Mnyika, Zitto waikaba koo CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, Zitto waikaba koo CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Feb 20, 2012.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WABUNGE machachari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Zitto Kabwe na John Mnyika, wamesema ni wakati muafaka kwa Watanzania kutafakati namna ya kuipumzisha CCM katika uongozi wa nchi katika uchaguzi ujao kutokana na hali mbaya ya uchumi na ya kimaisha.

  Wamesema serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete inalizamisha taifa kutokana na hali iliyopo sasa na kusema kuwa endapo haitafanya juhudi za dharura, hali inatakuwa mbaya zaidi.
  Akizungumza kwa nyakati tofauti jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Mombo, mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimtaka Rais Kikwete na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, kutoa kauli ya haraka juu ya mpango wa dharura wa kunusuru uchumi na kutatua tatizo la mfumko wa bei nchini.

  Mnyika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, alisema katika miaka zaidi ya sita ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania imekuwa ni ndoto ya kufikirika.
  Alisema wananchi walioichagua CCM kwa kurubuniwa na mbinu chafu, kama kuhongwa vyakula, fulana, kofia, sasa wanavuna matunda ya chaguo lao na kuwataka kutumia muda huu kutafakari upya.

  "Tumekuja Tanga mwaka huu, ikiwa ni moja ya nafasi ya kutekeleza tamko la Katibu Mkuu, Dk. Slaa, kuwa moja ya kipaumbele chetu mwaka huu ni kunusuru uchumi wa nchi na kukabiliana na gharama za maisha. Tunaitaka serikali kushughulikia vipaumbele ambavyo tumewaonyesha, kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira, ikiwa ni sehemu ya kudhibiti mfumko wa bei," alisema Mnyika.

  Aliongeza kuwa kutokana na tamko hilo, wabunge wa CHADEMA kila mmoja kwa nafasi yake, anasimamia hoja hizo za kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira, hali iliyomfanya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kuwasilisha hoja binafsi ya Mkonge, ambayo inalenga kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira katika kilimo.

  Alisema licha ya Zitto kuipeleka hoja hiyo kwa maslahi ya wakazi na wakulima wa Tanga, wabunge wa CCM wa mkoa huo waliipinga kwa kile walichoona Watanzania wakiondokana na umaskini nafasi yao ya kuwarubuni itakuwa mashakani.

  Akizungumzia viwanda, Mnyika alisema CCM badala ya kufanya ubinafsishaji wamefanya ubinafsi wa viwanda na kutolea mfano Kiwanda cha Tembo Chipboard, ambacho kilikuwa kikipata malighafi kutoka msitu wa Shume, lakini kutokana na sera mbovu na mipango mibovu, uzalishaji umedumaa na kiwanda kimefungwa.

  Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto, alisema kuwa hali ya maisha ni ngumu na inatishia uhai na usalama wa nchi kwa kuwa katika njaa maradhi na umaskini uliokithiri ustaarabu unakosa nafasi.

  Aliongeza baada ya Bunge kuikataa hoja binafsi kuhusu zao la mkonge, ni wajibu wa wananchi hao kuwakataa viongozi wasiowatetea kwa vitendo na hata katika masanduku ya kura pindi watakapojitokeza kuomba nafasi za kuwaongoza.
  Awali wananchi wa mji wa Mombo walizuia msafara wa Zitto na kuutaka ufike katika mashamba yao wakashuhudie kile ambacho wabunge wa mkoa wa Tanga waliudanganya umma kuwa zao la mkonge haliwezi kuwakomboa kimaisha.

  Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mashamba ya Mkonge ya Mwelya, Fredrick Malika, wananchi hao walisema katika heka moja wana uhakika wa kupata sh 800,000.

  Awali Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), aliwaahidi wastaafu wa kiwanda cha mbao cha Mkata Saw Mils kufuatilia malipo yao ambayo hawajalipwa tangu walipostaafishwa.

  Akizungumza katika mkutano ya hadhara mjini Mkata akiwa katika ziara ya siku tano mkoani Tanga, Zitto alisema atafuatilia serikalini kujua kama mwekezaji alifuata masharti ya kununua kiwanda hicho na kama uuzwaji uliangalia maslahi ya wafanyakazi.

  Nimeitoa:http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=33182
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Huko chadema mnapenda kujikosha.ile skendo ya NSSF imeishia wapi
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Great Move sawa manake wanasema kazi yenu ni kulalamika ,Nimependa ya Mnyika kila mtu atatafuta mbinu ya ajira kwa wananchi na kuisemea vizuri
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na wewe una hoja?
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  majembe kazini.

  limeni popote katika ardhi tuliyopewa na mwenyezi mungu ikiwa na utajiri kibao lakini kuna watz wenzetu wanauza kwa wajeni kwa kibaba cha uji.

  vizazi vitawakumbuka kwa hii kazi iliyotukuka mliyoamua kuifanya na mungu atawalipa.
   
 6. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Amina.
   
 7. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Yap hii ndio chadema mkombozi wa wanyonge' magamba hoi na bado 2015 patachimbika2 na endapo mtachakachua tena kura zetu wanacdm, mjue 2tawavua madaraka kwa lazima na hata kama itakuwa kinyume cha sheria sisi hatutajali hivyo kwani tumeshachoka na kuwachagua magamba wanokwenda kutetea posho na kuunga mkono hoja kwa asilimia% hata kama ni miswada ya kipumbavu.
   
 8. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Zitto endelea kufanya kazi iliyotukuka mpaka saed kubenea atubie dhambi ya kukuchafua kwa miaka mi nne mfululizo bila ya mafanikio,matokeo ya kazi zako hata wabaya wako Chadema wameanza wameanza kuiona!!!
   
 9. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,464
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Dah... Ndo shida ya interest ya vyama hii. Issue ni kuwakomboa wanananchi wa Tanga ambao Mkonge umekuwa hauna msaada wowote kwao.. Tuweke kando maswalahi ya chama na tujenge Tanzania kama wanavyofanya hawa Makamanda.
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  dah! Mi nadhani we ni boyfrend wa MWANAASHA koz hata akili zako 2 zinajieleza trgh your opinions!
   
 11. S

  SKY TP Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi nzuri na nawapapongezi kwa jitihada zenu za kutaka watanzania siku moja wawe na maisha mazuri. kwani mmekuwa mkiwasaidia hawa ccm ili kupitia ninyi waweze rudisha imani yao kwa wananchi juu ya yale waliokuwa wakijitapa kuwa watabolesha maisha y kila mtanzania lakini kinyume chake wamekuwa wakijifanya hilo hawalioni. mimi nawambia njia ya mwongo ni fupi na ipo cku ambayo inakuja ya mwaka 2015 itakavyokujawadabisha. CHADEMA endelehen kujipanga kila cku hasa juu ya suala zima la kuwawezesha wananchi wawezekuondokana na umasikini. MNYIKA, ZITO PONGEZI SANAAAA......
   
 12. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Hamna kitu hapo wakuu.Zitto anatupiga changa la macho.Issue hii ya mashamba ya mkonge aliitoa bungeni kama hoja binafsi ambayo siyo Mnyika au viongozi wake wengine walikuwa wanaifahamu.Tetesi ni kwamba alitumwa na mbunge mmoja tajiri wa CCM mwenye asili ya kiarabu ambaye anaendesha kampuni flani jijini DAR kusambaza mambo ya vyakula maji,mafuta nk,na wanamashamba mengi mnoo kila kona ya nchi.kwamba huyu jamaa baada ya kujaribu bila mafanikio kujimilikisha na kunyanganya wakulima wadogowadogo mashamba yao ili alime mkonge akaamua kumtuma zito aiingize bungeni ili apate support pia ionekane ni issue yenye maslahi kwa wananchi wakati ni kwa maslahi yake mwenyewe.ndio maana pia zito aliitoa kama hoja binafsi.baada ya kuona watu walishashtukia lengo lake kajaribu kumuingiza Mnyika ili kupotezea.sijawahi kumsikia kiongozi yeyote wa CDM beside Zitto ambaye ameigusia hoja hiyo ya mkonge.kuna issue za muhimu ambazo zinatugusa wananchi Zitto alitakiwa kuzipigania kama suala la muswada wa katiba.sio suala la mkonge ambalo sidhani kama lina umuhimu kwa manufaa ya wananchi wote.mbona katiba wakati wenzake wanapigania kubadilisha ule muswada yeye zitto alikuwa kimyaaaa kama hayupo vile.baada ya viongozi wenzake kufanikiwa kumshawishi Mh Jakaya ndio zitto akajitokeza na kudai ile idea aliitoa yeye kupitia kwa marehemu Regia.Behind the scene kwenye hoja yake ya mkonge inajulikana,kwamba mtu aliyetoa pesa kuhonga ili issue ya mkonge ipatiwe attention na kufanya raia waamini kama ni suala la maslahi ya taifa pia anajulikana.kama ni suala la kufufua mazao ya biashara mbona simwoni simwoni zitto akiongelea mazao mengine kama kahawa,tumbaku,karafuu nk?kwanini afunge mpaka safari kwenda kufanya mkutano wa hadhara tanga kwaajili ya kutetea mkonge.Mkonge ungekuwa unalimwa jimboni kwake atleast ingemake sense kwamba wale wakazi wa jimbo lake wangefaidika na ajira nk.Wakuu sisi ndio wadanganywa lakini kwa mwenye macho haambiwi tazama.Positivity and much blessings!
   
 13. A

  Ahakiz Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe tetesi huna ushahidi sasa hayo mashamba mwarabu atachukuaje?
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  nakukumbusha hapa tunajadili hoja ya mh.Zitto na Mnyika juu ya ufufuaji wa zao la mkonge na uchumi kwa jumla sasa wewe unaibua hoja mpya ya NSSF.kama unataka iandikie thread yake ili wanajamvi waijadili unajua hata kama wewe ni mjinga sio lazima kuuonyesha ujinga wako kwa kila mtu,.jadili mada usijadili mtu!!kama kuna kashfa unajua iweke wazi na vielelezo ijadiliwe!!
   
 15. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo
  Hakika mnategemewa na Watanzania!
   
 16. e

  elementary Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  hakika umemdadavulia vyema ss 2subilie ujinga wake vzr.
   
 17. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ili chama kionekane makini ni pale kinapotetea maslahi ya wananchi wanyonge,
  Suala la ufufuaji mashamba ya mkonge na biashara yake, ingawasaidia sana waTZ mafukara waliokata tamaa,
  Kwa hili CHADEMA, kweli Mungu atawapigania kwa jinsi mnavyoweza kuonesha nia ya kweli ya kumtetea huyu mnyonge!
  Na Mungu aliye juu awabariki. Amen.
   
 18. e

  elementary Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  anyway, kwng mm hoja n ya msingi coz inagusa maisha ya watu, kwa wale wasioipenda bac ccti kuwaita magamba yaliyoishia kiunoni.
   
Loading...