ya wawekezaji wa nje, Mechmar na baadaye Benki ya Standard Charter, baada ya kugundua wamefanya udanganyifu kwenye gharama za uwekezaji na madeni, vile vile Mechmar walikataa kugundua mchango wa VIP kwenye uanzishwaji wa IPTL na kushirikiana na benki kuingiza madeni yasiyohalali kwenye vitabu vya hesabu vya IPTL. Vita hii VIP ilipigana kwa takriban miaka yote 20 ya uhai wa IPTL kwa kutumia nguvu na gharama kubwa. Kwa miaka yote 20, hadi VIP ilipouza hisa zake 3, ndiyo mara ya kwanza imefaidika na ubia wake katika mradi wa IPTL.
 
Hongasuta

Member
Sep 10, 2006
81
0
Lazima tutambue kwamba pamoja na matatizo yote ambayo yamekuwa yakiikabili IPTL, na vilevile pamoja na kwamba mitambo ya IPTL bado haijabadilishwa kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kutumia gesi, ukweli ni kwamba IPTL imekuwa inauza Umeme kwa bei ya chini kuliko wazalishaji wengine binafsi hapa nchini. Umeme wa IPTL unauzwa US$ 1.06 kwa unit moja ya umeme, ukilinagnisha na Songas US$ 4.31 au Symbion US$ 4.99 au Aggreko US$ 5.70. Ukweli huu ni tofauti kabisa na propaganda iliyoeneza uongo kwamba mradi wa Umeme wa IPTL ndiyo umekuwa ukiwanyonya watanzania kwa kutoza bei kubwa ya Umeme kwa TANESCO
 
Maduhu2

Member
Mar 10, 2012
25
45
Historia inatuambia Huyu Bwana Rugemalira ndiye wa kwanza kuwaambia Tanesco hapa tunaibiwa,Myaka yote anatetea haki yake leo kapata tunaaza kuhoji.

Hivi Rugemalira akitoa misaada kwa jamii shida lakini misaada hiyo ikitolewa na wenzetu tunaona ni sawa.Hata vyama vya siasa/Wabunge wanapokea misaada mingi lakini hawajawhi kusema ku declare wamepata kiasi gani.!

Vyama vinapata misaada kutoka Ujerumani inaonekana ni sawa lakini akitoa Mtanzania Mwezetu liwe Tatizo.(Ukoloni Mambo leo umetawala.
 
Maduhu2

Member
Mar 10, 2012
25
45
Lazima tutambue kwamba pamoja na matatizo yote ambayo yamekuwa yakiikabili IPTL, na vilevile pamoja na kwamba mitambo ya IPTL bado haijabadilishwa kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kutumia gesi, ukweli ni kwamba IPTL imekuwa inauza Umeme kwa bei ya chini kuliko wazalishaji wengine binafsi hapa nchini. Umeme wa IPTL unauzwa US$ 1.06 kwa unit moja ya umeme, ukilinagnisha na Songas US$ 4.31 au Symbion US$ 4.99 au Aggreko US$ 5.70. Ukweli huu ni tofauti kabisa na propaganda iliyoeneza uongo kwamba mradi wa Umeme wa IPTL ndiyo umekuwa ukiwanyonya watanzania kwa kutoza bei kubwa ya Umeme kwa TANESCO
Kama ndio hivyo IPTL lazima apigwe vita pande zote,Haya Makampuni ya kigeni hayatakubali IPTL iuze umeme kwa bei chini.Watanzania kwa nini hizi habari hawaambiwi?
 
mangaukawa

Senior Member
Dec 5, 2014
153
170
Tumeingia kwenye mtego wa mabeberu! Hivi mnajua kwamba adui yetu mkubwa kwenye mradi huu wa IPTL sio kampuni ya kizalendo ya VIP, bali ni Benki ya Standard Chartered Bank Hong Kong, ambayo imekuwa ikijaribu kujiingiza kijanjajanja kama mdai wa IPTL, ili waendelee kuwanyonya Watanzania? Benki hii ya Standard Charted imekuwa moja ya kizuizi kikubwa kwenye kubadilisha mitambo ya Umeme kutoka matumizi ya mafuta mazito ambayo ni aghali kwenda kwenye matumizi ya gesi ambayo ingeleta unafuu mkubwa kwenye bei ya Umeme kwa mwananchi. Vilevile Benki hii imekataa kufuata masharti, taratibu na sheria za nchini kwetu kwenye kudai hicho wanachosema ni haki yao. Badala yake wametangaza Duniani kote kwamba Serikali na Mahakama zetu haziaminiki.
 
NCHI YANGU TZ

JF-Expert Member
Sep 13, 2014
663
0
Hivi Watanzania tunafahamu kwamba Muwekezaji Mzalendo katika ubia wa IPTL, Kampuni ya VIP ya Bw. James Rugemalira, ndiyo walianzisha vita ya kudai haki kwa niaba ya Watanzania dhidi ya wawekezaji wa nje, Mechmar na baadaye Benki ya Standard Charter, baada ya kugundua wamefanya udanganyifu kwenye gharama za uwekezaji na madeni, vile vile Mechmar walikataa kugundua mchango wa VIP kwenye uanzishwaji wa IPTL na kushirikiana na benki kuingiza madeni yasiyohalali kwenye vitabu vya hesabu vya IPTL. Vita hii VIP ilipigana kwa takriban miaka yote 20 ya uhai wa IPTL kwa kutumia nguvu na gharama kubwa. Kwa miaka yote 20, hadi VIP ilipouza hisa zake 3, ndiyo mara ya kwanza imefaidika na ubia wake katika mradi wa IPTL.

mnapotosha mada hakuna mwenye ugomvi JR, tatizo linalotokea mpaka JR anaongelewa ni kuwa kampuni iliyonunua IPTL AMBAYO JR na alikuwa mbia haikuwa na PESA. kwaiyo pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya IPTL( ESCROW) ndizo zilipotolewa zilitumika kumlipa bwana JR kwaiyo hata kama ni wewe lazima uhoji kulikoni kwani kama ni hivyo hata JR angeweza kutumia hizohizo fedha kuinunua IPTL, MANUNUZI YA MITAMBO HIYO YAMEKAA kimagumashi.fedha zilitolewa dec kwa PAP, JR akalipwa january kifupi alinunuliwa kwa pesa yake mwenyewe, je hiyo inakuingia akilini?
 
Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,910
2,000
Mbona unatetea kwa nguvu sana hawa wezi wenzako au na wewe mgao umekupitia nini sisi tunataka ccm warudishe pesa zetu za escrow na watuhumiwa wote wafikishwa mahakamani
 
Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,832
2,000
Lazima tutambue kwamba pamoja na matatizo yote ambayo yamekuwa yakiikabili IPTL, na vilevile pamoja na kwamba mitambo ya IPTL bado haijabadilishwa kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kutumia gesi, ukweli ni kwamba IPTL imekuwa inauza Umeme kwa bei ya chini kuliko wazalishaji wengine binafsi hapa nchini. Umeme wa IPTL unauzwa US$ 1.06 kwa unit moja ya umeme, ukilinagnisha na Songas US$ 4.31 au Symbion US$ 4.99 au Aggreko US$ 5.70. Ukweli huu ni tofauti kabisa na propaganda iliyoeneza uongo kwamba mradi wa Umeme wa IPTL ndiyo umekuwa ukiwanyonya watanzania kwa kutoza bei kubwa ya Umeme kwa TANESCO
Ya kweli haya mkuu....!? ni dola 1.06 au ni senti!
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,542
2,000
Hakuna Mnyamwezi alifaidika. Wahaya Kibao walilamba vi-Ruge. Remember, 1Ruge = 40.4m.
 
Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,593
2,000
Tena kwa faida yako na waliokutuma, usije kutamka haya maneno mbele ya watu wanakuona. Utakuja kujuta kwa kuwaona wananchi wenye hasira huwa wanakuwaje wanapomkamata mwizi kama wewe na wenzako unaowatumikia.Hivi toka lini Watanzania tumepoteza haki ya msingi, inayosema mtu hana hatia mpaka pale yule anayemshutumu aweze kudhibitisha kwamba ana hatia mbele ya mahakama? Lakini kwenye suala hili la IPTL, baadhi ya wabunge wetu walisimama bungeni na kuwahukumu watu mbalimbali waliopata misaada kutoka Kampuni ya VIP kwamba ni mafisadi na wakwepa kodi n.k., pasipo uthibitisho wowote wala fursa ya watuhumiwa kujitetea. Je, wao wanaweza kuweka rekodi za account zao wazi zikachambuliwa? Kila kukicha wanasiasa wanatoa na kupokea misaada ya kifedha na hakuna hata mmoja ana ripoti hiyo misaada kwenye Mamlaka husika. Ni dhahiri kwamba tatizo lingine tulilonalo hapa ni jamii kutokuzoea watu wa aina ya Mr. James Burchard Rugemalira ambao wana moyo wa kutoa kwa kiasi kikubwa na kwa uwazi pale wanapo amini mchango wao utakuwa unasaidia jamii au una maslahi ya kitaifa/umma.
 
mandy2013

Senior Member
Sep 7, 2013
150
225
jamaa anatoa kweli misaada,ila hasaidii masikini kwa kuwa hzo pesa anaingiza kwenye account za wa2 binafsi, asaidie shule za kata, shule za msingi watoto wanakaa chini, mahospitalini hakuna dawa hakuna vtanda. naamin ule mgao wa 1.6 bil,40.4 mil, 80 mil. ungepelekwa ktk sehemu nilizotaja hapo juu ningekubali kuwa jamaa anasaidia masikin lkn kwa sasa acha nikubali jamaa anasaidia MATAJIRI. ahsanteni.
 
mangaukawa

Senior Member
Dec 5, 2014
153
170
Mbona unatetea kwa nguvu sana hawa wezi wenzako au na wewe mgao umekupitia nini sisi tunataka ccm warudishe pesa zetu za escrow na watuhumiwa wote wafikishwa mahakamani
Sumu ya kina Zitto na washirika wake inaelekea imekuingia sana. Hata CAG mwenyewe amesita kutamka kwamba fedha zile ni za umma bali ni za IPTL baada ya Tanesco kutumia umeme wake. This issue has been blown out of proportion, tena kwa malengo mahsusi!
 
Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,910
2,000
Sumu ya kina Zitto na washirika wake inaelekea imekuingia sana. Hata CAG mwenyewe amesita kutamka kwamba fedha zile ni za umma bali ni za IPTL baada ya Tanesco kutumia umeme wake. This issue has been blown out of proportion, tena kwa malengo mahsusi!
humu hoja pesa ni za nani jibu limeshapatikana zilikuwa za umma .
 
Maduhu2

Member
Mar 10, 2012
25
45
Tabby unatatizo kidogo,
Jiulize haya Masawali kuhusu report ya Mwakyembe iliyomgoa Waziri Mkuu Lowasa
1.Mwakembe alisema Richmond ilikuwa ni Kampuni Feki ambayo haikusajiliwa sehemu yoyote Duniani.Je ilikuwa kweli?
2.Je umejiuliza kama Richmond ilikuwa feki Symbion ameinunua Richmond kutoka Kwa Nani?
3.Je waziri wa Mambo ya nje wa Marekani alipokuja kuzindua hiyo mitambo Richmond/Symbion alizindua kitu feki-Wamarekani ni wa hovyo wanaweza kufanya Biashara na Kampuni Feki.
3.Je Hiyo Symbion kama alimnunua Richmond ni kiasi gani cha Pesa alitoa?
5.Je Serikali ilipata Kodi Kiasi gani kutokana na Hayo Mauzo?
Ukiweza kupata majibu ya haya maswali ndio unaweza kutambua watanzania tunavyobuluzwa na Mataifa ya Nje.Wametuvuruga kupitia wanasiasa mpaka Serikali ikakubali Tukampoteza Waziri wetu Mkuu Lowasa,Mataifa ya Magharibi yakachukua Mitambo kirahisi.Na sasa wantuuzia umeme kutoka kwenye Mitambo yetu wenyewe tuliyoikataa.

Kwa style hiyo hiyo wanataka kuichukua IPTL kwa kupitia Wanasiasa Uchwara.
 
Nasolwa

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,829
1,225
Jamani tuvute subra tusubiri maamuzi ya JK baada ya uchunguzi wake kukamilika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom