Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni; Bravo JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni; Bravo JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundamilia07, Sep 1, 2008.

 1. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni vema tukampongeza Mh Kikwete kwa jinsi ambavyo amelishughulikia suala la EPA. Vyovyote iwavyo, ameonesha ni kiongozi imara na makini katika kutatua issues. Kula tano Mr President.

  IMF chief backs Kikwete on EPA
  Correspondent in Washington
  Daily News; Sunday,August 31, 2008 @18:01


  The International Monetary Fund (IMF) has supported the government for measures taken in dealing with over 133bn/- embezzlement of Bank of Tanzania (BoT) External Payment Account (EPA). The IMF Managing Director, Mr Dominique Strauss-Khan, lauded the government in dealing with the EPA scam during talks with President Jakaya Kikwete at the Omni Shoreham Hotel here over the weekend.

  The scandal involved fraudulent payment of about 133bn/- made by BoT to 22 firms in the 2005/06 financial year, involving the repayment of the country’s external debt. The scam claimed the then Governor of BoT, Dr Daudi Ballali, who died in the US a few months later, as its first casualty. Dr Ballali was fired by President Kikwete in January, this year, after he was implicated in investigative reports carried out by the Controller and Auditor General (CAG) and an international accounting and audit firm, Ernest & Young.

  Mr Strauss-Khan said his organization had confidence in President Kikwete’s leadership and expected that all pending issues in the EPA saga would be effectively concluded. President Kikwete met the IMF Managing Director on his last day of three day state visit to the United States at the invitation of President George W. Bush. President Kikwete briefed the IMF chief details of the EPA scam and measures taken by the government, including recovery of some funds.

  “We’re greatly satisfied and congratulating you for the way you handled the issue. “This thing can happen anywhere in the world. What is important is the way it is being handled. And you have handled it very well, with competence and professionalism of the highest order,” Mr Strauss-Kahn noted. The IMF Managing Director said most countries had faced similar problems, but none managed to recover such huge sums of money.

  “The EPA case is now closed in as far as IMF is concerned,” stressed the IMF Managing Director. He promised to assist Tanzania in putting in place water-tight systems to avoid such incidents in future. President Kikwete promised the IMF chief that he would not be ready to see such a thing (EPA scam) happening again in Tanzania. President Kikwete also said that the task now was to rebuild the image of Tanzania’s central bank, saying such institutions were sensitive and of crucial importance to the country.

  The IMF praises came a week after President Kikwete explained in detail in Parliament how the government handled the EPA scam. The president told the legislators on August 21 that owners of firms involved in the scandal had their passports seized and property confiscated. He said suspects in the EPA account embezzlement scandal who fail to return the looted funds by October 31 this year, will face criminal prosecution.

  The president, however, did not specify whether or not the government has offered some form of amnesty deal for those EPA scandal suspects who do return the looted funds. President Kikwete declared that the government will take custody of the recovered EPA funds and use them to finance an expanded fertilizer subsidy programme for the agricultural sector. He said part of the recovered EPA monies will furthermore be channelled towards re-capitalizing the state-owned Tanzania Investment Bank (TIB), to start offering loans to farmers
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  hatujaona matokeo.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sijaona sababu yoyote ya kumpongeza rais kwa mazingaombwe.
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  'Hatujaona matokeo' kichuguu ni wewe na nani ambao hamjaona?
   
 5. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  'Mazingaombwe?' hii kali sasa, nafikiri hata wale 'maprofesa' wa abrakadabra will admire your commets!
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mimi na familia yangu hatujaona matokeo yoyote ya serikali dhidi ya wizi wa EPA; ndiyo maana tunalalamikia hii kashfa ya EPA. Jeetu Patel yuko nje ya nchi akiendelea kutesa huku yeye ndiye aliyechukua karibu asilimia themanini ya pesa zile za EPA. Kikwete kamfanyia nini?

  Wakati ile document iliyohusu EPA ilipoanza kuzunguka hapa JF, serikali ilisema huo ni uwongo. Baada ya Wakaguzi kuthibitisha wizi huo, leo hii serikali inapiga danadana tu kujaribu kutushahulisha na kashafa ile.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,206
  Trophy Points: 280
  Wasiopenda maendeleo ya nchi yetu utawajua tu kwa kutaka kusifia 'juhudi' ambazo Watanzania wengi hatuzioni. Watapiga makofi, vigelegele na hata kuandamana ili kumsifia kiongozi ambaye hajafanya lolote lile kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni zake. Mungu atawasaidia labda nao wafunue macho waone kwamba hao viongozi wanaowasifia hawahitaji hata sentensi ya mstari mmoja ya kuwapongeza.
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kazi ya Rais kwenye suala hili la EPA tumeiona na sina sababu ya kuibeza hata kidogo. Wote tuliopata nafasi ya kusikiliza/kusoma hotuba yake tunakubali kuwa ametoa muda kwa kamati maalum ya akina Mwanyika na wenzake kuendelea kukamilisha baadhi ya mambo yaliyobaki. Vilevile ni wazi kuwa hatuwezi kusomewa ripoti nzima ya akina Mwanyika kwani huenda kuna mapendekezo mengine kwa sababu maalum hayawezi kutolewa kwenye public kwani yanaweza kuathiri mwenendo mzima wa kukamilisha yale yanayotarijiwa. Kwa hiyo issue ya Jeetu Patel siyo issue ya kumuinua Rais aende akamtafute, waachie akina Mwanyika na Mwema wao ndiyo wanajua how to implement. Sasa kama unataka Rais aende akamsake Jeetu hapo nadhani unataka kusherehesha tu.
  Bado ninasisitiza kuwa JK anastahili pongezi zangu kwa hatua alizochukua kutatua suala la EPA.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kichuguu,
  Niongeze na mimi kwenye kundi la wale ambao hawajaona matokeo yeyote ya utendaji wa serikali katika suala la EPA. Utasifiaje kitu ambacho hakisifiki?
   
 10. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Bubu ataka kusema,
  Wewe siyo msemaji wa 'Watanzania wengi' hizo zako ni hisia tu na ambazo hazijengi hoja ya nguvu katika majadliano. Ukweli unabaki kuwa JK amefanya kazi yake vizuri na anastahili pongezi kwa hilo. Tatizo ambalo amelitatua ni tatizo la nchi na wala siyo tatizo lake binafsi. Huenda wale ambao haitakii mema nchi yetu walitaka kuona kuwa suala EPA haliishi na liendelee kuwa ni ajenda kila kukicha, tutafika kweli? JK is smart and Intelligent!
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,206
  Trophy Points: 280
  Ama kweli kikulacho kinguoni mwako!!!
   
 12. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  You need to go and see optician.
   
 13. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Toa hoja wacha mafumbo!
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Je wewe ndiye msemaji wa watanzania wengi? Mbona uko biased kwenye kumsifia rais namna hiyo? Umefanya kazi yako ya kutushawishi tumsifie Kikwete, lakini tumekuambia kuwa hatujaona lolote aliolofanya la kutufanya tumsifie; kwa nini yasiishie hapo? Badala yake unajaribu kutulazimisha kukubaliana na wewe. Twambie nani aliyekamatwa na kushughulikiwa kisheria kutokana na wizi huo wa EPA. Hapa Tanzania, watu wanafungwa kwa kukutwa na picha zao wenyewe walizopiga wakiwa uchi, inakuwaje walioiba mapesa ya umma waachiwe huru halafu wewe unatutaka tukubali kuwa Rais kafanya kazi yake kweli? Unakumbuka yule mtu aliyefungwa mwaka mmoja jela kwa kuiba kuku?
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,206
  Trophy Points: 280
  Kuna hoja yoyote ambayo wewe unaweza kuielewa!!! Umekuwa mwanachama hapa JF kwa muda mrefu tu sasa, ungekuwa unafuatilia yanayoandikwa na kujadiliwa kuhusu EPA basi usingepoteza muda wako kutoa pongezi ambazo hazistahili.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  kichuguu,

  Niongezeni na mimi humo kundini kwa sababu naamini sifa haitolewi hovyo kama karanga halafu eti kwa asiyestahili kama JK. Anayethubutu kufanya hivyo siyo tu anajishushia hadhi mwenyewe bali analishushia hadhi neno sifa. How sad!!
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sijadiliani hapa kwenye forum kwa kutumia hisia, kwahiyo sijadai kuwa ni msemaji wa watanzania walio wengi, zaidi ya hapo siwezi pia kuwa msemaji wa familia yangu katika suala la EPA.
  Sitakushawishi wala kukulazimisha umsifie Mh Rais kwani hiyo siyo kazi yangu. Mimi nipo hapa kujieleza yale ambayo ninaamini ni ya kweli na hata taasisi na watu wengi wameona kama nilivyoona mimi.
   
 18. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hebu soma tena ulichokiandika, nimeshindwa kukuelewa kama ulikuwa unataka kuuliza swali au unashagaa!.
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni kawaida hata kwenye msafara wa mamba na makenge huwa wamo ndani yake. Lete hoja na si vinginevyo.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,206
  Trophy Points: 280
  Lini nilikwambia kwamba mimi ni msemaji wa Watanzania!!? :confused:
  Kufanya kazi nzuri kwa kuwapigia magoti wezi wa mabilioni ya shilingi na kuwaomba kwa kuwabembeleza warudishe mapesa hayo huku waiendelea kupeta uraiani!!? :confused:
  Nadhani umeshasikia polisi wakitamka kuhusiana na wizi wa pesa ndogo tu ukilinganisha na mabilioni ya EPA kwamba, "kutokana na unyeti wa kesi hii watuhumiwa wataendelea kuwekwa rumande huku wakisaidia polisi katika uchungizi wao" kulikoni katika wizi wa EPA wahusika bado wanapeta mtaani? au kwa kuwa ni matajiri wakubwa wakiguswa basi nchi itawaka moto!!!!:confused:

  Kama wewe unaona wizi wa EPA wa shilingi kati ya bilioni 300 na trilioni moja ni kitu kidogo ambacho Watanzania inabidi tuachane nacho basi kweli huitakii Tanzania mema, bali unataka kuwaona mafisadi na viongozi wasiostahili kuwepo madarakani wakiendelea kuiangamiza Tanzania. Mwaka mmoja tu 2005/2006 EPA zimeibiwa shilingi 133 bilioni na meremeta 155 bilioni. Kama ukaguzi ungeruhusiwa ufanyike tangi 1998 wakati Ballali alipoingia BoT si ajabu wizi huo ungefika shilingi Trillioni moja au zaidi, lakini wewe unaona kujadili hili la wizi wa EPA ni kupoteza muda na tuendelee na kuganga yajayo, AMA KWELI UNAITAKIA MEMA TANZANIA. Kwenye chama chenu cha mafisadi wengi wenu bado mnaona hivyo kuhusu JK, lakini Watanzania wengi tumeshastuka siku nyingi tu.
   
Loading...