Mikono yenye Sugu
Senior Member
- Jul 1, 2020
- 133
- 215
Pamoja na jeshi la polisi kujitwalia taswira mbaya machoni pa wapenda haki kwa kuonesha upendeleo wa wazi nyakati za nyuma, angalau tokea kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuuwa mwaka huu wameonesha kusimamia weledi na kutotumia maguvu yao kukandamiza washindani wa chama tawala.
Ingawa ni wajibu wao kufanya hivyo kwa mujibu washeria, hata hivyo wanastahili pongezi kwani Watanzania wana muda pasipo kushuhudia ustaarabu huo. Hatutegemei kuona ustaarabu huo ukiwa na ukomo.
Wapenda amani wana shauku ya kuona hali hiyo ikiwa endelevu ili kuweka uhalali wa ushindi kwa yeyote atakayeibuka kidedea kwa uchaguzi wa mwaka huu. Tunatamani kuona atakayeshindwa akikosa pa kushika kusingizia kuwa ameporwa kwa nguvu ya vyombo vya dola.
Kamanda Siro endelea kusimamia hilo, historia itakukumbuka kama mtumishi mwaminifu wa umma uliyesimamia vema nafasi yako.
MUNGU IBARIKI TANZANIA