Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni; Bravo JK

Sijadiliani hapa kwenye forum kwa kutumia hisia, kwahiyo sijadai kuwa ni msemaji wa watanzania walio wengi, zaidi ya hapo siwezi pia kuwa msemaji wa familia yangu katika suala la EPA.
Sitakushawishi wala kukulazimisha umsifie Mh Rais kwani hiyo siyo kazi yangu. Mimi nipo hapa kujieleza yale ambayo ninaamini ni ya kweli na hata taasisi na watu wengi wameona kama nilivyoona mimi.

hujaona upungufu ulionao katika hii mada uliyoanzisha mwenyewe? mimi situmii hisia bali ninataka kujua waliohusika na wizi wa EPA wamechukuliwa hatua zipi za kisheria. Nchi hii inaendeshwa kwa sheria siyo kwa longo longo nyingie yoyote ile, na serikali ndiye msimamizi mkubwa wa sheria. Kama wewe unajitenga na familia yako katika mambo ya kitaifa basi wengine tunashirikiana na familia zetu.
 
Zidumu fikra za Mwenyekiti wa chama cha mafisadi JK, zidumu! :( :(:(
 
Lini nilikwambia kwamba mimi ni msemaji wa Watanzania!!? :confused:
Kufanya kazi nzuri kwa kuwapigia magoti wezi wa mabilioni ya shilingi na kuwaomba kwa kuwabembeleza warudishe mapesa hayo huku waiendelea kupeta uraiani!!? :confused:
Nadhani umeshasikia polisi wakitamka kuhusiana na wizi wa pesa ndogo tu ukilinganisha na mabilioni ya EPA kwamba, "kutokana na unyeti wa kesi hii watuhumiwa wataendelea kuwekwa rumande huku wakisaidia polisi katika uchungizi wao" kulikoni katika wizi wa EPA wahusika bado wanapeta mtaani? au kwa kuwa ni matajiri wakubwa wakiguswa basi nchi itawaka moto!!!!:confused:

Kama wewe unaona wizi wa EPA wa shilingi kati ya bilioni 300 na trilioni moja ni kitu kidogo ambacho Watanzania inabidi tuachane nacho basi kweli huitakii Tanzania mema, bali unataka kuwaona mafisadi na viongozi wasiostahili kuwepo madarakani wakiendelea kuiangamiza Tanzania. Mwaka mmoja tu 2005/2006 EPA zimeibiwa shilingi 133 bilioni na meremeta 155 bilioni. Kama ukaguzi ungeruhusiwa ufanyike tangi 1998 wakati Ballali alipoingia BoT si ajabu wizi huo ungefika shilingi Trillioni moja au zaidi, lakini wewe unaona kujadili hili la wizi wa EPA ni kupoteza muda na tuendelee na kuganga yajayo, AMA KWELI UNAITAKIA MEMA TANZANIA. Kwenye chama chenu cha mafisadi wengi wenu bado mnaona hivyo kuhusu JK, lakini Watanzania wengi tumeshastuka siku nyingi tu.

Sina haja ya kuandikia mate wakati wino upo. Nimekopi hii thread yako uliyoitundika muda si mrefu, kama ulisahau ulichokiandika basi ninakurudishia uiosome tena

Wasiopenda maendeleo ya nchi yetu utawajua tu kwa kutaka kusifia 'juhudi' ambazo Watanzania wengi hatuzioni. Watapiga makofi, vigelegele na hata kuandamana ili kumsifia kiongozi ambaye hajafanya lolote lile kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni zake. Mungu atawasaidia labda nao wafunue macho waone kwamba hao viongozi wanaowasifia hawahitaji hata sentensi ya mstari mmoja ya kuwapongeza.
 
hujaona upungufu ulionao katika hii mada uliyoanzisha mwenyewe? mimi situmii hisia bali ninataka kujua waliohusika na wizi wa EPA wamechukuliwa hatua zipi za kisheria. Nchi hii inaendeshwa kwa sheria siyo kwa longo longo nyingie yoyote ile, na serikali ndiye msimamizi mkubwa wa sheria. Kama wewe unajitenga na familia yako katika mambo ya kitaifa basi wengine tunashirikiana na familia zetu.

Mada iko sawasawa, tatizo lako ni wewe ambaye umekiri huoni hatua ambazo ni muhimu zilizofikiwa hadi sasa juu ya EPA.

Read between the lines, 'siwezi pia kuwa msemaji wa familia yangu katika suala la EPA.' Familia yangu iko huru kifikra.
 
Sina haja ya kuandikia mate wakati wino upo. Nimekopi hii thread yako uliyoitundika muda si mrefu, kama ulisahau ulichokiandika basi ninakurudishia uiosome tena

Wasiopenda maendeleo ya nchi yetu utawajua tu kwa kutaka kusifia 'juhudi' ambazo Watanzania wengi hatuzioni. Watapiga makofi, vigelegele na hata kuandamana ili kumsifia kiongozi ambaye hajafanya lolote lile kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni zake. Mungu atawasaidia labda nao wafunue macho waone kwamba hao viongozi wanaowasifia hawahitaji hata sentensi ya mstari mmoja ya kuwapongeza.

1. Ahadi za kupitia mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania zilikuwa nyingi mno wakati wa kampeni, kilichofanyika hadi hii leo unakijua au kwa kukumbusha tu ni sifuri, zero, ZILCH.

2.Ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania hakuna chochote, bali tunachokiona ni ahadi za maisha bora kwa kila fisadi.

3. Fisadi Mkapa kakupua Kiwira mchana kweupe mgodi ambao unathamani ya shilingi bilioni 4. Amejiuzia kwa shilingi milioni 700, lakini kalipa shilingi 70 milioni tu. Juhudi zetu Watanzania kuhakikisha mgodi huu unarudishwa chini ya miliki ya Watanzania hadi hivi sasa zimegonga ukuta. "Viongozi" wanajifanya kama hawaelewi yale tunayoyazungumza.

4. Ahadi za ari mpya, nguvu na kazi mpya hatuoni chochote bali midebwedo tu kila kukicha, usanii na uVDG.

5. Ufisadi wa rada, mpaka leo hii Watanzania tuko gizani kuhusiana na pesa zetu shilingi bilioni 12 walizolipana mafisadi katika ununuzi wa rada hiyo akiwemo mzee wa vijisenti aliyekuwa na vijisenti katika bank account ya nje ya nchi.

6. Kwa kifupi hakuna chochote kilichofanywa ambacho kinamhamasisha Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania kumpigia kura JK, lakini kwenye chama cha mafisadi bado huyu ni mwenzenu anayestahili kuchaguliwa tena 2010 na si ajabu hata kubadilisha katiba ili aendelee kuwepo madarakani mpaka 2025!!! Halafu mnadai mna mapenzi ya kweli na Tanzania pamoja na kuona nchi inaangamia!!!!! kumbe mnatumia madaraka yenu kujitajirisha na kuwalinda mafisadi wenzenu!!!!
 
1. Ahadi za kupitia mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania zilikuwa nyingi mno wakati wa kampeni, kilichofanyika hadi hii leo unakijua.

2.Ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania hakuna chochote, bali tunachokiona ni ahadi za maisha bora kwa kila fisadi.

3. Fisadi Mkapa kakupua Kiwira mchana kweupe mgodi ambao unathamani ya shilingi bilioni 4. Amejiuzia kwa shilingi milioni 700, lakini kalipa shilingi 70 milioni tu. Juhudi zetu Watanzania kuhakikisha mgodi huu unarudishwa chini ya miliki ya Watanzania hadi hivi sasa zimegonga ukuta. "Viongozi" wanajifanya kama hawaelewi yale tunayoyazungumza.

4. Ahadi za ari mpya, nguvu na kazi mpya hatuoni chochote bali midebwedo tu kila kukicha, usanii na uVDG.

5. Ufisadi wa rada, mpaka leo hii Watanzania tuko gizani kuhusiana na pesa zetu shilingi bilioni 12 walizolipana mafisadi katika ununuzi wa rada hiyo akiwemo mzee wa vijisenti aliyekuwa na vijisenti katika bank account ya nje ya nchi.

6. Kwa kifupi hakuna chochote kilichofanywa ambacho kinamhamasisha Mtanzania yeyote yule mwenye mapenzi ya kweli na Tanzania kumpigia kura JK, lakini kwenye chama cha mafisadi bado huyu ni mwenzenu anayestahili kuchaguliwa tena 2010 na si ajabu hata kubadilisha katiba ili aendelee kuwepo madarakani mpaka 2025!!! Halafu mnadai mna mapenzi ya kweli na Tanzania pamoja na kuona nchi inaangamia!!!!! kumbe mnatumia madaraka yenu kujitajirisha na kuwalinda mafisadi wenzenu!!!!

Kila nchi ina matatizo yake na yanatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Jambo kubwa hapa ni umahiri wa kiongozi uliye nae juu wa uwezo wake wa kutatua matatizo hayo yaliopo. Mimi na wale wengine wanaoangalia utendaji wa Mh Rais hasa katika suala la EPA ni ushahidi tosha kuwa Rais amefanikiwa katika ku-handle hii issue kama kiongozi wa kitaifa. Ninafahamu kuwa si wote ambao mnaweza kuukubali ukweli huu, vilevile mko huru kuukata kwa kutegemea what you put before your eyes and minds.
 
Acha usanii wako!!! eti JK ana umahiri wa kutatua matatizo yaliyopo!! Labda kawadanganye hili wanachama wenzako katika chama chenu cha mafisadi, lakini Watanzania tulio wengi tumeshagundua kwamba hatuna uongozi jasiri wa kupambana na mafisadi, kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania walio wengi na pia kuhakikisha kwamba rasilimali mbali mbali tulizojaliwa Tanzania zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha maendeleo yetu, katika miaka 5 toka 2001 mpaka 2006 Dhahabu iliyochimbwa Tanzania na makampuni ya wageni ilikuwa na thamani ya $2.6 Billion lakini tulichoambulia Watanzania ni $78 million tu sawa na asilimia 3 tu wakati wageni wamepeleka kwao 97%!!!!! na JK haoni kasoro yoyote kwenye hili!!! Tunachokiona ni usanii tu na uwezo finyu, wewe unakiita ni umahiri!!! Ama kweli ukipenda, chongo utaita kengeza!!! Endeleeni kuzugwa na umahiri wa JK katika kupambana na matatizo ya Tanzania, lakini mjue kwamba kwenye ukweli, siku zote uwongo hujitenga.
 
...........ukiona watu wanatafuta kusifiwa na majirani wakati watoto nyumbani wamenuna..ni walevi....mlevi hufanya lolote ili apate pombe...na akilewa huanza kusifu au kusifiana....hata kupenda sifa ni ulevi....NOTHING TO BE PROUD OF ....

SCREW MUUNGWANA!!!!
 
Acha usanii wako!!! eti JK ana umahiri wa kutatua matatizo yaliyopo!! Labda kawadanganye hili wanachama wenzako katika chama chenu cha mafisadi, lakini Watanzania tulio wengi tumeshagundua kwamba hatuna uongozi jasiri wa kupambana na mafisadi, kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania walio wengi na pia kuhakikisha kwamba rasilimali mbali mbali tulizojaliwa Tanzania zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuharakisha maendeleo yetu, katika miaka 5 toka 2001 mpaka 2006 Dhahabu iliyochimbwa Tanzania na makampuni ya wageni ilikuwa na thamani ya $2.6 Billion lakini tulichoambulia Watanzania ni $78 million tu!!!!! na JK haoni kasoro yoyote kwenye hili!!! Tunachokiona ni usanii tu na uwezo finyu, wewe unakiita ni umahiri!!! Ama kweli ukipenda, chongo utaita kengeza!!! Endeleeni kuzugwa na umahiri wa JK katika kupambana na matatizo ya Tanzania, lakini mjue kwamba kwenye ukweli, siku zote uwongo hujitenga.

Bahati mbaya sijawahi kukisikia hata siku moja chama kinachoitwa chama cha mafisadi nawala sijakuwa mwanachama wa chama kinachoitwa chama cha mafisadi. Fikiria mambo kwa kutumia akili na wala siyo hisia. Hisia hupelekea kujenga hoja dhaifu.
 
Utasikia wapi chama kinachoitwa chama cha mafisadi na wewe unaishi katika nchi ya kusadikika!!! Hata muasisi wa CCM, Mwalimu Nyerere alishawahi kutamka kwamba CCM kimejaa wahuni na CCM siyo mama yake hivyo kulazimika kuendelea kuwa mwanachama wa chama cha mafisadi. Asingeona shida yoyote kuukana uanachama wa chama hicho ambacho kilianza kukiuka maadili ya chama hicho hata kabla Mwalimu hajafariki. Endelea kuishi kwenye nchi ya kusadikika ambayo kiongozi wake ana umahiri wa hali ya juu katika kutatua matatizo yaliyokuwepo. Yeyote anayefuatilia thread hii anajua ni yupi mwenye hoja dhaifu ya kusifia mediocre leaders.
 
IMF wakisifia tu Watanzania tupige makofi. IMF hawawezi kuijua Tanzania kuliko sisi wenyewe! Cha msingi cha kujiuliza ni mtu AKITHIBITIKA kwamba KAIBA; sheria zilizopo zinasemaje? Ndivyo alivyofanya Rais wetu ambaye ndiye MLINZI MKUU wa KATIBA yetu?
 
Nadhani sasa umepoteza dira, wewe umedai kuwa mimi ni mwanachama wa chama cha mafisadi. Nimekufahamisha kuwa hoja yako umeijenga kutokana na hisia kwani hunifahamu na huna ushahidi kwamba mimi ni mwanachama wa chama cha mafisadi. Zaidi ya hapo nikakueleza kuwa sijawahi kukisikia chama kinachoitwa chama cha mafisadi, sasa unataka nikueleze kitu gani ambacho mimi sikifahamu? Samahani kwa kutengua ubashiri na hisia zako kuwa ni za kufikirika na zisizokuwa na ukweli wowote. Please lete hoja za kweli na siyo za kupandikiza.
 
IMF wakisifia tu Watanzania tupige makofi. IMF hawawezi kuijua Tanzania kuliko sisi wenyewe! Cha msingi cha kujiuliza ni mtu AKITHIBITIKA kwamba KAIBA; sheria zilizopo zinasemaje? Ndivyo alivyofanya Rais wetu ambaye ndiye MLINZI MKUU wa KATIBA yetu?

Unahiyari unaweza kupiga ngumi ukutani!
 
Bubu ataka kusema,
Wewe siyo msemaji wa 'Watanzania wengi' hizo zako ni hisia tu na ambazo hazijengi hoja ya nguvu katika majadliano. Ukweli unabaki kuwa JK amefanya kazi yake vizuri na anastahili pongezi kwa hilo. Tatizo ambalo amelitatua ni tatizo la nchi na wala siyo tatizo lake binafsi. Huenda wale ambao haitakii mema nchi yetu walitaka kuona kuwa suala EPA haliishi na liendelee kuwa ni ajenda kila kukicha, tutafika kweli? JK is smart and Intelligent!

hata mimi naomba kusema sijaona chochote alichofanya JK ni mchezo mchafu tu, tunasifia kitu ambacho hatujaona result zake kama ni mtihani kafanya njia majibu hakuweka sasa kama wewe umeamua kusahihisha njia poa, sisi tunasahihisha njia na majibu, kati ya watu ninaokutana nao sijabahatika kusikia hata mmoja anayesifia ohh kwa siku nakutana na watanzania si chini ya 50, na 10 wapya mhh.... labda niwaulize na waganda...
 
kati ya watu ninaokutana nao sijabahatika kusikia hata mmoja anayesifia ohh

Una bahati mbaya, kwa msaada wa kuona nimekuwekea posting ya kwanza kabisa inajieleza, nadhani sasa utakuwa umepata bahati ya kuona wanaosifia juhudi hizo.

kwa siku nakutana na watanzania si chini ya 50, na 10 wapya mhh....

Hujaeleza ni watanzania gani, watoto wa KG au? Tuwekee hiyo list ya hao uliokutana nao tarehe na mahali na bila ya kusahau umri wao na genda. Ninasema hivyo kwani wewe umeonesha uko very specific kwa maana hiyo umefanya research, tuwekee data na siyo sentensi. Natanguliza shukrani.
 
Unahiyari unaweza kupiga ngumi ukutani!

Pundamilia,
Nilikuwa nakufuatilia kwa makini lakini umeniboa. Yaani unamjibu Wildcat hivyo? Mjibu kwa hoja kama unavyotaka wengine wajibu au wewe umetumwa kumtetea JK kwa ngawira kidogo sasa umechukia watu wooooote hawakuungi mkono?
 
Back
Top Bottom